Ni mara nyingi tumekuwa tunaacha kufanya baadhi ya vitu kwa kujipa moyo kuwa ni vigumu kufanyika. Unakuta mtu anafanya kitu kwa muda mchache anaacha kisa kuna ugumu anauona au kukutana nao.
Lakini ukweli ndio huu kwamba vitu vingi, ili vikamilike kuna juhudi nyingi zinapaswa kutumika. Juhudi hizi zinapaswa kuwa endelevu zaidi ya kawaida. Sasa wengi wetu baada ya kuona juhudi nyingi tunazoweka bila kupata matokeo huwa tunakata tamaa.
Hali inayofanya tushindwe kabisa kufanya vitu. Na pengine kuamua kufanya vitu vingine vipya zaidi tukihisi vitu vya kwanza havijafanya kazi. Leo ipo njia pekee nimekuletea nakushauri uifanyie kazi. Sio njia ambayo ni nyepesi kufanya ila ukiifanya kuna kitu kinaweza kuongezeka au ufanisi fulani katika kazi zako. Njia hii ni hii hapa.
Fanya kinachowezekana.
Hii ni njia na msemo unaoweza kuutumia kila siku katika maisha yako na utendaji wako. Kabla hujaacha kitu na kuanza kingine hakikisha kitu kimefanyika au jambo limefanyika. Umepanga kitu kabla hujakifanya unaachia njiani nakushauri kuitumia njia hii. Wewe fanya kile kinachowezekana.
Ni binti unahitaji kuzungumza naye kabla hujaacha fanya kitu. Usijipe majibu.
Kwa taarifa yako hakuna vitu au biashara inayoanza ikiwa kubwa wala mafanikio yanayoanzia juu. Vyote vinaanzia katika hatua za awali. Ikiwa na maana ya wahusika kufanya kile kinachowezekana.
Unataka kufungua duka. Fungua kisha unanze kuuza kadri utakavyoweza. Fanya kinachowezekana kufanyika. Usishindane na watu. Wewe fanya kilicho ndani ya uwezo wako wote. Hii itakusaidia kuona wapi panahitaji maboresho au kufanyiwa kazi zaidi.
Uzuri wa kufanya kinachowezekana ni kwamba unapata nguvu ya kuendelea zaidi.
Kila mara kabla hujaacha kitu jiulize je, nimefanya?
Kisha rudi kwenye msingi wa kufanya kinachowezekana kufanyika. Wasiliana nasi 0767702659.
Imeandaliwa na Lackius Robert
#32mwangaza2023
No comments:
Post a Comment