Haileti mwanga hadi uiwashe..
Kuna wakati pamoja na mambo mengi ninayofanya ninahisi kukata tamaa. Kila ninachojaribu kufanya hakionekani kuleta matokeo mazuri kama nilivyotarajia.
Kutopata matokeo hayo, ndiko kunakoendelea kunivunja moyo kwa kiasi kikubwa. Na kufanga ile shauku yangu kufanya kazi kupungua.
Najikuta ninakosa watu wa kunishika mkono. Kunitia moyo kwa nyakati ngumu ninazopitia. Na wakati mwingine watu wa karibu yangu huchangia anguko langu.
Kwa mfano nimejaribu kufanya biashara nyingi kama genge, viatu na ufugaji nikashindwa hata kabla sijafika mbali. Hakika niliumia sana. Maneno yalisemwa mengi juu yangu na kila hatua niliyopiga nilipingwa vikali sana.
Nikaamua kufanya biashara ya nguo za watoto ili angalau nione kama nitaweza kujiinua kiuchumi. Lakini wapi na yenyewe ikashindikana.
Ila nikakumbuka msemo usemao "Usiache kufanya kisa hawapo upande wako, fanya kwa sababu unaona ni sahihi kwako" ndipo nikafuta vumbi. Na kukaza kamba ya viatu vyangu na kuingia kazini.
Nikaamua kwenda kwa rafiki yangu kuomba ushauri namna gani ninaweza kujiboresha zaidi kibiashara. Rafiki yangu akaniambia: nitulize akili na kuchagua biashara ambayo nitaona inafaa na ninaweza kuifanya vema.
Niliporudi nyumbani nikamwambia mke wangu. Kila kitu nilichoshauriwa kisha tukaingia kwenye utendaji. Biashara ya kuuza genge tuliwahi kuifanya tena kwa ufanisi mkubwa. Ndiyo mke wangu alishauri. Ila tuje na maboresho. Kwa maana ya kufanya delivery.
Mke wwangu alikuwepo nyumbani lakini sikuwahi kukaa chini kuzungumza naye. Baada ya kunipa wazo la biashara yetu ndipo hapo nikaamini tochi usipoiwasha haiwezi kujiwasha.
Kwakuwa kuna pesa kidogo ilikuwepo tukaingia kazini. Tukafungua na kufanya kila tulichopanga kwa ushirikiano mzuri. Ama kweli kidole kimoja hakivunji chawa. Sasa hivi tunaendelea vema na Biashara yetu na tunapata wateja wengi.
Ushauri wangu:
-Usikate tamaa kwa hali unayopitia.
-Usikubali changamoto zikae kwenye kiti. Utapata taabu sana.
-Ikiwa kuna mwenza upo naye baadhi ya vitu vya msingi mshirikishe. Ni mimi Maarifa.
Imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659.
#mwangaza2023
No comments:
Post a Comment