Monday, March 20, 2023
Ukifanya hiki utajitoa kwenye mazoea
Saturday, March 18, 2023
Usichoke, ndiyo maisha yetu
Friday, March 17, 2023
Nini kinafanya wakuchague?
Thursday, March 16, 2023
Nguvu ya jina la kwanza
Monday, March 13, 2023
Unaweza kushinda mchezo wowote
Saturday, March 11, 2023
Mabadiliko yanaanza na wewe
Wednesday, March 08, 2023
Ni kidogo lakini kinampa faraja
Tuesday, March 07, 2023
Hiki ndicho huvunja uaminifu
Monday, March 06, 2023
Uwezo wako wa ushawishi umefichwa huku
Sunday, March 05, 2023
Maono na uwezekano
Saturday, March 04, 2023
Hii ndiyo sababu inayofanya usahau ulichojifunza
Friday, March 03, 2023
Tushirikiane sisi ni wamoja
Nilipata hamasa zaidi niliposoma hadithi inayosema kuwa:
"Kwenye Shule moja kulikuwa na kundi la wanafunzi watukutu ambao walikuwa wakionea wanafunzi wenzao. Wanafunzi hao walikuwa wakikuta mwanafunzi mwingine wanamlazimisha achague wa kupigana naye na akikataa wanampiga wote.
Siku moja kundi hili walikutana na mwanafunzi mmoja aliyeonekana kuwa mnyonge sana. Wakamwambia achague wa kupigana naye. Yule mwanafunzi akachora mstari na kusema yule ambaye anajiona ndio mbabe kuliko wote avuke huu mstari. Yule ambaye ndio alikuwa mbabe alivuka mstari ule na alipofika upande wa pili yule mwanafunzi mnyonge alimwambia sasa tupo upande mmoja, tuungane kupambana na hao wengine. Yule mbabe akakubali wakaliamsha kuwapiga wengine".
Unaweza kuona ni usaliti lakini sio kweli huyu mnyonge alimwambia neno la msingi. Huenda mtoto mbabe hakuwahi kulisikia. Maisha yeke yote aliishi kupigana na kushindana. Lakini alipoambiwa "tupo upande mmoja, hivyo tuungane pamoja". Aliona kuna jambo la msingi.
Hata maisha yetu ndivyo yalivyo. Mnapokuwa upande mmoja mnapaswa kuwa wamoja. Kushirikiana, kushauriana na kushirikishana katika masuala mbalimbali ya maendeleo.Bila kusahau watu wote wanaokuzunguka. Hao mpo nao upande mmoja. Ni vema kusaidiana na kushirikishana.
Tatizo ni kwamba wengi wetu hatuelewi hii dhana ya umoja. Ndio maana tumekuwa tunashindana lakini hatufiki mbali.
Mfano. Kama wanandoa wangejua kwamba wapo upande mmoja, wa kutaka maisha yao wote kuwa bora basi matatizo mengi sana ya ndoa yasingekuwepo na ndoa zingedumu. Lakini baadhi ya familia, unakuta mme anashindana na mke wake. Wakati mwingine mke anamuibia mali mme wake. Inashangaza sana.
Mwajiri na mwajiriwa hawa wote wapo upande mmoja. Kila mmoja yupo kunufaisha kazi yao na maisha yao kwa ujumla. Lakini mambo ni tofauti huyu anamkwaza na kumkandamiza mwenzake mara anamuibia. Vitu vya kushangaza vinafanyika.
Nashangaa kwanini tunafikiri kwamba tuko pande tofauti na hivyo kuishia kushindana, mashindano ambayo hayamfaidishi hata mmoja wetu. Mke na mme kushindana, kuibiana. Mtu na mdogo wake kunyanyasana, kutesana na kuibiana. Inashangaza sana.
Wakati ndio huu. Tushirikiane sisi ni wamoja. Tuache ushindani. Baba na mama jenga familia bora. Mwajiri na mwajiriwa ikuze taasisi yenu kupitia umoja. Hakika mtafanikiwa.
Je, nini kinazuia maendeleo yako?
Bonga nasi 0767702659
Imeandaliwa na Lackius Robert
#33mwangaza2023
Thursday, March 02, 2023
Jifunze Ushirikishe
Wednesday, March 01, 2023
Fanya kinachowezekana
Tuesday, February 28, 2023
Hiki ndicho kinachotupoteza
Monday, February 27, 2023
Juhudi na uvumilivu
Sunday, February 26, 2023
Jipongeze mwenyewe
Saturday, February 25, 2023
Furahi zaidi leo
Friday, February 24, 2023
Tunategemeana ili maisha yaende
Thursday, February 23, 2023
Huku ndipo nguvu zako uanzia
Umewahi kumuona Paka katika sehemu zenye taabu. Ikiwa na maana kwenye jua kali, moto mkali au sehemu hatarishi. Jibu ni hapana. Unataka kujua kwa nini? Twende pamoja.
Tupo katika dunia yenye changamoto nyingi zaidi. Kadri muda unavyozidi kwenda mbele ndivyo zinavyozidi kuongezeka. Kuongezeka kwa changamoto hizi kumewafanya baadhi yetu kukosa utulivu.
Hii imewafanya kila mara wapatapo changamoto kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii kupost n.k. Nia yao kuu ilikiwa ni kupata msaada juu ya magumu yanayowakabili. Matokeo yake imekuwa tofauti na kufanya mfadhaiko kwao kuzidi kuwa mkubwa.
Wanachoshindwa kujua ni kuwa mitandao ya kijamii haiwezi kutatua kila tatizo. Kwa sababu kule unakutana na watu wengine wenye matatizo. Hivyo, tatizo linazidi kuwa sugu. Na kinachoongeza uzito ni kule kusemwa au kusimangwa ambako mtu hukutana nako kwenye mitandao.
Siku ya leo nimekuja na njia mpya kukusaidia kutatua changamoto hiyo. Ukumbuke hapo juu nimeanza kukuuliza swali kuhusu Paka. Namna anavyopenda starehe na kukataa maisha ya shida. Utamkuta amekaa kwenye kochi ametulia. Amekaa kivulini uvunguni mwa gari. Amekaa sehemu ya upepo safi na tulivu. Lengo kuu ni kuponya majeraha anayokutana nayo katika harakati zake za utafutaji wa chakula.
Kwetu binadamu sehemu inayoenda kuwa baraka kwetu ni sehemu yenye utulivu kwa maana ya faragha. Huko ndiko nguvu zinakotoka. Maana unapata nafasi ya kutafakari kwa kina juu ya hali mbalimbali unazopitia katika maisha yako.
Kuna wakati tunaona kama tuna changamoto lakini unapopata muda wa kutafakari utagundua vitu vingi. Uwezekano wa vitu unaanzia kwenye fikra. Akili yako itakuwa na uwezo mkubwa wa kuwaza vitu na kutafuta suluhu. Una changamoto ya mauzo, ndoa, mahusiano au kazini. Tafuta eneo tulivu utulie kisha ujitakafari zaidi. Mara zote ikumbuke hii "tenga muda wa kufikiri kwa sababu ndipo kuna chanzo kikubwa cha nguvu zako"
Je, uko tayari kutafuta nguvu hizo? Bonga nasi hapa hapa 0767702659
Lackius Robert
#27mwangaza2023
Wednesday, February 22, 2023
Sikiliza ila fanya kinachofaa...
Tuesday, February 21, 2023
Inuka, unayo nafasi
Monday, February 20, 2023
Usiangaike na maneno yao...
Kwenye maisha, watu wanayo nafasi ya kuamua kulingana na wanavyoona. Iwe ni sahihi au sio sahihi. Wanakuwa wanaamini wanachokisema kwa asilimia mia moja.
Inapotokea wewe ukawapinga inakuwa ngumu kukuelewe. Maana tayari kipo kitu wanakiamini kutoka kwao. Unachotakiwa kuzingatia ni yale unayoona yanafaa.
Ndio maana huwa ninasema mara zote wewe amua upande unaotaka. Maana ukifanya wanasema, usipofanya wanasema na ukiacha watasema pia. Pale unapoona panafaa ingia upande huo. Kisha fanya kinachowezekana kufanyika.
Wanakusema sio kwamba unakosea bali kuna hatua kubwa wanaona unaenda kuipiga. Hiyo, ndio inayowafanya wanakusema. Ukiweka nguvu kuyasikia maneno yao itakuwa ni ngumu kuendelea.
Hata wale walio karibu yako huwezi kuwazuia kusema. Nao watasema kulingana na namna wanavyoona inawafaa.
Wakati mwingine hata ukifa bado watasema kuwa fulani alikuwa hivi ama vile. Wajibu wako kama mtu unayetaka kufanikiwa kuweka nguvu kwenye kazi zako.
Huenda unajiuliza maswali, ufanye nini sasa?
Maana ukweli ndiyo huo kuwa, watu lazima watakusema iwe unafanya au hufanyi. Watasema bila kuwa na wasiwasi wowote.
Nakushauri, usiangaike na maneno ya watu juu yako. Usiangaike weka nguvu kwenye kazi zako. Fuata moyo wako kwa kile unachotaka kufanya. Pia, fuata ushauri huu wa aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Winston Churchill aliwahi kunukuliwa akisema,“Kwa muda mrefu Sasa nimeacha kuwasikiliza watu, badala yake naangalia kile wanachofanya. Tabia ndiyo ukweli pekee.”
Hutawazuia kusema ila unaweza kujizuia kufanyia kazi yale yasio mazuri kwako.
Imeandaliwa na Lackius Robert
0767702659
#25mwangaza2023
Sunday, February 19, 2023
Hiki ndicho hupoteza nguvu zako
Saturday, February 18, 2023
Umuhimu wa kuwa Orodha ya Vitu vya kufanya(To do list)
Friday, February 17, 2023
Uchambuzi wa Kitabu Cha Where There is a Problem There is Money...
Thursday, February 16, 2023
Unajua nini kuhusu?....
Wednesday, February 15, 2023
Usifuate mkumbo..
Tuesday, February 14, 2023
Jinsi kitabu cha Think and Grow Rich kilivyokuza shauku yangu
Monday, February 13, 2023
Njaa waliyonayo wengi wetu...
Sunday, February 12, 2023
Huwezi kukwepa ujasiri
Saturday, February 11, 2023
Moja inakutosha?
Ni swali ambalo nilimuuliza, mmoja wa watu naowafanyia training kwenye program zangu. Yeye yupo kwenye mauzo kwa maana ya biashara. Nilihitaji apate pia, huduma nyingine kati ya ninazotoa.
Kabla hajaanza program aliniambia, ndoto yake kuu ni kuwa muuzaji bora. Kuongeza ushawishi mkubwa katika biashara yake. Kuna vitu vingi alinielezea vinampa shida. Nikamwambia "mauzo sio kitu cha siku moja bali ni kitu chenye mkusanyiko wa vitu vingi ikiwemo kujifunza kila siku".
Ni mengi tuliongea lakini, moja ninalotaka kukushirikisha leo ni hili. Limekaa kama swali lakini lina nguvu kubwa unapomwambia mteja.
Ni kweli program aliyokuwa anataka nilimpatia. Lakini kwa kuwa zipo nyingine, sikusubiri aulize baada ya kukubali ya kwanza. Nilimuuliza hilo swali. Akashaangaa kidogo, baadaye akasema kama ipo nyingine inayoendana na hii nipe Kaka.
Mpaka sasa amekuwa akilitumia mara nyingi zaidi katika hudhma zake.
Sasa wauzaji wengi wamekuwa hawalitumii mara baada ya kumuuzia mteja. Tafiti zinaonyesha ukilifanyia kazi kwa wateja wengi wapo wachache utawafanikisha.
Ipo hivi pale unapokuwa umemuuzia mteja kitu. Au unazo huduma labda za mafunzo unazitoa. Mteja akaja na kuhitaji bidhaa moja. Usisubiri hadi akwambie nataka kitu kingine. Wewe muulize je, moja inakutosha?
Unapokuwa umemuuliza hili maana yake yeye atakwambia ikiwa anahitaji au la. Epuka kujipa majibu. Wewe kazi yako ni moja. Na swali hilo ni je, moja inakutosha. Wewe mwambie kila anayekuja kupata huduma kwako.
Mfano unafanya uandishi, tafsiri na printing. Mteja akihitaji huduma ya kuandikiwa mwambie moja inakutosha. Ikiwa na maana mpatie huduma nyingine.
Point yangu ni kwamba, wewe timiza wajibu kumuuliza hilo swali. Kila mteja unayekutana naye katika huduma yako. Usiache akachukua huduma yako bila kumuuliza.
Tahadhari: Usimuulize kabla hajafanya mauzo. Subiri akamilishe mauzo ndipo umuulize. Ili umhudumie zaidi.
Na mimi nakuuliza ndugu yangu mpendwa. Makala hii inakutosha?
Bonga nasi hapa hapa
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#16mwangaza2023.
Friday, February 10, 2023
Ungepita njia hii?
Ilikuwa majira ya asubuhi, Rama akiwa anaendesha gari kuelekea kazini. Ni muda ambo alikuwa anawahi kazini kwenye kikao na wakurugenzi. Rama alikuwa anaendesha gari alilopewa na ofisi ili kuongeza ufanisi kwake ikiwemo kuwahi kazini.
Siku hii kulinyesha mvua kiasi. Baadhi ha njia zikawa na foleni. Sasa wakati Rama aneendesha alifika sehemu iliyomshangaza kidogo....
Ukiachana na Main Road kulikuwa na njia ya chocho, ambayo magari mengi yalikuwa yanapita. Huku nyingine hakuna gari lolote lililokuwa linapita. Akajiuliza sababu na kuikosa. Na jana yake wakati anatoka kazini ndiko alikopitia. Rama akaanza kujiuliza juu ya nini afanye. Awafuate wengine au ajitose kwenye njia ya peke yake.
Wakati anawaza zikaja gari nne nyuma yake na zote zikapita kwenye njia nyingine ya chocho. Kwa kuwa aliona magari yote yanapita katika njia hiyo. Bila kuuliza na yeye akaamua kuungana nao. Dakika chache baadaye simu ikaita bosi wake anauliza kama amefika.
Rama: Helow! Boss!huki akiwa ameshika kichwa afanye nini, kule alikoingia gari nyingi hawezi kutoka tena. Njia ni ndogo. Kwa sababu kila mtu alikuwa anapita katika njia hiyo.
Bosi: Uko wapi kijana wangu?
Rama: Mhh! Yaani! Unajua Bobosii! Nipo hapa sio mbali na barabara kuu. Kuna chocho tumeingia kuna msongamano wa magari.
Boai: Msongamano wa magari? Mhh mbona dakika chacha nimetoka huko hamna foleni.
Rama:Sasa kilichotokea, nilifika kwenye kinjia pale kati nikaona watu wote wanapita nikaacha Main Road nikaunga. Japo niliwaza kitu kama hicho kukazania main road. Ila baadaye nikaona magari mengi yanapita njia hii nikaliunga. Kwa hiyo tunafanyaje bosi? Bosi: Nadhani huu mradi tushaukosa ila wewe ndio responsible.
Ndio maana tulikupa gari ili uwahi. Ni nini umefanya? Muda wa kikao umefika.
Rama: Mhhh hapana bosi..je, naweza kukuuliza? Boss ndio kijana wangu.
Rama: Ingekuwa ni wewe, unaona watu wote wanapita njia ya chocho. Huku Main Road hakuna anayeendelea kwenda mbele ungepita njia hii?
Bosi:Mhh ngoja kwanza nimeitwa ntakucheki baadaye.
Rama: Helow Boss Helow boss.
Sime imekatwa. Hakuweza kutoa jibu.
Sasa kwako mpendwa msomaji. Ingekuwa ni wewe ungepita njia hii?
Nini tunajifunza?
Kwanza hapo juu bosi alikata simu. Kwanini alikata simu? Swali aliloulizwa na Rama lilimpa utata sana. Aliona mazingira yalivyo. Ili kuyaepuka akakata simu.
Ila Rama hakuuliza kujua kwa nini njia kuu haipitwi na hakuna kibao kinachoonyesha njia imezuiwa. Hivi ndivyo tunavyokutana na vishawishi maishani mwetu.
Kumbe, kwenye maisha kila mtu anazo njia zake. Anayo safari yake. Anayo matarajio yake. Ikiwa huna yako, jua utaenda kukamilisha ya wengine.
Chocho lako lipo katika kazi zako, familia yako, biashara yako. Lakini ili uyashinde yote haya. Baki njia kuu. Wengi wanapenda sana njia za mkato. Na unapofika kule kujitoa sio kazi ndogo.
Wakati ndio huu kubaki katika njia kuu ambayo wengi wanaikataa. Ni njia iliyowazi kumfanye yeyote aliyejipanga kufikia hatma ya safari yake. Karibu tupite wote njia kuu.
Mungu akubariki sana. Karibu tujifunze zaidi.
Bonga nasi hapa hapa
Imeandaliwa na Lackius Robert. 0767702659
Mwangaza2023
Thursday, February 09, 2023
Siku yako inalipa?
Kila siku huwa inanza tofauti. Fikra, hamasa au motisha ya jana huwezi kuifananisha na leo. Pata picha ni siku mpya imefika huku ukiwa huna mpango au ratiba yoyote. Ni nini kinakujia kwa haraka haraka akilini? Na unaionaje siku hiyo? Hakika jibu linachanganya sana.
Kwa lugha nyepesi lolote litakalotokea kwako litakuwa kipaumbele. Na utaliona lina uzito. Kwa sababu hakuna mbadala wake. Mwisho wa siku utagundua siku yako imekuwa ngumu, ndefu na imebana sana.
Upande wa uzalishaji au matokeo utaona hayaridishi. Mengi yamefanyika, safari nyingi zimefanyika. Lakini tija ni kidogo. Kwa nini uligusa kila kilichokuja mbele yako. Kukianza litakuwa suala moja kukimaliza nalo pia litakuwa lingine. Na utaona ni sawa maana hamna mpangilio wowote unaokuongoza. Na itakuwa ni ngumu kufanya tathimini kwa kuwa huna mwongozo..
Hayo siyo maisha unayopaswa kuyaishi ndugu yangu mpendwa. Weka nguvu kubwa katika kuwa na mipango(to do list) kuendana na kile unachofanya. Kupitia mipango yako ndipo utaweka vipaumbele. Kwa maana ya kipi kianze na kipi kifuate.
Natumaini umewahi kuisikia kanuni ya Pareto ya 80/20. Ikisema asilimia 80 ya matokeo unayopata yanatokana na asilimia 20 za juhudi zako. Hapo unaweza kuona, ukifanya vitu vichache vyenye tija vinaweza kukusaidia kupata matokeo makubwa. Kuliko kufanya vitu vingi visivyokuwa na tija. Swali la kujiuliza ni je, inalipa? Kile unachofanya kinachangia nini kufanikisha vipaombele vyako? Ikiwa ni hapana kiweke pembeni. Kama ni ndio hongera. Kifanyie kazi tena kwa upendo mkubwa.
Hujachelewa, wakati ndio huu. Ipangilie vema siku yako, ili ikusaidie kufikia ndoto kubwa za maisha yako. "Ikiwa huna kitu, usiogope kwa unachokipoteza".
Je, ni nini ungependa tukusaidie katika kuweka mipango au vipaombele?
Bonga nasi hapa hapa
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#1mwangaza2023
Wednesday, February 08, 2023
Unavyoitafsiri dunia sivyo..
Unavyoitafsiri dunia sivyo...
Mafanikio yako yapo katika kile kitu unachotaka kuwa au kufanya. Na sio anachofanya mtu mwingine. Kama unataka kuwa mtu wakuandika unapaswa kuyaishi maisha hayo. Kama wewe ni mfanya biashara na ndiyo maisha unayoyataka, basi unapaswa kuishi katika hali hiyo. Na sio kwamba waimbaji, wachezaji au walimu ndio hufanikiwa.
Maana kitu unachokiwekea nguvu na kukifanya kila siku ndicho kinachokufanya uwe na amani na furaha.
Kama wewe ni mtu wa kuimba ukiishi mziki na ukaishi maisha ya uchezaji mpira kuna kitu kwenye maisha yako hakitaenda sawa. Yaani hutopata matokeo mazuri. Kuna kimoja kitakuwa na matokeo mazuri kuliko kingine.
Ili uweze kuwa mtu wa mafanikio unapaswa kuyaishi maisha ya kitu unachotaka au unachofanya. Ikiwa umeona kinaweza kukuvusha. Weka nguvu katika kitu hicho. Fanya kinachowezekana kukifanikisha. Jifunze na kuwapenda watu waliofanikiwa na kitu hicho. Tofauti na hapo hutofanikiwa.Usiache pia, maeneo mengine kufuatilia na kujifunza zaidi.
Katika maisha yangu nimejifunza kuwa; ili uweze kufanikiwa unahitaji kitu kimoja kwanza. Ambacho kitakuvusha kutoka sehemu moja hadi nyingine. Yaani iwe mchana au usiku. Wakati na masika wakati wa kiangazi. Unakifanya kweli kweli. Kila unapoamka asubuhi fanya kile kitu ulichochagua. Mfano angalia "Google" inahusu "search" kwa maana ya kutafuta. Wao waliwekeza hapo. Na ndiyo kilichowavusha waanzilishi. Angalia Apple, Amazon na zingine.
Kwani ukiamka asubuhi mipango yako inahusu kitu ulichochagua? Na vipi kuhusu ratiba zako? Mizunguko yako na watu wako wa karibu?
Kama huwezi kufanyia kazi kitu unachokitaka kwa kujituma mafanikio utayasikia kwa watu. Na hapo utabakia na tafsiri yako kwamba; dunia ni ngumu au maisha ni magumu. Kumbe ugumu unauweka wewe. Kwa lugha nyingine wewe mwenyewe ndiye unayejizuia. Ukifanya kazi zako kwa bidii kila siku na ukatumia muda wako vizuri maisha yako yatabadilika na kuwa mazuri.
Swali: Kitu kipi kimoja unakifanya bora kuliko kingine?
Bonga nasi hapa hapa
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#13mwangaza2023.
Tuesday, February 07, 2023
Ni siku nzuri au mbaya kwako?
Ni swali unalopaswa kujiuliza kila mara uamkapo asubuhi. Maana namna unavyoanza siku yako ni kiashiria tosha kuwa itakuwa nzuri au mbaya. Unaweza kuanza na maombi, tahajudi au mazoezi, kusoma kitabu au kusikiliza redio au mafundisho mazuri yenye hamasa chanya. Kutenga muda asubuhi kujifunza kitu ni muhimu sana, maana itakupa nguvu na kuiangaza siku yako. Japo baadhi yetu hatufanyi hivyo.
Mwingine ukimwambia kuhusu maombi ya asubuhi, kumshukuru Mungu kwa kumpa nafasi kuona siku nyingine, anaona kama unampotezea muda. Lakini ni muhimu sana kwa mtu mwenye maono makubwa. Muda wa asubuhi ni mzuri sana kupangilia ratiba zako. Hasa hasa baada ya kuwa umepata hamasa kupitia vitu mbalimbali. Binafsi mawazo mengi mazuri huwa ninayapata asubuhi. Hii ni kwa sababu akili yako inakuwa mpya ina nguvu haijavurugwa na kitu chochote, ukiachana na ndoto za usiku.
Najua umewahi kusikia msemo huu; “umenikuta na akili zangu za asubuhi”. Maana yake umenikuta nipo timamu, sijapigwa na jua, kuvurugwa na usafiri, baba mwenye nyumba au bosi wangu kazini. Akili inakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria.
Watu wengi waliofanikiwa huwa wanatumia sana muda wao wa asubuhi kupangilia ratiba za siku zao. Katika hili sio lazima utumie muda mwingi sana. Oh! Et masaa manne au matatu. Unaweza kutenga hata dakika 30 au zaidi pengine saa moja kulingana na unavyotaka wewe. Labda kuanzia saa kumi hadi saa kumi na moja asubuhi, au saa kumi na moja asubuhi hadi saa kumi na mbili asubuhi. Wewe tu kulingana na uchaguzi wako.
Safari ya maili elfu moja huwa inaanza hatua moja. Mafanikio ya wiki, mwezi au mwaka, vyote hujengwa kuanzia siku moja. Ambayo ndio kama hii uliyoamka asubuhi ya leo.
Yule unayemuona amefikisha miaka mia moja alianza na siku moja. Aliye juu ya mlima hajaibuka tu kupanda mlima, bali alijipanga na kufanya mazoezi aliyokuwa anafanya kwa siku moja. Mchezaji maarufu alianza na mazoezi ya siku moja. Mwandishi maarufu kadharika na wengine.
Leo ni leo amua ufanye kitu. Hakika lilo jambo utalibadili. Ikiwa kuna changamoto tuwasiliane 0767702659.
Mimi nimeanza na hii ☝️ wewe je?
Bonga nasi hapa hapa...
Imeandaliwa na Lackius Robert
#12mwangaza2023.
Monday, February 06, 2023
Hivi sivyo hukutoa kwenye dira?
Hivi sivyo hukutoa kwenye dira?
Ebu chukulia mfano kwenye hosptali Daktari amshafishe mgonjwa, amsikilize, apige simu na wakati huo amhudumie mtu mwingine kwa kumpatia madawa. Baada ya hapo afanye ukaguzi wa list ya malipo yanayopaswa kufanyika. Daktari huyo huyo awafuatilie wagonjwa wengine wanaosubiri huduma. Kwa hali yoyote lazima atafanya makosa kwa mmoja au kukosea kwa wote, either katika kutoa dawa zisizo sahihi au kushindwa kumuosha vizuri mgonjwa mwingine.
Halikadharika sisi, Kila wakati tunapokuwa tunafanya kitu zaidi ya kimoja tunakuwa tunagawanya mazingatio yetu au nguvu zetu. Katika sehemu nyingi. Hali inayotupeleka nje ya dira yetu. Ni sawa na ule msemo wa “huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja”. Ikiwa hutawakosa wote bali utamkosea mmoja na kumfanyia usahihi mwingine.
Utafiti uliowahi kufanywa na taasisi moja ulionesha matokeo ambayo mtu anayefanya kazi nyingi kwa wakati mmoja anaweza kuyapata;
i. Kupoteza ufanisi. Yaani hapa kazi yako inakuwa haina ubora ule unaotakiwa. Maana nguvu zinaenda katika vitu vingi ndani ya muda mmoja.
ii.Kadri unavyotumia muda mwingi kufanya zaidi ya kitu kimoja ndivyo unavyopata matokeo kidogo maana hujaweka nguvu kwenye kitu kimoja.
iii. Unapoteza zaidi ya asimilia 28% kufanya vitu ambavyo vinapunguza ubora na ufanisi wetu. Pale ambapo unakuwa unafanya vitu vingi kwa wakati mmoja.
iv. Muda unaoutumia ni mwingi kulingana na kitu husika. Badala ya kufanya kitu kimoja kwa wakati ukakimaliza unaenda kufanya kitu kingine. Wewe unafanya vyote kwa pamoja kitu kinachopelekea kuchelewa kumaliza kwa wakati.
v. Makosa. Watu wanaofanya kazi nyingi kwa wakati mmoja ni rahisi kukosea au kufanya makosa mengi
kuliko wale wanaofanya vitu vichache vya msingi.
vi. Msongo wa mawazo (stress) watu wanaofanya kazi nyingi kwa wakati mmoja wanasumbuliwa sana
na msongo wa mawazo maana vitu vingi wanakuwa hawajavimaliza kwa wakati. Anawaza hiki mara kingine kinamjia. Yote hayo yakiungana yanatengeneza kitu kinachoitwa stress ambayo hupoteza furaha ya mhusika.
Zingatia hizi big idea;
1.Usijisikie vibaya ukutanapo na miingiliano yaani distraction maana kila mtu anakutana navyo. Wewe weka nguvu katika vitu vichache vya muhimu kuzingatia dira yako.
2.Usiruhusu miingiliano itawale kazi zako maana inapoteza concentration, furaha na vitu vinginevyo.
Kufanya vitu vingi inawezekana lakini haviwezi kuwa na ufanisi mzuri chagua kitu kimoja kifanye vizuri. Kisha fanya kingine au tenga muda. Vipe nafasi kulingana na uharaka lakini sio kwa wakati mmoja ili usitoke nje ya dira yako. Lengo kuu ni kutotoka nje ya dira yako na kuwa na ufanisi mkubwa.
Ikumbuke kanuni ya Pareto ya 80/20. Asilimia 80% ya matokeo inatokana na asilimia 20 ya juhudi. Ikiwa na maana vitu vichache vyenye tija hukupatia matokeo makubwa.
Je, wewe upo kwenye dira yako?
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#11mwangaza2023.
Sunday, February 05, 2023
Fanya kwa moyo wako wote
Fanya kwa moyo wako wote..
Ili uwe na mafanikio kikazi au hata masuala mengine huhitaji miujuza, maombi au mfungo. Kwamba mpaka ukoo ufunge maombi ya siku 7 au zaidi ili kazi au mambo yako yafanikiwe. Huku wewe ukiwa mahali umetulia, unasubiri fulani aamue au kufikiria kwa niaba yako.
Bali unahitaji kufanya kazi yako au mambo yako kwa moyo wako wote. Kwa uwezo wako wote na kwa namna unavyoona inafaa. Sasa changamoto ambayo imekuwa inatukumba walio wetu ni ile hali ya kufanya kazi au kitu pale tunapojisikia. Yaani wiki hii hatuna "mood" ya kuifanya hiyo kazi au kitu tunaacha. Tunasubiri siku "mood" ikipanda tukiwa na amsha amsha ndipo tufanye kazi.
Hiyo kitaalamu tunaita kugusa kazi juu juu huwezi kuifanikisha. Na hii imekuwa changamoto kubwa kwetu. Imesababisha malalamiko kwa wengi wetu. Oh sioni maendeleo ya kazi yangu.Oh mimi nina bahati mbaya. Nataka niamie mjini huku kijijini wananichezea. Huku mjini siku hizi pamoto sioni matokeo. Mme/Mke, mpezi, bosi kabadilika. Ikumbuke hii, "huwezi kupata kama utafuti".
Kumbe; wewe mwenyewe ndiye unayejikwamisha. Kazi au kitu chako unakigusa juu juu alafu unategemea kukifanikisha kwa kiwango kikubwa. Ni ngumu sana. Hata jua litelemke bila kukifanya kitu au kazi yako kwa ubora wa hali ya juu hutofanikiwa. Ndio maana Wakolosai 3:23-24 inasema
"Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu". Maandiko yameweka wazi. Fanya kwa moyo wako wote.
Upo shuleni, unasomea mtihani. Huwezi kuwa na ufaulu mkubwa. Maana hujakaa kwenye mchakato sahihi kiusomaji.
Upo kazini, unasubiri hadi bosi awepo ndipo unakuwa na ari ya kazi. Hapo sahahu ufanisi.
Upo nyumbani unasubiri shinikizo la Mume au Mke sahahu maendeleo.
Upo kwenye mahusiano ubasubiri kila mpango utoke kwa mtu fulani. Hiyo ngoma ni nzito. Utachelewa sana.
Ukifanya kitu au kazi kutoka ndani yako bila kuchoka lazima ifanikiwe. Hapo hakuna miujiza. Ni kazi na matokeo. Iwe wakati wa jua au mvua ifanye kazi yako au kitu kwa upendo mkubwa. Huwezi kujua nani anaenda kuwa mfano kutokana na kazi yako.
Usisubiri watu waje kukupa hamasa katika kufanya kazi au kitu chako. Jipe hamasa mwenyewe maana ndiye unayejua safari yako. Mungu atakubariki sana. Ifanye kazi yako kwa uwezo wako wote, upendo wako wote na kwa moyo wako wote. Hakika itakuheshimisha.
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#10mwangaza 2023