Tunaishi mara moja. Hili endelea kulikumbuka katika utendaji wako wa kila siku. Huenda linakuja na kutoka katika maisha yako.
Kwanini ninasema, furahia zaidi leo? Ni kwa sababu mafanikio na furaha ni vitu vinavyoenda pamoja. Ikiwa huna furaha hutapata mood ya kufanya kazi. Na bila mood ya kufanya kazi basi hamna maendeleo yoyote.
Wengi wetu tunasema hatuna furaha kwa sababu hatuna pesa. Tunasahau hili kuwa; kama furaha yako ni pale utakapopata pesa. Basi tambua furaha yako haitapatikana daima. Maana pesa ni namba hazina mwisho.
Ukiwa na laki moja utahitaji milioni moja. Ukiwa na milioni moja utatamani milioni kumi. Ukiwa na milioni kumi utataka ishirini au therathini. Kadri utakavyozidi kupata pesa zaidi ndivyo utazidi kuhitaji pesa zaidi.
Ni nini kifanyike?
Kuwa na mtazamo kuwa pesa yotote uliyonayo ni zao lako na unapaswa kuifurahia. Hii ni kwa sababu kupitia kuifurahia ndipo utapata kubwa zaidi. Maana ukiwa na furaha utaweza kupata nguvu za kutafuta zaidi.
Usiseme sina pesa nyingi. Hivyo, siwezi kutoa msaada kwa watu. Usubiri upate pesa zaidi. Hilo halitawezekana. Pesa ni namba na namba hazina mwisho. Hivyo, kuitafuta kwako furaha hakutakuwa na mwisho.
Timiza wajibu wako kufanya kazi yako kwa ubora hata kama malipo ni kidogo. Usiache kufanya endelea kusonga mbele. Iwe wakati wa jua au mvua wewe fanya tu. Matokeo mazuri huwa yanaanzia kwako kwa kufurahia kazi yako.
Hutapata nafasi ya kuishi tena hapa duniani. Nafasi ni moja tu. Ikiisha imeisha. Furahia leo zaidi kisha fanya zaidi
Je, wewe furaha yako iko wapi?
Bonga nasi hapa hapa 076772659
Lackius Robert
#28mwangaza2023
No comments:
Post a Comment