Thursday, February 02, 2023

UMUHIMU WA KUWA NA SHAUKU KUBWA

 Alikuwepo bwana mmoja tumuite Jayleen japo sio jina lake halisi. Alikuwa anacheza mpira. Siku moja akashangaa kuambiwa na kocha wake, kuwa hataondolewa katika kikosi mpaka masuala fulani juu yake yakae sawa. Jayleen aliwaza bila kupata majibu. 

Akaamaua kumfuata mwalimu wake na kumuuliza juu ya kilichotokea. Mwalimu akamwambia, Unajua Jayleen unapokuwa uwanjani unaonekana myonge sana. Huna amsha amsha.  Unacheza kwa hofu kubwa. Tumeona bora tukuondoe kwenye kikosi ili uone kama unaweza kubadilika. Wachezaji wakiona tunakuacha na unyonge wako kikosini wataiga tabia yako na hawataweza kuingia kwenye ushindani.  

Jayleen alikili na kusema; ninapokuwa uwanjani ninakuwa na hofu kubwa hasa ya kupoteza mpira. Mwalimu wake akamwambia, ni kweli nimekuona na hali hiyo muda mrefu huna hata shauku ndani yako. Endelea kufanyia kazi suala hilo. Usipolifanyia kazi hutoweza kupata namba tena.

Jayleen alipofika nyumbani kwao aliwaza sana. Mpira anaupenda lakini hofu inampelekea kukosa namba. Ndipo, akaanza kujiuliza kuhusu shauku na namna inavyoweza kumsaidia katika uchezaji wake. Ili apate matokeo anayotaka.

Jayleen akaamua kutengeneza shauku kubwa ndani yake. Akadhamiria kuwa mchezaji bora kuwahi kutokea. Na hayo ndiyo matokeo aliyokuwa anahitaji kupata.  

Alipoingia mazoezini taratibu akaanza kubadilika. Akiwa na mpira anakuwa na shauku kubwa ndani yake. Akaanza kuwa mchangamfu sana hadi mwalimu wake akaanza kumshangaa maana alikuwa na shauku kubwa hamasa anajiamini. Kubwa zaidi uwezo wa kufunga magoli ukaongezeka mara dufu.

Siku zilizofuata shauku kubwa ya kufanya kwa Jayleen ikazidi kushika hatamu. Hatimaye akarejeshwa kwenye kikosi, maajabu aliyoyafanya yalikuwa ni makubwa aliweza kuisaidia timu yake kutoka kifua mbele kwa ushindi. Mechi zilizofuata akawa ana shauku kubwa na ushindi ukazidi kuwa mkubwa. Mwisho wa msimu akaisaidia timu yake kuibuka bingwa. 

Hapo juu tumeona namna gani Jaylee mwanzoni kabla ya kuwa na shauku kubwa alikuwa anafanya vitu visivyo sahihi. Lakini baada ya kuwa na shauku kubwa ameweza kufanya mambo makubwa. 

Hata wewe yapo mambo makubwa unaweza kuyafanya. Kikubwa ni kuongeza shauku kubwa ya kufanya.....

Je, kitu gani kinakukwamisha na ungependa tuongelee hapa? Bonga nasi hapa hapa..

Lackius Robert 0767702659

#mwangazaacademy2023

No comments:

Post a Comment