Sunday, February 19, 2023

Hiki ndicho hupoteza nguvu zako

Alikuwepo bwana mmoja tumuite Chris japo sio jina lake halisi. Alikuwa fundi mzuri katika masuala ya kutengeneza magari. Chris alikuwa analalamika sana kuhusu kazi kuwa kubwa na haoni matokeo. Anasema, wakati anafanya kazi moja, inakuja nyingine nzuri zaidi anaikimbilia. Mwisho wa siku anajikuta amechoka sana kwa kufanya mambo mengi. Ila akijaribu kupima uzito wake anaona nguvu aliyotumia ni kubwa kuliko matokeo aliyopata. 
 
Chris aliona ni vema kumtafuta mtaalamu wa msuala na maendeleo binafsi(Personal Development Issues) ili aone kama anaweza kupata masaada. Siku ilifika mtaalamu akaonana naye. Akajielezea namna anavyotaka asaidiwe. Mtaalamu alimsikia vizuri akamwambia sentensi moja. Naomba ukimaliza kazi zako leo, niandikie vitu vitano na vikiwa sita sio mbaya  unavyoenda kufanya kesho. 
 
Chris akamuangalia mtaalam na kumuuliza, ina maana kukuita kwangu kote hapa na malipo ninayokupa hiki ndo umeona kinaweza kunisaidia? Mtaalamu akamwambia, naomba usinipe pesa yako. Ila hivi vitu vitano nilivyokwambia wewe nitumie. Kisha endelea kufanya hivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja. Utaniambia nafaa kulipwa au kukulipa? 

 Chris  alilalamika sana kwa kutosikia neno la hamasa na pole kutoka kwa mtaalam. Kwa mbinde sana akakubali kisha kufanya kama alivyoambiwa. Akilini mwake alifanya kama kumkomoa mtaalamu. Kweli vitu vitano au sita tu ndo nifanya kila siku? Mh! Hapa nimekula kamongo. Haya! Ngoja nifanye nione. 
 
Kesho yake akamtumia orodha ya vitu hivyo. Na siku hiyo ya kwanza akafanikisha kufanya vitu vinne pekee. Siku iliyofuataalifanikisha vitu vitatu. Baada ya wiki moja Chris akaangalia kwenye orodha yake. Akagundua bado hata hivyo sita hajavifanya katika kiwango kizuri na kila akipanga havimalizi. 

Akaamua kuweka nguvu kwenye kuzingatia orodha yake. Siku inapoisha anapitia kuona kama alivyokamilisha ni kweli au la. Baada ya mwezi mmoja kuisha aligundua vitu vingi sana. Kwanza alianza kuiona kazi yake kama inampa matumaini kifedha na mambo ya muhimu angalau yalikuwa yananyika. Hii ni kwa sababu alikuwa anaenda na namba zake. 
 
Baada ya hapo aliomba kuonana na mtaalam kwa ajili ya kumpatia mrejesho na ushauri mwingine. Mtaalamu alikubali ombi lake na akaja tena ofisini kwake Chris Mazungumzo yalianza huku Robby akianza kuomba samahani wa maneno makali aliyotamka siku ile. Na akasema, mwanzoni nilichukulia kama kitu cha hovyo kisicho na maana lakini nilivyoanza kukufanya niliona ugumu na umuhimu wake. 
 
Siku zilivyoenda nikawa ninapata unafuu najikua hata muda wa kupumzika ninaupata. Kitu ambacho hapo awali akikuwepo. Nilikuwa bize asubuhi hadi jioni. Huwezi amini hadi mke wangu kipenzi Mama Joy anashangaa ninaenda mapema nyumbani huku nikiwa sina kazi nyingi za kufanya tofauti na hapo awali. Kwakweli , ninakushukuru sana. Naomba tu nikupe hiki kiasi cha pesa kama shukurani. Umenisaidia pakubwa naomba uwe unafutailia maendeleo yangu nitakulipa kiasi utakachoniambia. Mtaalamu akampongeza Chris na kazi ikaendelea. 
 
Huenda na wewe unapitia hali kama aliyokuwa anaipitia Chris Siku yako inakuwa na vitu vingi ambavyo mwisho wake ukiangalia hamna cha maana kilichofanyika. Inafika mahali unakosa muda wa kukaa na familia yako. Wakati ndio huu. 

Kumbuka,  kuweka orodha ya mambo unayoenda kuyafanya wa siku ni kitu cha muhimu zaidi. Wengi wetu tumezoea kusema vitu vyangu navijua kichwani sikia, "wino uliokauka ni bora kuliko akili" kwa sababu akili inaweza kusahau lakini wino ulioandikwa tayari hauwezi kuondolewa.      
Kuweka orodha ya mambo unayoenda kufanya kwa siku sio zoezi jepesi maana wengi wetu hatuna mazoea. Ni zoezi linalohitaji msukumo na ufuatiliaji wa mara kwa mara. Ikiwa ukifanikisha hili utakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo yako yasonge mbele. Siku ya leo unapomaliza kusoma makala hii anza kuweka orodha ya mambo unayoenda kufanya kwa siku yako inayofuata ili yakusaidie zaidi.

Je, wewe siku yako unaianzaje? 
Bonga nasi hapa hapa 0767702659 

Imeandaliwa na Lackius Robert 
#24mwangaza2023

No comments:

Post a Comment