Fanya kwa moyo wako wote..
Ili uwe na mafanikio kikazi au hata masuala mengine huhitaji miujuza, maombi au mfungo. Kwamba mpaka ukoo ufunge maombi ya siku 7 au zaidi ili kazi au mambo yako yafanikiwe. Huku wewe ukiwa mahali umetulia, unasubiri fulani aamue au kufikiria kwa niaba yako.
Bali unahitaji kufanya kazi yako au mambo yako kwa moyo wako wote. Kwa uwezo wako wote na kwa namna unavyoona inafaa. Sasa changamoto ambayo imekuwa inatukumba walio wetu ni ile hali ya kufanya kazi au kitu pale tunapojisikia. Yaani wiki hii hatuna "mood" ya kuifanya hiyo kazi au kitu tunaacha. Tunasubiri siku "mood" ikipanda tukiwa na amsha amsha ndipo tufanye kazi.
Hiyo kitaalamu tunaita kugusa kazi juu juu huwezi kuifanikisha. Na hii imekuwa changamoto kubwa kwetu. Imesababisha malalamiko kwa wengi wetu. Oh sioni maendeleo ya kazi yangu.Oh mimi nina bahati mbaya. Nataka niamie mjini huku kijijini wananichezea. Huku mjini siku hizi pamoto sioni matokeo. Mme/Mke, mpezi, bosi kabadilika. Ikumbuke hii, "huwezi kupata kama utafuti".
Kumbe; wewe mwenyewe ndiye unayejikwamisha. Kazi au kitu chako unakigusa juu juu alafu unategemea kukifanikisha kwa kiwango kikubwa. Ni ngumu sana. Hata jua litelemke bila kukifanya kitu au kazi yako kwa ubora wa hali ya juu hutofanikiwa. Ndio maana Wakolosai 3:23-24 inasema
"Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu". Maandiko yameweka wazi. Fanya kwa moyo wako wote.
Upo shuleni, unasomea mtihani. Huwezi kuwa na ufaulu mkubwa. Maana hujakaa kwenye mchakato sahihi kiusomaji.
Upo kazini, unasubiri hadi bosi awepo ndipo unakuwa na ari ya kazi. Hapo sahahu ufanisi.
Upo nyumbani unasubiri shinikizo la Mume au Mke sahahu maendeleo.
Upo kwenye mahusiano ubasubiri kila mpango utoke kwa mtu fulani. Hiyo ngoma ni nzito. Utachelewa sana.
Ukifanya kitu au kazi kutoka ndani yako bila kuchoka lazima ifanikiwe. Hapo hakuna miujiza. Ni kazi na matokeo. Iwe wakati wa jua au mvua ifanye kazi yako au kitu kwa upendo mkubwa. Huwezi kujua nani anaenda kuwa mfano kutokana na kazi yako.
Usisubiri watu waje kukupa hamasa katika kufanya kazi au kitu chako. Jipe hamasa mwenyewe maana ndiye unayejua safari yako. Mungu atakubariki sana. Ifanye kazi yako kwa uwezo wako wote, upendo wako wote na kwa moyo wako wote. Hakika itakuheshimisha.
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#10mwangaza 2023
No comments:
Post a Comment