Sunday, February 12, 2023

Huwezi kukwepa ujasiri

Tunaposema ujasiri maana yake ni hali ya kutenda jambo bila kuogopa. Kwa lugha rahisi bila kuwa na wasiwasi wowote.

Kwa bahati mbaya ujasiri sio jambo la kurithi kama tulivyozoea katika baadhi ya vitu. Ni zao unalolizalisha mwenyewe kutokana na jambo unalofanya. Ikilinganishwa na matokeo unayohitaji kuyapata. 

Ikiwa hutakuwa na ujasiri katika utendaji wako basi ujue hata kufanikiwa itakuwa ngumu. Maana mafanikio yenyewe ni ujasiri tosha.

Kuna wakati utasimama uso kwa uso na mlima mrefu unaohitaji ujasiri kufanya maamuzi. Juu ya gharama kiasi gani inahitajika kuupanda. 

Una biashara, kila mmoja atakuja na maoni yake. Kwanini usiongeze hiki. Mwingine kwanini usipunguze hiki. Kwa nini usikope kiasi fulani benk uongeze hiki au kitu kingine. Bila kuwa na ujasiri hutaweza kukwepa hali hiyo. 

Unahitaji kumpata mwenza wako. Lazima uwe na ujasiri wa kuyakwepa mapingamizi ya watu wako wa karibu. Maana kila mmoja atakuwa na ushauri juu ya mtu huyo. Kuna watakaosema, tafuta mwenye level fulani ya elimu. Mwenye kazi, biashara au kutoka katika kabila fulani. Yote hayo bila kuwa na ujasiri utapata shida katika maamuzi. 

Hivyo basi, ujasiri ni hitaji muhimu kwa mwanamafanikio yeyote. 
Kuongozi lazima uwe jasiri kuwaongoza wafuasi wako. 
Mchungaji lazima uwe jasiri kuwachunga kondoo wako. 
Msanii lazima uwe jasiri kuwaburudisha wafuasi wako. 
Mwalimu lazima uwe jasiri kuwafundisha wanafunzi wako. 

Bila kuwa jasiri utabaki njia kuu. Woga, hofu na lawama vitakujaa. 
Wakati ndio huu. Kama sio sasa ni sasa. 

Je, wewe ni jasiri katika kazi yako? 
Bonga nasi hapa hapa.

Imendaliwa na Lackius Robert 0767702659 
#17mwangaza 2023

No comments:

Post a Comment