Friday, February 24, 2023

Tunategemeana ili maisha yaende

.            Nikiwa na nazungumza na                             wanafunzi wa shule moja Dsm.

Sio rahisi na haitakuwa rahisi hadi mwisho wa dunia. Kwamba et, kuna mtu anayeweza kusimama mbele ya  watu na kusema; mimi ninaweza kufanya kila kitu ili maisha yaende. Mimi ni jeshi la mtu mmoja ninaweza kila kitu peke yangu. 

Yaani anajitibu, anajiendesha, anajipikia, anajifulia, anajitengenezea bidhaa au mahitahi mengine. Hii sio kweli. Kwa namna moja au nyingine tunategemeana kwa kiasi kikubwa msaada kutoka kwa watu wengine. Sio kifedha tu bali mawazo, nguvu na ushauri wetu. 

Mfano mchungaji hawezi kusimama mbele ya kadamnasi na kusema mimi nayaweza mambo yote peke yangu. Anahitaji waumini. Katika kuendesha kanisa ikiwemo sadaka na utawala. 

Mfanya biashara hawezi kuvimba mbele ya watu kuwa, anapata pesa kivyake au kwa juhudi zake. Lazima awategemee wateja kununua bidhaa zake. Bila wateja hakuna manunuzi. Unaweza kuwa na bidhaa zote. Wateja wasipokuja, huwezi kuongeza vingine. Ndio maana upo msemo wa mteja ni mfalme. Kupitia manunuzi ndipo biashara inakua.

Mwanamme au mwanamke hawezi kujigamba mbele za watu oh mimi ni mimi. Nina watoto wa peke yangu. Hivyo, ninajitosheleza. Kumbuka, huwezi kupata mtoto bila kuwa na mwanamme au mwanamke. Kwa sababu mtoto hashuki kutoka mbinguni au kwenye chai. Lazima jinsia mbili wakutane kimwili(Kufanya tendo la ndoa). Baadaye mtoto apatikane. Tunategemeana kumbuka. 

Mwanasiasa hawezi kusimama au kuzungumza mbele ya vyombo vya habari akijigamba yeye ni yeye anaweza kila kitu. Ni makosa. Anawategemea waliomuweka kwenye kiti ambao ni raia. 

Ninaweza kuandika hadi kesho lakini point ni kwamba tunategemeana. Wakumbuke wahenga, "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu". Ni dhahiri unamtegemea mtu mwingine kukamilisha umoja huu. 

Shule inahitaji walimu. Walimu wanahitaji wanafunzi. Wanafunzi wanawategemea wazazi. Soma kurudi nyuma. Wazazi wanategemea wanafunzi kuwapeleka shule. Shule inahitaji walimu ambao wanawategemea wazazi. 

Wewe sio jeshi la mtu mmoja. Kuna watu walikufanya kuwa hivi ulivyo kwa sasa. Heshimu, saidia na wajali watu bila ubaguzi wa aina yoyote. Safari yako ya mafanikio sio ya peke yako. Unahitaji watu kuifanikisha. 

Je, unaweza kufanikiwa ukiwa peke yako? 

Bonga nasi hapa hapa 0767702659 

Imeandaliwa na Lackius Robert 
#27mwangaza2023

No comments:

Post a Comment