Kuna simu inaitwa cold calling (Simu ya baridi):
Hii ni simu ambayo unaipiga kwa Mteja au mtu ambaye hakujui na humjui ila namba yake umeichukua mahali. Labda kwenye gazeti, jarida, makala au kwenye mitandao ya kijamii.
Ni Moja kati ya simu ngumu kupiga. Kwa sababu nyote hamfahamiani. Hivyo, usipokuwa makini na mazungumzo. Mpokeaji anaweza akakata simu yako.
Huenda wewe ni shaidi ulichukua namba ya simu kwenye website, jarida au mtandaoni. Kila ukipiga inakatwa au haipokelewi na ilipopokewa ukapata utata namna ya kuingiza kitu chako.
-Sasa Kuna vitu vichache naomba uvizingatie:
Moja, jitahidi kuwa na taarifa sahihi. Ikiwa umesave namba fuatilia status yake. Soma vizuri kipeperushi ulichochukua namba au mtandao uliochukua namba. Lengo ni kuwa na taarifa sahihi za mhusika labda jina vitu anavyopendelea na vitu kama hivyo.
Hakuna kitu kizuri, kama kuongea na mtu ambaye una taarifa zake. Unakuwa na uwanja mpana wa kuzungumza naye.
Pili, Muda wa kupiga simu. Ni kweli umepata namba ya simu. Usiamke asubuhi saa 12 au saa nne usiku ndo unapiga simu. Angalia muda unaohisi yupo active (mida ya kazi).
Tatu, Jitambulishe. Helow, naitwa Robby. Nimepata namba Yako 1,2,4 je mwenzangu ni. Tumia hii...ikiwa hujui jina.
Ikiwa unajua Jina nenda straight taja jina lake. Helow Lackius, Unaendeleaje? Ataweka umakini kwako.
Nne, Dhumuni la kumpigia simu. Usikae unasema eh! Lackius niambie, hali vipi uko, mpo kwenye mavuno, ehh niambie ndugu!..ataona unamsumbua. Andaa vema nini unaenda kuzungumza naye. Usianze mazungumzo baadaye ukamuuliza akwambie kinachofuata.(Mpigaji ndiye anakuwa na kitu cha kuzungumza)
Mwisho, Mshukuru. Kwenye Kushukuru epuka. Kusema Nisamehe nimepoteza muda wako. Mwambie àsante Kwa muda wako. Tutaendelea kuwasiliana zaidi.
Je, ungependa tuongelee nini baadaye? Bonga nasi hapa hapa
Lackius Robert 0767702659
#mwangazaacademy2023
No comments:
Post a Comment