Saturday, February 18, 2023

Umuhimu wa kuwa Orodha ya Vitu vya kufanya(To do list)

Ndugu yangu mpendwa: 
Usiianze siku yako ya bila kuwa na orodha ya majukumu unayokwenda kuyakamilisha kwenye siku hiyo. Majukumu hayo yanapaswa kupangwa kulingana na vipaumbele vyake na hayapaswi kuwa mengi sana. Idadi ya majukumu yawe angalau tano au sita muhimu ya kukamilisha kwa siku ni nzuri ambayo ukiifanyia kazi utakuwa na matokeo mazuri. Ikiwa orodha itakuwa na vitu vingi utaona uvivu kuvikamilisha. Hii ni kwa sababu akili yetu imeumbwa hivyo. Vitu vikiwa vingi huwa inatafuta namna ya kuvikwepa. 
 
Naomba tuelewane katika hili; kwenye uandaaji wa orodha yako usiweke vitu hivi kuoga, kula, kulala hivi vinajulikana. Unaweza kuvifanya ukiwa katiza kazi yoyote ile. Orodha yako iendane na majukumu yako kikazi. Kama unafanya kazi katika ofsi fulani orodha yako ilenge majukumu hayo. Kama unauza duka, unasuka nywele weka ahadi ya kusuka watu wegi zaidi. Kama wewe ni bodaboda weka orodha ya kwenda safari nyingi zaidi. 
 
Ninakuandikia hivi kwa sababu kubwa watu wengi hupoteza muda  kufanya mambo kwa mihemko. Ili  kukabiliana na kila jambo linalokuja mbele yao. Wanakuwa hawana kipaumbele chochote kwenye siku yao, hivyo chochote kinachokuja mbele yao kinakuwa ndiyo kipaumbele kwao. Hali inayopelekea mwisho wa siku kuambulia kitu kidogo. 
 
Kwa mfano unaweza kuwa umepanga kukamilisha yafuatayo;

1. Kujifunza kwa kusoma kitabu kulingana na uhitaji wako, au kuhudhuria kikao 

2. Kuonaana na bosi katika taasisi fulani, kufungua duka au kwenda sehemu kufutilia mzigo.

3. Kuwahudumia na kuwatembelea wateja 5, kuandaa ripoti au kupiga simu ya ufuatiliaji wa malipo.

4. Kufuatilia ahadi ambazo wateja walitoa, bosi au rafiki, kuandaa cheque list ya malipo au quotation kwa ajili ya kampuni fulani kulipia. 

5. Kuweka miadi na wateja wapya viongozi,  marafiki au kutembelea ofisi fulani kwa ajili ya kupata taarifa fulani(visitation).

6. Kufanya mazoezi, kupeleka cheque benki, kufanya matembezi na familia au rafiki. 
 
Orodha hii utaitengeneza kulingana na namna unavyotaka mambo yako yawe ndani ya siku husika. Orodha inakuwa kama mwongozo wako kwa siku. Pia inakupa hamasa kutimiza kile ulichopanga kwa ufanisi wa hali ya juu. Bila kuweka orodha nzuri utajikuta ukifanya mambo mengi yasiyo na tija. Hii ni kwa sababu mambo hayajwahi kupungua. Wakati unafanya hili litajitokeza lingine. Utaona ni muhimu kulifanya ujakaa sawa linaingia jingine mwisho wa siku utajikuta umechoka sana na ukiangalia ulivyofanya havieleweki au kukupa nguvu. 
 
Nakusihi usijifunge au kukosa amani kisa ujatimiza au kukamilisha kila kitu ulichoweka kwenye orodha yako. Wewe zingatia utendaji, kilichofanyika kikakamilika ni bra kisichofanyika. Siku hazilingani leo unaweza usitimize yote uliyoweka kesho ukayatimiza yote. Inapotokea hujatimiza yote usijisikie vibaya. Jipange kesho ingia kwenye utendaji. Lakini hii isiwe sababu ya wewe kuzembea ukijipa moyo nitafanya hata nisipotimiza. Zingatia kufanya kile ulichopanga kwenye orodha yako. 

Umuhimu wa kuwa kuwa na orodha ya vitu vya kufanya: 

1. Kutopoteza muda katika mambo yasiyo ya msingi. 
2. Kuwa na mwongozo unaokuongoza katika siku yako.
3. Kutumia muda wako katika vitu vyenye tija. 
4. Kuweka nguvu katika mambo machache yenye kuleta ufanisi. 
Wakati ndio huu kuweka orodha ya vitu vya kufanya ili siku yako iweze kuwa nzuri na yenye manufaa makubwa. 

Je, siku yako inaongozwa na nini? 

Bonga nasi hapa hapa 0767702659 

Lackius Robert 
#23mwangaza2023
 

No comments:

Post a Comment