Dunia tuliyomo inayo mambo mengi. Kadri siku zinavyozidi kusogea ndivyo mambo yanavyozidi kuwa makubwa.
Na ndani yake kuna matukio yanayojitokeza kila siku. Kutokana na uwepo wa matukio hayo yanayokuja na matokeo tofauti. Wengi wetu tumejikuta tunaweka nguvu kwenye vitu vyetu.
Ukitaka kujua hili, nenda na mwenzako mahali. Piga picha naye alafu mtumie picha ambayo hayupo. Kisha mwambie umependeza akusaidie kuipost hapo Mtagombana. Umimi umeanza kushika hatamu. Hadi imefikia point msaada pakee unaoweza kuupata ni "pole sana". Hope unanielewa na wewe ni shaidi
Hii hali imepelekea hata watu kushindwa kuwasifia hata baada ya kufanya kitu kizuri. Lakini moja ya siri kubwa ninayokupa leo ni hii. Kumsifia mtu baada ya kufanya kitu kizuri au maamuzi sahihi. Ni eneo linalomfanya mtu afurahie zaidi.
Hii inamfanya aweke umakini kwako. Pata picha umeenda dukani kununua vitu vyenye thamani ya elfu hamsini. Muuzaji akakwambia hongera sana kuchukua vitu vyenye thamani ya pesa nyingi sio wengi wanamudu. Au hongera kuchukua hatua kununua simu nzuri, gari, pikipiki, nguo au kiatu. Unasikia furaha isiyo na kifani. Hadi unatamani kumpa buku la ziada..
Kwa taarifa yako. Hii ndio njaa waliyonayo wengi wetu. Unaenda kukutana na Bosi, mme/mke, Boy/girl friend wako. Ile unafika mbele yake. Unamwambia aise! Hongera sana Robert/Glory, umependeza sana hicho kiatu au shati limebamba, mmmh! hizo nywele zako hatari sana. Utaona anatabasamu.
Hivi unafikiri hakuna anayetaka kufisiwa? Hayupo kila mmoja anapenda. Na hii ndio njaa waliyonayo wengi wetu.
Wakati ni sasa. Mwambie hongera kwa maamuzi mazuri uliyofanya. Mme/mke wako mzuri sana. Nyumba yako, gari yako, tisheti yako nzuri sana. Hongera sana
Mtu anaposifiwa hata kama sifa ni ndogo inamfanya mtu anajisikia vizuri. Sasa ni nini unaenda kumsifia? Hapa unaangalia namna alivyo mfano nguo. Amevaa jezi ya Mnyama au mwananchi. Unaanzia hapo, ikiwa ananunua kitu msifie mwambie hongera sana kwa kuchukua hatua. Kununua vifaa hivi, sio wote wanaweza kumudu gharama.
Unapofanya hivyo na yeye kichwa chake kinavimba na anaanza kukusikia. Uzuri kwenye kusifia huwezi kukosea. Wewe unaongea na mtu unayemtazama.
Lengo kuu ni kutaka kuongeza umakini na usikuvu mkubwa kwenye kile mnachoenda kuzungumzia. Kumsifia mtu kunakusaidia kuwa na pa kuanzia. Maana unapomsifia lazima ataongea.
Nikuulize je, hutaki kusifiwa? Bonga nasi hapa hapa.....
Imeandaliwa na Lackius Robert
#18mwangaza2023.
No comments:
Post a Comment