Wednesday, February 08, 2023

Unavyoitafsiri dunia sivyo..

 Unavyoitafsiri dunia sivyo...

Mafanikio yako yapo katika kile kitu unachotaka kuwa au kufanya. Na sio anachofanya mtu mwingine. Kama unataka kuwa mtu wakuandika unapaswa kuyaishi maisha hayo. Kama wewe ni mfanya biashara na ndiyo maisha unayoyataka, basi unapaswa kuishi katika hali hiyo. Na sio  kwamba waimbaji, wachezaji au walimu ndio hufanikiwa. 

Maana kitu unachokiwekea nguvu na kukifanya kila siku ndicho kinachokufanya uwe na amani na furaha.

Kama wewe ni mtu wa kuimba ukiishi mziki na ukaishi maisha ya uchezaji mpira kuna kitu kwenye maisha yako hakitaenda sawa. Yaani hutopata matokeo mazuri. Kuna kimoja kitakuwa na matokeo mazuri kuliko kingine. 

Ili uweze kuwa mtu wa mafanikio unapaswa kuyaishi maisha ya kitu unachotaka au unachofanya. Ikiwa umeona kinaweza kukuvusha. Weka nguvu katika kitu hicho. Fanya kinachowezekana kukifanikisha. Jifunze na kuwapenda watu waliofanikiwa na kitu hicho. Tofauti na hapo hutofanikiwa.Usiache pia, maeneo mengine  kufuatilia na kujifunza zaidi.

Katika maisha yangu nimejifunza kuwa; ili uweze kufanikiwa unahitaji kitu kimoja kwanza. Ambacho kitakuvusha kutoka sehemu moja hadi nyingine. Yaani iwe mchana au usiku. Wakati na masika wakati wa kiangazi. Unakifanya kweli kweli. Kila unapoamka asubuhi fanya kile kitu ulichochagua. Mfano angalia "Google" inahusu "search" kwa maana ya kutafuta. Wao waliwekeza hapo. Na ndiyo kilichowavusha waanzilishi. Angalia Apple, Amazon na zingine. 

Kwani ukiamka asubuhi mipango yako inahusu kitu ulichochagua? Na vipi kuhusu ratiba zako? Mizunguko yako na watu wako wa karibu?

Kama huwezi kufanyia kazi kitu unachokitaka kwa kujituma mafanikio utayasikia kwa watu. Na hapo utabakia na tafsiri yako kwamba; dunia ni ngumu au maisha ni magumu. Kumbe ugumu unauweka wewe. Kwa lugha nyingine wewe mwenyewe ndiye unayejizuia. Ukifanya kazi zako kwa bidii kila siku na ukatumia muda wako vizuri maisha yako yatabadilika na kuwa mazuri. 

Swali: Kitu kipi kimoja unakifanya bora kuliko kingine? 

Bonga nasi hapa hapa

Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659

#13mwangaza2023.

No comments:

Post a Comment