Hivi sivyo hukutoa kwenye dira?
Ebu chukulia mfano kwenye hosptali Daktari amshafishe mgonjwa, amsikilize, apige simu na wakati huo amhudumie mtu mwingine kwa kumpatia madawa. Baada ya hapo afanye ukaguzi wa list ya malipo yanayopaswa kufanyika. Daktari huyo huyo awafuatilie wagonjwa wengine wanaosubiri huduma. Kwa hali yoyote lazima atafanya makosa kwa mmoja au kukosea kwa wote, either katika kutoa dawa zisizo sahihi au kushindwa kumuosha vizuri mgonjwa mwingine.
Halikadharika sisi, Kila wakati tunapokuwa tunafanya kitu zaidi ya kimoja tunakuwa tunagawanya mazingatio yetu au nguvu zetu. Katika sehemu nyingi. Hali inayotupeleka nje ya dira yetu. Ni sawa na ule msemo wa “huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja”. Ikiwa hutawakosa wote bali utamkosea mmoja na kumfanyia usahihi mwingine.
Utafiti uliowahi kufanywa na taasisi moja ulionesha matokeo ambayo mtu anayefanya kazi nyingi kwa wakati mmoja anaweza kuyapata;
i. Kupoteza ufanisi. Yaani hapa kazi yako inakuwa haina ubora ule unaotakiwa. Maana nguvu zinaenda katika vitu vingi ndani ya muda mmoja.
ii.Kadri unavyotumia muda mwingi kufanya zaidi ya kitu kimoja ndivyo unavyopata matokeo kidogo maana hujaweka nguvu kwenye kitu kimoja.
iii. Unapoteza zaidi ya asimilia 28% kufanya vitu ambavyo vinapunguza ubora na ufanisi wetu. Pale ambapo unakuwa unafanya vitu vingi kwa wakati mmoja.
iv. Muda unaoutumia ni mwingi kulingana na kitu husika. Badala ya kufanya kitu kimoja kwa wakati ukakimaliza unaenda kufanya kitu kingine. Wewe unafanya vyote kwa pamoja kitu kinachopelekea kuchelewa kumaliza kwa wakati.
v. Makosa. Watu wanaofanya kazi nyingi kwa wakati mmoja ni rahisi kukosea au kufanya makosa mengi
kuliko wale wanaofanya vitu vichache vya msingi.
vi. Msongo wa mawazo (stress) watu wanaofanya kazi nyingi kwa wakati mmoja wanasumbuliwa sana
na msongo wa mawazo maana vitu vingi wanakuwa hawajavimaliza kwa wakati. Anawaza hiki mara kingine kinamjia. Yote hayo yakiungana yanatengeneza kitu kinachoitwa stress ambayo hupoteza furaha ya mhusika.
Zingatia hizi big idea;
1.Usijisikie vibaya ukutanapo na miingiliano yaani distraction maana kila mtu anakutana navyo. Wewe weka nguvu katika vitu vichache vya muhimu kuzingatia dira yako.
2.Usiruhusu miingiliano itawale kazi zako maana inapoteza concentration, furaha na vitu vinginevyo.
Kufanya vitu vingi inawezekana lakini haviwezi kuwa na ufanisi mzuri chagua kitu kimoja kifanye vizuri. Kisha fanya kingine au tenga muda. Vipe nafasi kulingana na uharaka lakini sio kwa wakati mmoja ili usitoke nje ya dira yako. Lengo kuu ni kutotoka nje ya dira yako na kuwa na ufanisi mkubwa.
Ikumbuke kanuni ya Pareto ya 80/20. Asilimia 80% ya matokeo inatokana na asilimia 20 ya juhudi. Ikiwa na maana vitu vichache vyenye tija hukupatia matokeo makubwa.
Je, wewe upo kwenye dira yako?
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659
#11mwangaza2023.
No comments:
Post a Comment