Kila kuna kitu kinampa nguvu kubwa hasa pale anapofanyiwa kitu kizuri. Iwe ni pesa amepewa au hamasa amepata. Kutokana na faraja baada ya kupitia hali fulani nzuri au ngumu.
Ninapoona sentensi hii napata faraja sana "With people, little things are the big things" ikiwa ina maana ya vitu vidogo, kwa watu vina nguvu sana.
Ila umfanye mtu ajisikie vizuri huna haja ya kumpa zawadi ya gari, pesa nyingi au kumpatia nyumba. Au iwe na elimu ya juu. Ni kupitia vitu vidogo unavyomfanyia ndivyo humfanya mtu ajisikie vizuri.
Huenda unajiuliza ufanye vitu gani ili umfanye mtu ajisikie vizuri. Jibu hili hapa.
Unahitaji kutoa kitu kidogo kinachotoka moyoni mwako. Mfano mtu anaumwa ukaenda kumjulia hali anafurahi. Unamtumia ujumbe au unampigia simu ya kumpa pole. Unamtembelea, huna kitu lakini uwepo wako unampa nguvu kubwa sana.
Mama amejifungua, umeenda kumjulia hali na zawadi kidogo kwa mtoto. Ni faraja tosha kwa mama mzazi. Sio mpaka uwe na pesa nyingi au ndo uende kumuona. Ujio wako unamfanya ajisikie vizuri.
Mtu kafiwa na mpendwa wake sio mpaka uwe na vitu vingi kwenda kumfariji au una kiasi kingi cha pesa nenda. Nenda na hicho kitu kidogo. Kaa naye mfariji mpe pole inamfanya ajisikie vizuri.
Kwa bahati mbaya walio wengi wetu wanachofanya ni kusubiri wawe na vitu vingi. Kama ni pesa ziwepo nyingi. Kama ni mali au vitu awe na vitu vingi kama vyakula au vitu vingine.
Ukweli ni kuwa, chochote kidogo ulichonacho na ukakitoa kwa moyo wako wote kinamfanya ajisikie vizuri.
Unachotakiwa ni kufanya kile kinachowezekana kwako. Usimpe mtu ukabaki na kinyogo moyoni. Toa kidogo, lakini moyoni ufurahie au ubaki na amani moyoni.
Hii ndio siri kubwa ya kumfanya mtu ajisikie vizuri. Toa kitu ata kama ni kidogo, ila ukiwa na kitu kikubwa usiache kutoa kikubwa kisa umeambiwa toa kidogo.
Je, wewe uliwahi kufanyiwa kitu kipi kikakufurahia?
Bonga nasi hapa hapa 0767702659.
Imeandaliwa na Lackius Robert
#37mwangaza2023
No comments:
Post a Comment