Wednesday, February 22, 2023

Sikiliza ila fanya kinachofaa...

Ni kawaida yetu binadamu kutoa ushauri au mapendekezo pale inapobidi au tunapoombwa. Katika hili wengi wetu tumekuwa tunatoa mapendekezo au ushauri wa moja kwa moja hata kwa baadhi ya vitu ambavyo hatujawahi kufanya. 

Wakati mwingine hujawahi kufanya biashara fulani. Mtu anapokuomba ushauri kutokana na changamoto anayopitia. Wewe unamwambia haa! kama wateja wachache achana nayo. Fungua nyingine. Tena unamhakikishia inaenda kumlipa zaidi. Cha kushangaza hiyo unayomshauri hujawahi kuifanya unaisikia kwa watu. 

Hii ilimpata rafiki yangu  Japhet japo sio jina lake halisi. Aliomba ushauri kwa rafiki yake. Bahati mbaya rafiki yake alikuwa ni wale wanaotoa ushauri wa moja kwa moja. Tena kwa msisitizo wa hali ya juu. Na hakuwahi kufanya biashara yoyote.

Wakati Japhet alikuwa anafanya biashara ya nguo. Alikuwa anafungua saa nne na kufunga saa kumi. Hivyo, wateja wakawa ni wachache anaowapata kulingana na muda anaofungu na kufunga. 

Baadaye akaona mtu wa muhimu kuomba ushauri ni rafiki yake. Akaenda, wakazungumza. Akajielezea kuwa; biashara yake imedolola hapati faida wateja ni wachache, anapata hasara. 

Rafiki yake, kusiki hivyo. Akamwambia Japhet. Wewe hiyo biashara ya nguo achana nayo. Haiwezi kukulipa. Fanya biashara ya viatu. Hii inalipa sana. Karume pale viatu afu 3,000. Baadaye unauza elfu 10,000 hadi 20,000/= raha na biashara tamu mdomoni. Rafiki yake kamwambia atafute pesa kiasi fulani kwa kuuza nguo zilizopo. Ili baadaye aanze kuuza viatu. Na akamwambia yeye atakuwa mteja wa kwanza kununua viatu. 

Japhet akasahau msemo wa "Usichinje Ng'ombe kwa oda ya maini". Akafanya kama alivyoambiwa. Akaacha biashara ya nguo na kuuza viatu. Akaweka matarajio mengi. Anaenda kupata faida kubwa zaidi ya ile ya awali. Akafanya haraka maamuzi.

Muda mrefu amefungua rafiki yake hajafika kuchukua viatu. Kila akimpigia kumtaka anunue anampiga kalenda. Imekuwa changamoto kubwa zaidi ile ya awali. Pesa alizotumia hata kurudi bado. Wateja wanaokuja mara nyingi ni wale wanaohitaji nguo. Yale aliyotarajia hakuyapata. Akaanza kukata tamaa. 

Pesa alizotumia bado hazijarudi. Mtaji wa kununua nguo hana hadi maumivu. Akaumia sana kufanya maamuzi ya haraka sana. 

Huenda upo kwenye kada nyingine. Biashara nyingine, upo kwenye ndoa. Take care do what is right for you. 

Funzo: 
Kabla hujaenda kuomba ushauri kwa mtu jitafakari kwanza. Mfano Japhet alikuwa anafungua saa nne na kufunga saa kumi. Ni muda mchache sana. Hili lilikuwa tatizo la kwanza.

Unapata changamoto namna ya kuitatua. Nenda kwa mhusika. Ambaye amewahi kuipitia hiyo au ana uzoefu zaidi yako. 

Sikiliza ushauri wa kila mmoja ila fanyia kazi yale unayoona yanafaa kwako. 

Biashara yoyote ile inalipa ukiifanya kwa nguvu zote, upendo na moyo wako wote. 

Je, ni maamuzi gani uliyofanya yakakuangusha? Bonga nasi hapa hapa 0767702659

Imeandaliwa na Lackius Robert. 

#26mwangaza2023

No comments:

Post a Comment