Friday, February 17, 2023

Uchambuzi wa Kitabu Cha Where There is a Problem There is Money...

Katika kuendelea kuikuza Shauku. Nilipata nafasi ya kusoma, Kitabu cha  "Where There is a Problem There is Money" kilichoandikwa na Dkt. Sunday Adelaja mnaigeria mwenye mafanikio makubwa katika uandishi na uchungaji. Akifanyia utume wake mjini Kiev Ukraini. Katika kusoma kitabu hicho ndipo nilipokutana na neno "Air Ambulance Service au Flying Doctors Health Care" nikata kupata uelewa kwa ndani. 

Mwandishi Dkt. Sunday katika kitabu chake  anaelezea namna shauku ilivyo na nguvu kubwa kubadilisha maisha ya watu.  Anamwelezea Dkt. Ola Orekunrin mnaigeria aliyezaliwa mjini London Uingereza akiwa na shauku ya kuwa dakatari.  Kwa jitihada zake zote na kuufanikisha na akapata udaktari akiwa na umri mdogo. Mwandishi anasema alifanikiwa kuwa daktari akiwa na miaka 21. na kupata ufadhiri kusoma Japani na aadaye kurudi Uingereza kuendelea kazi. 

Dkt. Ola akiwa anaendelea na kazi zake za udaktari alipata taarifa kuhusu hali ya dada yake. Kuwa anaumwa ugonjwa wa "Sickle Cell Anemia" hali inayofanya kuishiwa damu muda mwingi. Hali hiyo ilimuumiza kichwa sana Dkt. Ola akaona ni bora afanye mpango wa kumsafirisha dada yake kwenda kupata matibabu katika nchi zilizo karibu. 

Usafiri uliokuwa unahitajika ulikuwa ni wa Air Ambulance yaani unasafri angani huku ukiwa unaendelea kupata matibabu. Maana yake ni kwamba wakati unapelekwa hospitali matibabu kwako yanaendelea bila shida. Na aina hizi za huduma wanapea watu waliozidiwa na ugonjwa. 

Kutumia usafiri wa ndege kutoka nchi moja kwenda nyingine kidogo inachukua muda mrefu kama hakuna matibabu ndani ya ndege inaweza kupelekea mgonjwa kuaga dunia. Kwa hiyo Dkt. Ola akafaya utafiti kwa nchi za Ghana, Sierra Leone, Cameroon na nchi zingine za Afrika Magharibi kuona kama itapatikana ndege hiyo au taasisi inayotoa huduma hiyo ili amsafirishe dada yake kutoka Nigeria kwenda katika nchi hizo lakini haiweza kupatikana. 

Katika utafiti akagundua ipo moja katika nchi ya Afrika ya kusini haraka haraka taratibu za kumsafirisha zikafanyika. Yakiwa yamebaki masaa matano taratbu zote kukamilika kwa baati mbaya dada yake akaaga dunia. Moja kati ya kitu kilichomuumiza sana Dkt. Ola 

Aliumia sio kwa sababu pesa haikuwepo bali kukosekana kwa huduma ya Air Ambulance ambay ni salama na haraka. Ni huduma inayokuwa na jopo la madaktari wenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya kumtibu mgonjwa akiwa angani. Yaani kabla hujafika hospitalini tayari huduma za kimatibabu zinakuwa zinaenelea. Na hiyo huduma inaunguza saa vifo kwa sababu wagonjwa wengi wanakufa wakiwa safarini hasa katika maeneo ya vijijini na nchi zenye vita. 

Baada ya kifo cha dada yake Dkt. Ola alifanya maamuzi ya kucha kazi yake ya uuguzi katika nchi ya Uingereza na kuamua kwenda kwao nchini Nigeria kuona kama lipo jambo anaweza kulifanya kuzuia vifo vingi visitokee. Anasea kigfo cha dada yangu kimetokana na kukosekana wa huduma abayo tunaweza kuianzisha na kuwaponya wengi zaidi. 

Hapo ndipo  wazo la Air Ambulance Service au Flying Doctors Health Care likaanza kufanyiwa kazi. Aliamini likifanikiwa litawasaidia wengi sio tu katika nchi ya Nigeria bali Afrika Magharibi na Afria kwa ujumla. Kupitia wazo hilo aliona ili lifanikiwe ipo elimu za ziaa inahitajika kwake. Hivyo aliamua kusomea masuala ya huduma za angani yaani Air Ambulance Service na baadaye apata mafunzo ya urubani upande wa helikopita. 

Shauku yake kuu ilikuwa ni kuwasaidia wagonjwa wanaopata shida za kifaya katia nchi ya Nigeria na Afrika Magharibi kupata huduma haraka. Hakuendelea kuweka nguvu kwa dada yake bali aliona kuna haja ya kuwaponya wengi zaidi na hapo ndipo msemo wa usipoziba ufa utajenga ukuta unapofanya kazi. Aliona ni bora kuzuia vifo vingine kuendelea kutokea. 

Flying Doctors Nigeria Limited chini ya Dkt. Ola ndiyo taasisi ya kwanza kutoa huduma za haraka kwa watu wanaopata majeruhi na wenye uhitaji wa matibabu ya haraka Afrika Magharibi. Norman Vincent aliwahi kusema , “kila tatizo lina mbegu na suluhu yake. Kama huna tatizo hutakuwa na mbegu” na hiki ndicho tulichoona kwa Dkt. Ola. 

Dkt. Ola alinukuliwa akisema, chini nyingi za kiafrika zna changamoto ya magari ya ambulasi na hayo machache unakuta kuna changamoto ya barabara kuwa mbovu hali inayopelekea baadhi ya wagonjwa kuaga dunia wakiwa wanapelekwa kupata matibabu. Anasema, sikuja Afrika kuonyesha kwamba mimi nina utaalamu sana. Bali nilitaka kuja na suluhu inayoweza kuokoa maisha mengi ya watu. Sikuona haja ya kulalamika kwamba serikali haikuwa imewea mkazo au kulalamikia barabara zetu. Niliona nifanye kile kinachowezekana kufanyika kuwaokoa wenzetu. Changamoto zilikuwa nyingi, makosa na vizuizi vigi lakini tulifanikiwa. 

Dkt. Ola amepewa tuzo mbalimbali, ameajiri wafanyakazi zaidi ya 30 na kwa na ndege zaidi ya 20 zinazotoa huduma ndani na nje yaNigeria. Amekuwa mhamasishaji bora na mjasiriamali mkubwa kwa sasa lakini yote hiyo imetokana na shauku aliyokuwa nayo kuwa daktari na kuwaponya wengi zaidi. 

Maana ya flying doctor hawa ni madaktari wanatoa huduma za kiafya huku mgojwa akiwa kweye ndege au katika maeneo yaliyo mbali na huduma au yaliyotengwa. Mfano wakati wa vita kunakuwa hakuna  huduma boraza kiafya hivyo wanachukulia madaktri kwenda katika maeneo hayo kutoa huduma. Wanakuwa na vifaa vya kutosha kuwapatia tiba wagonjwa katika maeneo yao. 

Ndugu yangu mpendwa unautumiaje muda wako? Je, unatafuta sababu za kujificha kwenye makosa? Sikia hii; kama wewe sio sehemu ya suluhu bali ni sehemu ya tatizo. Wakati ni sasa ni malengo mengi umepanga usiendelee kuwa mtu wa kulaumu serikali ndugu jamaa na marafiki. 

Hayo ni machache katika kitabu hicho tuwasiliane upate uchambuzi kamili. 

Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#22mwangaza2023

No comments:

Post a Comment