Thursday, February 16, 2023

Unajua nini kuhusu?....

Kama upo kwenye biashara au unatoa huduma yoyote kwa maana unapokea malipo au unafanya mauzo. Basi ipo njia sahihi ninayotaka kukushauri leo. 

Ukweli ni kuwa, tumekuwa tukiingia kwenye malumbano na wateja wetu mara kwa mara. Moja kati ya sababu inayopelekea sisi kuingia kwenye malumbano hayo ni pale tunapobishana na mteja. 

Kitu kimoja usichokijua ni kuwa pale mteja anapokuja kwako kwa ajili ya huduma au biashara. Kuna eneo analokuwa amejiwekea ukomo. Hii haijalishi anaijua bidhaa au biashara yako.

Inapotokea wewe ukaenda nje ya ukomo huo lazima akatae. Sio tu kukataa lazima akupinge. Wakati mwingine anatafuta sababu nyingi ili aondoke bila kuchukua bidhaa. Usipokuwa makini utajikuta unalumbana na kila mteja.  Na yeye anaamini yupo sahihi hata kama sio. 

Hivi, unakumbuka siku alipokuja mteja anahitaji huduma yako. Ulivyoanza kumuelezea akaanza kukubishia? Imagine wewe ndiye mwenye biashara au unayotoa huduma halafu anakubishia. 

Ulipomwambia inafanya vizuri sana. Akakwambia, tena hii bidhaa au huduma niliwahi kuitumia ni mbovu. Au nimeambiwa haidumu kwa muda mrefu. 

Hope, unakumbuka ulimbishia sana. Hali iliyopelekea sintofahamu. Ulipotoka pale ukasema yaani huyu bwana! kaniharibia siku. Ukatamani kufunga duka au kusitisha huduma.

Ipo namna nzuri kutumia. Pale anaposema huduma mbaya. Bidhaa aifanyi kazi muulize hivi, unajua nini kuhusu? ...mfano unauza vifaa vya spear. Mteja anasema vifaa vyako vibovu. Unamuuliza hivi; je, unajua nini kuhusu spear za JK? Au unajua nini kuhusu huduma ya delivery? Hapo atatoa maelezo mengi. Akiwa anaamini ni mshindi. 

Akiwa anaelezea, msikilize kwa makini. Usimkosoe au kumwambia umevurunda. Wewe msikilize kisha msahihishe eneo analokosea. Kiupole sana. Mwambie, sasa hivi tunatoa huduma ya delivery au spear za JK zinafanya hivi na vile. Kumuuliza aseme mwenyewe kuna vitu atagundua anavikosea na kuwa tayari kukusikia. 

Ukielezea vizuri utaona anaanza kuzunguka oh! Unajua hivi ama vile. Basi nitakuwa nadanganywa au basi nipe nijaribu nione na vitu kama hivyo. 

Itumie hiyo kila unapokutana na mteja anayelalamikia huduma yako. Muulize kwa upole kabisa. Je, unajua nini kuhusu?......kaa kimya msikilize. Hii njia inaondoa malumbano kwa kila aina. 

Unajua nini kuhusu branding? 
Unajua nini kuhusu tlanslation, Ndoto yako, Maendeleo binafsi, ustawi wa biashara, uaandaji wa proposal, project, ubunifu, mauzo na mengine mengi kutokana na huduma unayotoa. 

Na mimi nikuulize je, unajua nini kuhusu mauzo, kusudi au ndoto Ya Maisha Yako? 

Ni kipi kingine ungependa tuzungumzie?

Bonga nasi hapa hapa 

Imeandaliwa na Lackius Robert 
#21mwangaza2023. 

No comments:

Post a Comment