Thursday, February 09, 2023

Siku yako inalipa?

Kila siku huwa inanza tofauti. Fikra, hamasa au motisha ya jana huwezi kuifananisha na leo. Pata picha ni siku mpya imefika huku ukiwa huna mpango au ratiba yoyote. Ni nini kinakujia kwa haraka haraka akilini? Na unaionaje siku hiyo? Hakika jibu linachanganya sana. 

Kwa lugha nyepesi lolote litakalotokea kwako litakuwa kipaumbele. Na utaliona lina uzito. Kwa sababu hakuna mbadala wake.  Mwisho wa  siku utagundua siku yako  imekuwa ngumu, ndefu na imebana sana. 

Upande wa uzalishaji au matokeo utaona hayaridishi. Mengi yamefanyika, safari nyingi zimefanyika. Lakini tija ni kidogo. Kwa nini uligusa kila kilichokuja mbele yako. Kukianza litakuwa suala moja kukimaliza nalo pia litakuwa lingine. Na utaona ni sawa maana hamna mpangilio wowote unaokuongoza. Na itakuwa ni ngumu kufanya tathimini kwa kuwa huna mwongozo..

Hayo siyo maisha unayopaswa kuyaishi ndugu yangu mpendwa. Weka nguvu kubwa katika kuwa na mipango(to do list) kuendana na kile unachofanya. Kupitia mipango yako ndipo utaweka vipaumbele. Kwa maana ya kipi kianze na kipi kifuate. 

Natumaini umewahi kuisikia kanuni ya Pareto ya 80/20. Ikisema asilimia 80 ya matokeo unayopata yanatokana na asilimia 20 za juhudi zako. Hapo unaweza kuona, ukifanya vitu vichache vyenye tija vinaweza kukusaidia kupata matokeo makubwa. Kuliko kufanya vitu vingi visivyokuwa na tija. Swali la kujiuliza ni je, inalipa? Kile unachofanya kinachangia nini kufanikisha vipaombele vyako? Ikiwa ni hapana kiweke pembeni. Kama ni ndio hongera. Kifanyie kazi tena kwa upendo mkubwa. 

Hujachelewa, wakati ndio huu. Ipangilie vema siku yako, ili ikusaidie kufikia ndoto kubwa za maisha yako. "Ikiwa huna kitu, usiogope kwa unachokipoteza". 

Je, ni nini ungependa tukusaidie katika kuweka mipango au vipaombele?

Bonga nasi hapa hapa

Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659


#1mwangaza2023

No comments:

Post a Comment