Umewahi kukutana na mtu kwenye mazungumzo akakwambia unajua mi nani?
Hilo ndilo swali liliouliza Anania mbele ya Sebani. Hii ni baada ya kuwa amepewa nafasi ya kuwa msemaji kwenye sherehe moja. Kupata nafasi ya hiyo Anania aliona amemaliza kila kitu.
Kusema kweli, Anania ni mzuri kwenye ushawishi na anayo amsha amsha kubwa. Wahudhuriaji walimsifu kwa kwa kazi nzuri ya kuwa na ushawishi mkubwa. Na alikuwa anapata nafasi ya kuwa msemaji katika baadhi ya sherehe. Katika sherehe hii alipata nafasi ya kufikiwa na watu huku wakimpongeza. Mmoja mwa watu waliomfikia alikuwa ni Seban.
Seban alikuwa ni mkurugenzi mkuu katika taasisi mojawapo inayohusika na ukopeshaji fedha. Kwakuwa uso wetu hauonyeshi cheo au nafasi ya mtu sio rahisi kitambua.
Seban wakati anaenda kuongea na Anania. Kuna kutoelewana kati ya Anania na Rafiki wa mwenye sherehe kulitokea kuna jambo alitaka kufahamishwa ndilo likaleta utata. Sebani alipomfikia mzozo ulikuwa haujaisha. Alipofika akamuomba rafiki wa mwenye sherehe awe mpole wayamalize. Yule rafiki akakubali kutulia. Ndipo Anania akamjia juu Sebani.
Huku akimwambia kwa sauti ya ukali, hivi wewe unajua mimi nani? Sijapenda ujue. Mimi ninaweza kusema jambo likafanyika watu wananikubali. Angalia Mzee. Watu wengine hatuna dogo. Ukitugusa tunalipuka oho! Ebu muone suti yenyewe kaazima. We mzee umenikera sana. Mwenye harusi ndugu yangu ujue! Na kwa kuwa nina sauti leo utajua mi nani. Naamuru wakutoe unataka kuhatarisha usalama.
Seban akashuka, huku akimuomba Anania wayamalize amsamehe lakini alichofanya sio kosa bali alitamani wasiendelee kuzozana. Ndipo Anania akamwambia mwenye sherehe huyu bwana ingekuwa kwenye part yangu ningemtoa ndani. Amenikera sana. Mwenye sherehe akamuomba awe mpole. Siku hiyo yakaisha.
Baada ya wiki moja Anania akauguliwa na mwanaye. Pesa ikawa haitoshi kulipia matibabu. Mke wake akamshauri waende kuchukua fedha katika taasisi inayotoa mikopo katika kijiji chao.
Anania akakubali wazo na siku iliyofuata mapema akaenda kwenye taasisi hiyo. Alikaribishwa vizuri kisha kuelekezwa kufika kwa mkurugenzi. Ile anaingia tu kwa mkurugenzi uso kwa uso na bwana Seban. Anania akaanguka chini. Hii ni baada ya kuonana Uso kwa Uso na Sebani.
Baadaye wakammwagia maji kumshtua akaamka. Sebani akamkaribisha vizuri. Karibu sana Anania; jisikie huru. Nipo kwa ajili yako. Anania kwa kujingata ngata akasema ahasante saana Mh. Bosi mkubwa.
Kabla hatujaenda mbali naomba unisamehe kwa kitendo kisicho cha kiungwana nilichokufanyia juzi. Nisamehe sana. Sebani akamwambia mbona nishakusamehe muda mrefu Anania. We kuwa na amani. Mimi sina shida yoyote na wewe. Isitoshe hapa nipo kazini. Naomba nikusaidie shida yako.
Anania akainama akainuka na kusema. Nashukuru sana. Boss mkubwa. Alitumia bosi mkubwa kwa sababu alikuwa hajui jina lake. Baadaye Sebani akajitambulisha. Mimi naitwa Sebani Meshaki, ni mwanzilishi na mkurugenzi wa taasisi hii..tunahusika na ukopeshaji wa fedha kwa riba nafuu.
Hivyo, Nakukaribisha ofisini kwetu kupata huduma. Anania akamwelezea jinsi mwanaye anavyoumwa na anavyohitaji fedha kwa ajili ya matibabu.
Sebani akamwambia hiyo huduma ipo akamtajia riba. Mdhamini akachukuliwa rafiki yao Bwana Mtindi aliyekuwa na sherehe siku za karibu. Anania alifurahi sana kupata huduma. Sebani hakuongea kitu chochote yaani kuanza kufufua makaburi kuhusiana na kale ka mzozo kao. Alitenganisha masuala binafsi na masuala ya kazi. Kisha wakaagana huku wote wakifurahia.
Anania alipofika nyumbani akamwambia mke wake kisa kizima. Mke wake akasema yaani wewe Mume wangu nishakukataza hilo neno "unajua mi nani? Unapenda sana kulitumia. Angalia siku nyingine utakosa huduma hivi hivi. Baadaye wakampeleka mtoto wao hospital na akapata matibabu mazuri.
Funzo:
1. Heshima haina gharama, mheshimu mtu yeyote bila kujali cheo au kazi yake.
2. Watu wema wapo, ni sisi tunaowavunja moyo.
3. Tenda wema nenda zako, usingoje shukurani.
4. Ukipewa nafasi katika kufanya kazi fulani usivimbe kuvuka mipaka. Iheshimu na ijali kazi itakuheshimisha.
5. Kosa sio kosa bali kurudia kosa ndilo kosa.
Asante sana
Imeandaliwa na Lackius Robert.
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659 #8Mwangaza2023
No comments:
Post a Comment