Ni swali ambalo nilimuuliza, mmoja wa watu naowafanyia training kwenye program zangu. Yeye yupo kwenye mauzo kwa maana ya biashara. Nilihitaji apate pia, huduma nyingine kati ya ninazotoa.
Kabla hajaanza program aliniambia, ndoto yake kuu ni kuwa muuzaji bora. Kuongeza ushawishi mkubwa katika biashara yake. Kuna vitu vingi alinielezea vinampa shida. Nikamwambia "mauzo sio kitu cha siku moja bali ni kitu chenye mkusanyiko wa vitu vingi ikiwemo kujifunza kila siku".
Ni mengi tuliongea lakini, moja ninalotaka kukushirikisha leo ni hili. Limekaa kama swali lakini lina nguvu kubwa unapomwambia mteja.
Ni kweli program aliyokuwa anataka nilimpatia. Lakini kwa kuwa zipo nyingine, sikusubiri aulize baada ya kukubali ya kwanza. Nilimuuliza hilo swali. Akashaangaa kidogo, baadaye akasema kama ipo nyingine inayoendana na hii nipe Kaka.
Mpaka sasa amekuwa akilitumia mara nyingi zaidi katika hudhma zake.
Sasa wauzaji wengi wamekuwa hawalitumii mara baada ya kumuuzia mteja. Tafiti zinaonyesha ukilifanyia kazi kwa wateja wengi wapo wachache utawafanikisha.
Ipo hivi pale unapokuwa umemuuzia mteja kitu. Au unazo huduma labda za mafunzo unazitoa. Mteja akaja na kuhitaji bidhaa moja. Usisubiri hadi akwambie nataka kitu kingine. Wewe muulize je, moja inakutosha?
Unapokuwa umemuuliza hili maana yake yeye atakwambia ikiwa anahitaji au la. Epuka kujipa majibu. Wewe kazi yako ni moja. Na swali hilo ni je, moja inakutosha. Wewe mwambie kila anayekuja kupata huduma kwako.
Mfano unafanya uandishi, tafsiri na printing. Mteja akihitaji huduma ya kuandikiwa mwambie moja inakutosha. Ikiwa na maana mpatie huduma nyingine.
Point yangu ni kwamba, wewe timiza wajibu kumuuliza hilo swali. Kila mteja unayekutana naye katika huduma yako. Usiache akachukua huduma yako bila kumuuliza.
Tahadhari: Usimuulize kabla hajafanya mauzo. Subiri akamilishe mauzo ndipo umuulize. Ili umhudumie zaidi.
Na mimi nakuuliza ndugu yangu mpendwa. Makala hii inakutosha?
Bonga nasi hapa hapa
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#16mwangaza2023.
No comments:
Post a Comment