Kwani ninataka chakula gani?
Ilikuwa jumamosi majira ya mchana. Kimvua mvua ndo kinakatika. Na jua Mbali linaanza kuangaza. Maeneo ya Songambele.
Ndipo Robin alipoenda kununua chakula Kwa Mama Ntilie aliyekuwa karibu na kwako. Robin alipofika alikaribishwa na harufu nzuri ya mapishi jikoni.
Alipofika Mama Ntilie akamkaribisha Kisha kumuuliza juu ya chakula anachotaka aletewe:
Mama Ntilie: Karibu kaka Mkubwa!
Robin: Àsante Mama.
Mama Ntilie: Kuna Ugali, Wali, Ndizi nyama, maharage, dagaa samaki na mboga mboga. Tukuletee chakula Cha aina gani Kaka?
Kimya kikatawala..Mama Ntilie akisubiri jibu kutoka Kwa Robin.
Robin: Akauliza kwani ninataka chakula Cha aina gani?
Mama Ntilie: Sijui. Ndio maana nimekutajia aina ya vyakula vilivyopo tayari. Ili wewe uchague mwenyewe unachotaka kulingana na bajeti yako.
Robin: Niletee chochote kizuri unachoona kinanifaa.
Mama Ntilie: Sawa mwanangu, lakini ungechagua mwenyewe ingependeza zaidi. Maana Mimi sijui chakula unachotaka. Ila ngoja niende ntakuletea.
Kimya kikatawala...Robin. Akaenda kunawa mikono. Baada ya dakika 10 chakula kikaletwa.
Mama Ntilie: Hiki hapa chakula mwanangu.
Robin: Àsante Mama Nina njaa Kali sana.
Mama Ntilie: Usijali mwanangu njaa imepata dawa.
Robin akaanza kula.
Alipomaliza, Mama Ntilie akaja kuchukua vyombo na pesa. Robin akatoa shillingi 1500/= Mama Ntilie akamwambia haitoshi. Robin akajam na kusema kwani chakula unauzaje?
Mama Ntilie, Pilau niliyokuwekea ni sh. 3000/= Kwa hiyo bado sh. 1500/=.
Robin macho yakaanza kumtoka mithiri ya mjusi uliyebanwa na mlango. Kujiangalia mfukoni hakuna pesa nyingine. Mama Ntilie akamwambia, ikiwa huna pesa nyingine weka simu Yako rehani. Ukipata pesa utakuja uichukue. Robin akakata na Kuanza kulalamika. Kwanini ujaniambia bei kabla ujanipatia chakula na mengine mengi. Mama Ntilie akamwambia, nilikuuliza hukusema. Mzozano ukawa mkubwa. Mwisho wa siku Robin akapewa vyombo avioshe Ili afidie pesa yake.
Je, nani mwenye kosa kati ya Mama Ntilie na Robin?
Mwenye kosa ni Robin hakutaka kuuliza bei.
Kwenye maisha, hupaswi kuchukulia kitu katika njia rahisi. Uliza ujue, upate details zaidi.
Je, hali hiyo iliwahi kukukumba?
Usiache kufuatilia na kutoa comment Yako hapa hapa. Endelea kukaa mkao wa kula yajayo ni makubwa.
Imeandaliwa na Lackius Robert
Tuwasiliane 0767702659
#mwangazaacademy2023
No comments:
Post a Comment