Wednesday, December 18, 2019

MBINU ZA MAFANIKIO NA LACKIUS ROBERT


UCHAMBUZI WA KUHUSU MAISHA NA MAFANIKIO NA  LACKIUS ROBERT
Zingatia haya machache yafuatayo

 TABIA YA KUBAGUA KAZI;
Hakuna binadamu aliyeumbwa kufanya kazi fulani na mwingine afanye kazi ile sote tunafanya kazi kuendana na maisha yetu yalivo.utfiti unaonesha kuwa asilimia 80% ya kushindwa kufikika kwa malengo kunachangiwa na sisi  mwenyewe katika fikra zetu yaani inner feeling halafu asilimia 20% ni Sababu za nje,matumaini yangu makubwa kwamba wengi wetu tunazitambua changamoto zinazotukabili kwa ambao tupo kwenye masomo tunatambua kwamba changamoto kama vile  ajira ipo tumeisikia hata wengi wetu  bado hatujaingia kwenye elimu ya juu na cha kushangaza ni kwamba baadhi yetu pesa tunazopewa  na wazazi wengine wnapewa na bodi lakini tunazitumia katika matumizi ambayo wakati mwingine yasiyo sahihi simanishi kwa wote ila kama unazitumia katika matumizi ambayo sio sahihi inakuhusu na tutambaua mlima ulio mbele yetu kwenda nyumabani kulima hautaki wakati pesa unazipata umazitumia vibaya je nani wa kulamiwa mzazi wako serekali au nafisi yako.nayaongea hayo maana nimewatazama vijana wengi wakiangaika baada ya kuhitimu masomo yao,huku wakilaumu sana.

Pia vijana wenzangu baada ya kuhitimu masomo kubagua kazi kunakuwepo wapo wengine wanaona kazi kama vile kuuza maji ,kupakia mizigo ni kazi ambazo anaona hazimfai kabisa tunashindwa kutambua kwamba hio pesa yenyewe tunayoitafuta haijawahi kumbagua mtu yeyote ndio maana utajiri auna ubaguzi utakuta vijana wengine miaka ishirini ana pesa za kutosha mzee mwenye miaka sitini au hamsini ana pesa za kubabaisha ,wzazee wengine wanapesa za kuosha wengine wamesoma wengine hata chekechekea hawajaenda lakini pesa anazo kwa hio vijana wenzangu swala la kubagua linatufanya tunabaki kuhangaika tu mijini na vijijini.Kinachoshangaza ni kwamba unamkuta kijana mwenzangu hana hata mia lakini ukimwambia njoo basi tukapige kibarua hata kusomba tofali kwa siku elfu saba au elfu kumi anakwambia hizo kazi sio za kwetu wapo wenye uwezo kwa kuzifanya ,na je! pesa na yenyewe ingesema mi nataka nishikwe na huyu Yule hafai ingekuwaje au kama ingewachagua wasomi tu,au ambao hawajasoma duniani tungeishi je?.

Vijana wenzangu ambao hatupo kwenye masomo ni mengi sana tunayaona pamoja na kuyasikia redio mbali mbali zinatangaza viongozi mbali mbali wanasema kuhusu namna gani vijana tuwe na maisha mazuri.Mimi nafurahi sana ninapowakuta vijana wanajishughulisha na shughuli kama vile biashara ndogo ndogo siku moja nilikuwa Ubungo nikakutana na kijana mmoja anabeba mizigo kwenye mkokoteni na kuzipereka sehemu tofauti kutegemea na wasafiri wanapoelekea nikabaatika kuzungumza nae kwa kina akanieleza jingi gani anavyopenda kazi yake licha ya kwamba pesa anayopata sio nyingi lakini mahitaji ya familia anayapata pia na kulipa kodi ya nyumba..

Changamoto yetu vijana wengi tunadharau kazi hasa hasa zile za kutumia nguvu nyingi lakini tukumbuke imeandikwa kila mtu atakula kwa jasho lake ,mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamba yake ila tunashindwa kufanya mfano mdogo wa kuku,nafukili wengi tunamjua jinsi gani anavyotafuta chakula chake kwa kuparua parua huku asipopata wadudu anageukia pale pale upande wa pili na kupata wadudu na kuwala .Vijana tuchotaka kuona ni kupata kazi nyepesi nyepesi kwa hali hio hatutafka mbali tuutume ujana wetu kufanya kazi nzito juani wakati  huo tukitegema kuvuna mazao tukiwa kivulini Walen Buffet anasema’ kivuli cha mti uliokalia leo kuna mtu aliupanda’kwa hio tupande mbegu bora kwa ustawi wa maisha yetu. Kila mtu anaouwezo mkubwa wa kufanya kazi yoyote endapo akilegeza mwili na kururusu moyo kuwa na  amani kwa kila kazi iliyoko mbele yetu. .

ILE HARI YA TAMAA;
Hali ya kutamani kitu fualani haiepukiki kwa maisha ya mwanadamu yeyote maana kutoka na kutamani ndiko tuapata ushindani pengine mafaikio pia wapo wanaotamani wazaliwe kama wachezaji wakubwa kama hapa Tanzania Mbwana Samatta kina Msuva na wengineo,wasanii wakubwa kama Diamond ,Lady Jay Dee ,waamashishaji maarufu kama Eric Shigongo,Nanauka Antony Luvanda na wengineo wengi tamaa ya namna hio kama tukitamani na kuongeza juhudi inakuwa ni nzuri .Kiuharisia kila mwanadamu anapaswa kutamani  tama mbele mauti nyuma maana kutokana na kutamani ndipo tunapata namna ya kusogeza maisha yetu mbele tama ipo katika Nyanja tofauti maana kila mmoja wetu  ana namna anavyotamani. 

Tamaa ya moyo, yaani tama hii Kwetu vijana imekuwa ni tamaa ambayo wakati mwingine hutususumbua na kuharibu mipango yetu ya maisha 20% katika wimbo wa’’ tama mbaya’’ anasema moyo sifa yake kutamani tama ya moyo inaweza kukuweka matatani. Mara nyingi tumekuwa tunatamani mambo makubwa kuliko uwezo wetu kama vile nyumba magari  nyingi wakati hatujaweka njia za kupata vitu hivyo na tamaa hiyo mara nyingi inapelekea kuhahirisha baadhi ya vitu tunavyokuwa tumeweka tumeona vijana wawili waliokuwa na mpango wa kujenga nyumba na mmoja wao akatamani ashobokewe na mabinti hadi akaamua kununua pikipiki ambayo hakudumu nayo muda mrefu na tama yake ilimponza.

Pia kuona kitu chochote kizuri moyo unakitamani kwetu vijana unamwona binti au mvulana mzuri moyo unamtani hadi akili nzima kichwani ivnavurugika unatamani kupata japo hata dakika kadhaa za kuzungumza nae ,uwepo pia wa mitandao ya kijamii umechangia sana vijana wengi kutamani sana maana kuna wengine wanapost picha zinazoonesha nguo za ndani ,aina mbalimbali za mitindo mara nywele,nguo n.k na sisi vijana tukiona wanapata comments na likes nyingi tunapata shauku ata kubadilisha miili yet undo wengine tunaona wanajichubua wananyoa mitindo tofati ya nywele na vijana wa kuime kutoboa masikio lengo ni kutaamani kuwa kama wale anaowaona lakini tutambue vijana  kusimama imara na kutunza miili yetu ni jambo ambalo linaleta heshima hata kwa jamii inayotuzunguka.

Tamaa ya pesa,jambo lisilo napingamizi kwamba kila mmoja wetu anataka awe na pesa za kutosha ili kujikimu kimaisha tama ya pesa hauwezi kuikwepa hata siku moja wengi tunaishia tu kutamani lakini hatuweki mipango madhubuti ya kupata pesa hizo inafika hatua wengi wetu wanaingia kwenye wizi,unyanganyi kwa watu wanoonekana wanapesa ,mali lengo ni kutaka kuwafanya hao vijana waingie katika ulimwengu wa matajiri.

Kuwa UNSTOPPABLE maana yake usitishiwe au kuyumbishwa na vitu vinavyoonekana havina tija kwa maisha yako ya kila siku,vijana tunyanyuke na kufanya kazi kwa bidii pes ipo ukiitafuta utaipata lakini kuendelea kulalamika pesa hakuna vyuma vimekaza hakutatusaidia kumbuka wanasema hata safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja Yule tajiri tunayemuona anapesa za kutosha naye alianza na shilingi 100 na kuendelea je mimi na wewe tunataka tuanzie shilingi ngapi ?.

Jambo la muhimu kuzuia tama ya pesa kutusumbua tuweke ratiba maalumu ya kuwa tunatunza akiba kila baada ya kupata kiasi fuani cha pesa haijarishi tumetunza kiasi gani baada ya muda alienza na mia moja tutakuwa katika harakati za kumfikia .Natambua changamoto zipo kila siku na hazitaisha lakini najiuliza kama baadhi ya vijana wenzetu wamefaulu kuzishinda changamoto hizo wakawa unstoppable kwa nini mimi na wewe? Je! Wao wana miguu,macho na mikono  zaidi ya mbili? .

Tufanye maamuzi sasa wakati ndio huu, katika kutamani kupata pesa Elieshi Lema katika kitabu cha ‘’In the Belly of Dar es salaam ‘’ amejaribu kuonesha baadhi ya vijana wanaotamani kuja mjini wakifikilia kuna maisha mepesi na kukimbia maisha yao ya kijiji baada ya kufika mjini wanakuta ni tofauti kabisa na matarajio waloyawaza pindi wapo nyumbani baada ya kuona maisha yamekuwa magumu huanza kujiingiza katika matendo mabaya ikiweo kufanya ukahaba wizi n.k.

Tamaa hii mara nyingi inachochewa sana na makundi ya marafiki tunaokuwa nao nimesoma stori kadhaa za madada wenye kutamamani pesa za haraka mpaka wakajiingiza kwenye biashara ya kuuza mwili,vijana wengi wa kiume kuishia kucheza kamali lengo ni kutaka kuwa na pesa alizonzo Fulani katika kundi lao na hali hii ya tamaa humfanya mambo yasiyo na tija kubwa kwa maisha ya badae mfano madwa ya kulevya, mtu anakosa amani anafanya kazi kufa na kupona mpaka apate kama cha mwenzake badala ya hizo nguvu kuziweka katika maendeleo ambayo yatanufaisha familia yake na taifa kwa ujumla.

Mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu sana. Ili kuendelea kupata chambuzi mbali za vitabu bonyeza link hii ili uendelee kupata ucambuzi wa vitabu kwa lugha ya kiswahili.
htthttps://t.me/SOMAONLINETELEGRAM




Uchambuzi wa kitabu cha How successful people think chake John Maxwell


MORNING MOTIVATION DIARY 
PRESENT: UCHAMBUZI WA KITABU
JINA: HOW SUCCESSFUL PEOPLE THINK: Change your thinking,change your life
JINSI WATU WALIOFANIKIWA HUFIKIRIA: Badilisha fikra zako, Badilisha maisha yako.
MWANDISHI : JOHN C.MAXWELL
UTANGULIZI

Wafikiriaji wazuri daima wanaangalia mahitaji,Wanatambua kazi zao za kila siku na kila wakati ni watu wanaojua kwanini wao ni mabosi.Mara zote hutatua shida zinazojitokeza katika sehemu wanazoziongoza iwe ni kwenye kampuni au la kamwe hawapungukiwi na maini jinsi kuendesha uongozi wao,wanakuwa na fikiri za mbali kuhusu kuwa na kesho ambayo ni bora.
Mwandishi John Maxwell anasema ,Nimejifunza zaidi ya miaka  arobaini na kugundua kuwa kinachowatofautisha waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni namna wanavyofikiri,waliofanikiwa mara zote wanajua umuhumu wa kujifunza zaidi na uzidi kujifunza ukilinganisha na watu wasio na mafanikio.

Kwanini unapaswa kubadili fikra zako?
Japokuwa kubadili fikra zako sio rahisi lakini ukiamua unazweza lakini unapswa ujue kwamba kubadili fikra hakuji automatiki lazima kuwe na kichocheo ,hivyo  kubadili fikra zako kunakusaidia kutatua matatizo mbalimbali na kukutengengenezea fursa.Pia unapelekea kuruhusu hisia zako kufanya kazi vizuri maana mfumo uwezo wetu wa kufanya jambo lolote unaanzia katika fikra zetu ndipo matendo yanafatia.Ufikiriaji mzuri unasaidia sana mtu kuyafikia malengo aliyoyaweka katika kazi zake ikiwemo wale anaowaongoza.
Ilii uweze kuboresha zaidi ufikiriaji wako
Tafuta sehemu tulivu ambayo haina mizunguko ya watu ukae utulie na uanze kutafakari kuhusu yale unayoyatamani kuyafanya baada ya kuyafikiria vizuri na kuyaweka katika mipangilio mizuri hatua kubwa inayofuata ni kuyaweka katika matendo.Jambo la kuzigatia ni kuwa unafanya hivyo mara nyingi ili kuweza kuuzoesha ubongo wako ufanye kazi zaidi na zaidi mafanikio yako yanaongozwa na fikra zako.

Ndugu karibu tuzichambue sura moja baada ya nyingine ni  matumaini kuwa  utafurahia pamoja na kuchukua hatua baada ya kufika mwisho wa uchambuzi wa  kitabu hiki.
SURA YA KWANZA

Tengeneza picha kubwa ya kufikiria
David SCHWARTZ aliwahi kusema "Pale ambapo mafanikio yanahusika, watu hawapimwi kwa nchi, pesa walizonazo au digrii za chuo kikuu, au asili ya familia zao bali hupimwa kwa ukubwa wa mawazo na yao. "
Unapokuwa umefikiri katika mapana ya picha kubwa ni njia ambayo itakupa ufanisi wa fikra zako. Sifa kubwa waliyonayo watu wanaofikiri kwa mapana ya picha kubwa ni kwamba daima huwa hawaridhiki na hali inayowakabili muda wote bali wanakuwa macho kwa ajili ya fursa mpya. Watu hawa wanajifunza kila mara kutoka kwa watu wengine na hivyo wanafanya kazi kwa bidii na ubunifu katika shughuli zao kila siku. Watu hawa wanatambua nguvu kubwa iliyopo kwenye usikivu kutoka kwa wengine kuliko kuwa wazungumzaji wakubwa. Pia, watu hawa muda wote wanatazama mbali malengo yao makubwa ni kutafuta fursa mpya ili wazifanyie kazi.
Kwa nini utengeneze picha kubwa ya kufikiria?
·         Kufikiria mapana yenye picha Kubwa inakusaidia kuongoza,Kama kiongozi unapokuwa na picha kubwa katika ufikiriaji wako unakuwa na maono makubwa kabla ya wengine kuyaona,unakuwa unawaza ya kesho kabla yao,unakuwa na mitazamo ya kule mnakoenda tofauti na wao waliyonayo.Ikiwa ni kujenga barabara, kupanga safari za kikazi katika uongozi, mawazo ya picha kubwa hukuruhusu kufurahia mafanikio zaidi. Watu ambao wanaangalia kila wakati picha nzima wana nafasi nzuri ya kufanikiwa kwa juhudi yoyote.
·         Kufikiria picha katika ukubwa Kunakupeleka kwenye mahali ulipolenga,Ili kufanya vitu vizuri, unahitaji kufikiria jambo katika upana wake ikiwemo kulielewa na kulifanyia kazi pasipo kusuburia.
·         Kufikiria jambo  kwa upana kunakusaidia kuona wengine wanapoona ,Moja kati ya ujuzi ambao mtu yeyote anahitaji kuwa nao ni uwezo wa kuona wengine wanapoona ,kwa kufanya hivyo hujikuta anawahudumia wateja wake vizuri tena kwa kuwaridhisha lakini hali hii inaambatana na ufikiriaji mzuri  unaoendana na kuwa unatafakari mambo katika ukubwa.
·         Kufikiri jambo kwa upana kunasaidia kuboresha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa pamoja na kuboresha mahusiano ikiwemo kusaidia na hii upendeza watu wanaofikiria mambo kwa upana zaidi wanapokutana.
Hivyo ili kuweza kuboresha uwezo wako wa kufikiri jambo kwa upana zaidi unatakiwa kujifunza kutoka katika kila uzoefu unaopitia au pale unapokuwa unafanya kazi na wengine mkabadirishana mawazo ya hapa na pale.Unapokuwa na wazo sahihi, unatakiwa uwashirikishe watu sahihi kwa ajili ya wazo husika, wazo pia lazima lishirikishwe katika mazingira sahihi, muda pia unatakiwa uwe sahihi.

SWALI : Je nafikiri zaidi yangu,ulimwengu wangu ili niweze kushughulikia maoni kwa mtazamo kamili?.Karibu upate sura ya pili mpaka mwisho wa kitabu hiki

Kupata uchambuzi zaidi wa kitabu hiki tuwasiliane kupitia 0767702659 Lackius Robert

Wednesday, December 04, 2019

Uchambuzi wa kitabu cha Ishinde tabia ya kughairisha mambo chake Joel Nanauka


MORNING MOTIVATION DIARY 
PRESENT: UCHAMBUZI WA KITABU
JINA: OVER COMING PROCRASTINATION,  ISHINDE TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO
MWANDISHI : JOEL NANAUKA.
UTANGULIZI:

Moja ya sababu kubwa ambayo inawafanya wengi kushindwa kutimiza malengo yao kwa wakati ni kughairisha mambo.Wengi wetu tunaseam ngoja niache kidogo ntamalizia baadae lakini baadae inapofika tunajikuta tayali tuna mambo mengine ya kufanya ilo tunalisahau.
Mwandishi Nanauka anaanza kwa kuuliza “Unakumbuka wakati watu wametangaziwa kujisajili kwaajili ya kupiga kura? Unakumbuka watu walivyotangaziwa kuhusu usajili wa vitambulisho vya utaifa? Ni siku gani watu walijaa zaidi? Bila shaka, utakumbuka ni siku ya mwisho hata kama waliliona tangazo. Kuna watu kila siku wanatuma maombi ya kazi siku ya mwisho hata kama waliliona tangazo hilo miezi miwili kabla. Kuna watu kila wakati watatuma ripoti yao siku ya mwisho, kuna watu kila wakati kazi waliyopewa kufanya wataiwasilisha dakika za mwisho”.Bila kujua madhara mkubwa yanayotokea baadae ,wengi wao hujikuta katika hali ya kuwa na stress(msongo wa mawazo) maana ata kazi wanapozifanya zinakuwa hazina ubora mzuri na hufanywa kwa kiwango cha chini kabisa na hali hii utokana na tabia ya kughairisha.Anasema alimia 95 ya wazee walipoojiwa walisema tunajuta kwa kughairisha mambo mengi katika maisha yetu ambayo tungeyafanya basi tungekuwa mbali zaidi.Huo ndio ukweli watu wengi wameghairisha mambo mengi tena ya msingi na kujikuta hawawezi kuyafanya tena.

Ndugu karibu tuzichambue sura moja baada ya nyingine ni  matumaini kuwa  utafurahia pamoja na kuchukua hatua baada ya kufika mwisho wa uchambuzi wa  kitabu hiki.

SURA YA KWANZA
Kwa nini watu wanaghairisha mambo?,utafiti wa kisayansi kuhusu kughairisha mambo.

Utafiti uliofanywa na William James ambaye ni mtaalamu wa saikolojia uliochapishwa katika jarida la sayansi ya saikolojia mwaka  1997 akishirikiana na Dianne Tice ambao uliwahusisha wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Western Reserve uligundua kwamba wanafunzi waliokuwa wanaghairisha walikuwa na msongo wa mawazo kuliko wanafunzi wasioghairisha hali hii ilikuwa inatokea hasa hasa katika ukusanyaji wa kazi(assignment) kwa mwalimu husika.Wakati wanafanya hivyo wanakuwa hawaoni Kama ni tatizo lakini baadae linakuja kuwa tatizo ,na mwishowe walijikuta hata kazi zao hazina ubora ukilinganisha na wanafunzi amabo walikuwa hawaghairishi mambo.

Mwandishi amebainisha taswira halisi katika maeneo ya kazi. Anasema wapo wafanyakazi ambao hawapendi kutekeleza kazi zao kwa wakati badala yake wanasubiri hadi dakika za mwisho ndipo waanze kuhaha huko na huko. Kimsingi tabia hizi zinazozungumzwa zinawagusa watu wa kila kaliba. Haijalishi umri wala nasaba au jinsia, Unaweza ukachukua daftari lako kuandika, ama ripoti yako ama hata kusoma kitabu, ukaamua kuwa unafanya unachotaka kwa nusu saa bila kuyumbishwa na kitu chochote, ghafla baada ya dakika 10 unajikuta nunashika simu na unasema ngoja niangalie meseji, kuja kushtuka unajikuta umeshatumia takribani nusu saa kuperuzi mitandao na hamu ya kuendelea na kazi uliyokuwa unaifanya inapotea kabisa. Ama wakati mwingine unasema ngoja niangalie TV kidogo kisha nitalala ama nitasoma kidogo, kuja kugundua unakuwa imeshafika saa 7 usiku na umeshindwa kuondoka kwenye TV yako.

Katika muktadha huo mwandishi anakumbusha kuwa wapo watu wanaoishi kwa kuahirisha. Wengine ambao hadi wakumbushwe ndipo hutekeleza jambo fulani. Wapo watu ambao hawezi kujikita kwenye eneo husika. 

Mwandishi anatumia utafiti wa Profesa Joseph Ferrari ambaye aligundua kuwa takribani asilimia 20 ya watu duniani ni waahirishaji wakubwa wa mambo yao,ambapo ufafanuzi wake umejikita katika mifumo miwili iliyopo kwenye ubongo kwa jinsi inavyoshindana.
Kuna mfumo unaitwa Limbic system huu una sehemu ambayo ndiyo unahusika na wewe kujisikia raha unapofanya jambo Fulani,mfano unapokula chakula kizuri,unapofanya tendo la ndoa na mengineyo.

Mfumo wa Prefrontal Cortex huu ni mfumo upo nyuma ya kipaji chako cha uso kazi yake kubwa ni kukuongoza katika kufanuya maamuzi mbali mbali.Huu ndio mfumo unaokusaidia kujua kipi kizuri na kipi kibaya kupitia tathimini hiyo unaweza kufanya tathimini ya kila kitendo amabacho unakifanya na kupima madhara yake.Hiyo ndiyo vita inayoendelea katika ubongo wako katika mambo mbalimbali unayotaka kufanya.
Unaporuhusu mfumo wa limbic kuwa na nguvu kuliko prefrontal cortex ambao ndio una uwezo wa kufanya maamuzi basi utajikuta unakosa hamasa na kuwa mgairishaji mzuri ambapo madhara yake ni kukosa nidhamu ya muda, kuhisi una mambo mengi yasiyokwisha sababu ya kutotekeleza kwa wakati na kulimbikiza majukumu ,utakosa hamasa ya kufanya jambo pia  utakosa  kuweka vipaumbele.
karibu ujipatie sura ya pili na kuendelea .....

Mchambuzi LACKIUS ROBERT karibu kwa mawasiliano zaidi 0767702659 email maarifarobert@gmail.com Kila kitabu kimoja kilichochochambuliwa ni shilingi 1000/= uchambuzi upo katika  mfumo wa PDF kupitia email ,Whatsup na telegram

UCHAMBUZI WA KITABU CHA EAT THAT FROG


MORNING MOTIVATION DIARY 
PRESENT: UCHAMBUZI WA KITABU
JINA: EAT THAT FROG, 21  GREAT WAYS TO STOP  PROCRASTINATING AND  GET MORE DONE IN LESS TIME. KULA HUYO CHURA ,NJIA 21 ZA KUEPUKA UGHAIRISHAJI NA KUFANYA MENGI KWA MUDA MFUPI.
MWANDISHI: BRIAN TRACY.
UTANGULIZI:

Brian Trace ni mwalimu mwenye uzoefu sana katika eneo la mafanikio. Baadhi ya mambo mengi ambayo Brian anatushirikisha ni yale ambayo amekuwa akijifunza, kisha anayafanyia kazi yeye binafsi na ndipo anatushirikisha kupitia vitabu vyake. Katika kitabu hiki ametushirikisha namna ya kupambana na hali ya kuahirisha mambo uliyopanga kuyafanya.
Ukweli kuhusu Chura
Mark Twain aliwahi kusema jambo kubwa unalopaswa kufanya kila asubuhi ni kula chura moja kwa moja."Chura" wako ndiye kazi yako kubwa na muhimu zaidi, ndio iliyo na uwezekano wa kuchelewesha ikiwa hautafanya jambo fulani juu yake. Pia ni kazi moja ambayo inaweza kuwa na athari nzuri zaidi maisha yako yote.
Sheria ya kwanza ya kula chura ni, "Kama utatakiwa kula vyura wawili, kula mbaya kwanza aliyebaki mmalizie baadae " ,Hii ni njia nyingine ya kusema kwamba, ikiwa una kazi mbili muhimu mbele yako, anza na kazi kubwa, ngumu na muhimu zaidi kwanza. Jiridhishe mwenyewe kuanza mara moja na kisha kuendelea mpaka kazi imekamilika kabla ya kuendelea na kitu kingine.Fikiria hii kama "jaribio.", Kataa jaribu la kuanza na kazi rahisi .
Sheria ya pili ya kula chura ni, "Ikiwa itabidi kula chura moja kwa moja, hailipi kukaa na kuiangalia kwa muda mrefu sana. " Ufunguo wa kufikia viwango vya juu vya utendaji na tija ni kwako kukuza tabia ya maisha yako yote ya kushughulikia kazi yako kuu kwanza kitu kila asubuhi. Lazima uendeleze utaratibu wa "Kula yako chura "kabla ya kufanya kitu kingine chochote, na bila kuchukua muda mwingi kufikiria juu yake.
Ndugu karibu tuzichambue sura moja baada ya nyingine ni matumaini kuwa  utafurahia pamoja na kuchukua hatua baada ya kufika mwisho wa uchambuzi wa  kitabu hiki.


SURA YA KWANZA,
Panga ratiba
Napoleon Hill aliwahi kusema"Kuna sifa moja ambayo mtu anayependa  kushinda anapaswa kuwa nayo , nayo ni kuweka kusudi  na ujuzi wa kile kitu ambacho ana hamu ya kukifanikisha. ”
Kabla ya kuamua kumla "chura" wako ili uendelee na kazi, lazima uamue unataka kufikia wapi kwenye  maisha yako.
Watu wengi wanashindwa kuyafikia malengo yao kwa sababu wanakosa motisha ya kufanya kazi ,kwa sababu hawana mwongozo ulio imara katika kuyafikia malengo waliyoweka.Utafiti unaonesha kuwa asilimia 3 ya walioweka malengo ndio waliofanikisha na wengine asilimia 97 walishindwa kuyafanikisha. Kuna hatua saba kama unahitaji kufikia malengo yako inabidi uzifahamu na kuzizingatia :
Hatua ya 1.Amua unataka uwe nani ,kaa chini tafakari chagua eneo ambalo unaona linakufaa lifanyie kazi.Steven Covey aliwahi kusema’’ kabla hujaamza kupanda ngazi ya mafanikio hakikisha ,ngazi imenininginia katika sehemu sahihi ya jengo’’
Hatua ya 2.Andika shehemu,Chukua kipande cha karatasi andika malengo yako ,wakati unaandika hakikisha unaandika malengounayoweza kutimizika ,yanayoonekana na kueleweka maana kuwa na malengo yasiyoandikiwa kunakupoteza.
Hatua ya 3.weka ukomo wa malengo yako,Maamuzi au malengo yasiyo na ukomo yanakuwa hayana uharaka ,hivyo unapopanga malengo hakikisha yanakuwa na ukomo ili kuepusha kughairisha mara kwa mara.
Hatua ya 4.Andika vitu vyote ambavyo unahisi ukiwa navyo vinaweza kukusaidia kuyafikia malengo yako.
Hatua ya 5. Pangilia vizuri mahitaji yako,weka vipaumbele/ pangilia vitu vya msingi sana unavyohitji ikifatiwa na vitu vingine amabvyo sio vya msingi sana.
Hatua ya 6. Chukua hatua,Fanya chochote, Mpango wa wastani uliotekelezwa kwa nguvu ni bora zaidi kuliko mpango wa kipaji ambao hakuna kitu kinafanyika .
Hatua ya 7.Amua  kufanya jambo moja kila siku lililo kwenye lengo lako,jitahidi kuzidi kujifunza zaidi na zaidi.

KUNA NGUVU KUBWA YA KUANDIKA MALENGO
Malengo ya maandishi yaliyo wazi yana athari nzuri kwa mawazo yako maana yanakuhamasisha na kukuchochea kuchukua hatua. Malengo ni mafuta katika tanuru ya mafanikio. Fikiria juu ya malengo yako na kuyapitia kila siku,Kila asubuhi baada ya kuamka, chukua hatua juu ya kazi muhimu zaidi unayoweza kukamilisha kufikia lengo lako muhimu zaidi kwa sasa.
SWALI:Je ni malengo yapi uliyojiwekea ili kufikia ndoto yako?.

Uchambuzi umefanywa na Lackius Robert kwa mawasiliano zaii 0767702659au maarifarobert@gmail.com

karibu  utatumiwa kwa njia ya PDF kupia whatsup,email,au tegegram.

Monday, October 21, 2019

Kwa ni mafanikio yanafananaje

MORNING MOTIVATION DIARY

Tafakari:
Kwani mafanikio yanafananaje?.

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena ambapo tunakuatana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary ,yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa na kuing'alisha siku yako.

Kulikuwa na watu watatu Jr,Jk na Jn ambao walikutana katika kijiwe kimoja wakawa wanapiga stori mdogomdogo.Jn akauliza kuna mtu mmoja nilimsikia akisema sema kuhusu mafanikio lakini sikumuelewa.Ndipo  wakaanza kuijadili mada hiyo,
Jr akasema Mimi nafikiri mtu mwenyewe mafanikio ni mtu anayejali wengine kutoka na shida walizonazo hivyo hupata baraka /dhawabu kwa kujitoa kwake kuwasaidia.Kuna shehe mmoja anajitoa sana kuwasaidia watu wengine hivyo ana mafanikio mengi sana pale mtaani kwetu.
Jk akasema mh! Hapana mi nafikiri mtu mwenye mafanikio ni mtu mwenye malengo,asiyekata tamaa,anayeongeza juhudi katika kutenda yale anayopenda pia na kubuni njia nyingine za kumuondolea utegemezi.Kuna mkaka mmoja mtaani kwetu namwonaga sana anavyojituma sana waga anaamka asubuhi anaenda kwenye kazi zake na kurudi jioni.
Jn,akasema mh! Mnanipoteza nyote hamjui ,mtu mwenye mafanikio ni mtu anayetokea katika familia bora ambayo Baba na Mama wanakazi nzuri ,nyumba,magari n.k hivyo mtoto anapewa na wazazi kila kitu anachohitaji na baadae anakuwa na mafanikio makubwa hasahasa kifedha.Maana mtaani kwetu nawaona ona watu wa namna hii.

Ndugu yangu mpendwa, Hakuna aliyekuwa anamsikiliza mwenzake anachoongea badala yao kila mmoja alitaka kuonekana yeye ndio mwenye mawazo sahihi .
Vivyo hivyo kwenye maisha yetu na kazi wapo watu wa namna hii wanaokalia kile tu wanachojua hawataki kupata kitu kipya.

CHONDE CHONDE "" Tabia usipoiacha itakung'ang'ania"".
,Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert
Karibu.

Monday, September 30, 2019

Jinsi ya kupata mtaji wa biashara au mradi

MORNING MOTIVATION DIARY

Jinsi ya kupata mtaji

Ndugu,
Ni siku nyingine tena ambapo tunakutana katika program yetu ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.

Unaweza kuomba mkopo Kutoka Kwenye Vyama na Vikundi mbali mbali,

Vyama vya kama SACCOS na Vikoba  Sifa kubwa unayotakiwa Kuwa nayo ni kuwa mwanachama wa chama chenye kukopesha na kufuata masharti ya chama husika.Mara nyingi vyama hivi na vikundi huwa vinatoa mkopo wenye riba na masharti ambayo siyo magumu kuyazingatia.
Watu wengi wamekuwa wanaanza biashara kwa kukopa Pesa kutoka kwenye VICOBA na kuweza kufanikiwa .
Miongoni mwa faida ni kwamba unakuwa na uhakika wa mtaji kuupata japo ata kama utakuwa ni mdogo ,na na mara nyingi wanakikundi wanakuwa wanakujua jinsi unavyochangia au jinsi unavyojituma.Inaweza kuanza na mtaji  mdogo, kama unahisi au unaepuka kufilisiwa mali zako ,lakini ukishaanza kuizoea biashara na ukaziju changamoto zake unaweza kukopa zaidi na ukawa inarudisha faida. Ni muhimu kutumia kanuni ya
 MAUZO _FAIDA= MATUMIZI hii ni kutokana na mwandishi Mike Michalowicz kayika kitabu kinachotwa  Profit First: A Simple System To Transform Any Business From A Cash-Eating Monster To A Money-Making Machine kilichoandikwa na Mike Michalowicz.Mwandishi anasema wafanya biashara wengi wamekuwa wanachukua mauzo na matumizi afu mwisho wa siku wanakuja kutafuta faida hivyo kama mjasriamali inabidi utoe faida kwanza uiweke pembeni ndo uangalie mauzo.

Ndugu yangu mpendwa hata kama umepata mtaji mdogo usisite kuanza kisa mtaji ni mdogo anza tu utakuwa unaongezea kidogo kidogo.

Unaweza kukopa kupitia taasisi za kifedha,
Taasisi mfano Benki
 Vigezo vikubwa wanavyoangalia benki ili wakukope ni kuwa na biashara ambayo umeianzisha angalau kuanzia miezi  sita au zaidi ambayo  ina mzunguko mzuri wa fedha.Uwe na account ya benki husika au uwe unaitumia benki husika pia uwe na dhamana ambayo utaiweka ili kama unashindwa kulipa waweze kuichukua ile dhamana ili kufidia.
Kadili unavyokuwa unaitumia benki ndivyo unavyozidi kuipa ushwawishi benki kukukopa maana benki nao wanaangalia mihamara (transaction) unazokuwa unazifanya.Wakati mwingine kama wewe ni mdau mzuri benki wenyewe wanaweza kukushawishi kukukopa maana kutokana na mihamara unayofanya unaonekana kukopesheka.

Lakini pia zipo  microfinances, hizi ni taasisi za kifedha ambazo hutoa mikopo midogo midogo kwa wahitaji.Hivyo unaweza tumia hizo na kuweza kuifanikisha biashara yako au mradi wako.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702759 Lackius Robert
Karibu.


Jinsi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara au mradi

 MORNING MOTIVATION DIARY

Jinsi ya kupata mtaji

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika programu yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako kwa kukuongezea maarifa na kuifanya kuonekana mpya.

Kujiwekea akiba wewe mwenyewe (saving),Akiba ni sehemu ya mapato ya ambayo huwekwa kando kama akiba ya dharura na mahitaji yasiyotarajiwa,mara nyingi akiba hutegemea sana jinsi mtu alivyojithatiti katika kuwekeza.Ukiweka akiba kubwa utakuwa na faida kubwa ,ukiwekeza kidogo utakuwa na faida kidogo.
Hii ndiyo sehemu ya kwanza na muhimu sana ambayo kila mmoja wetu anaweza kuanzia. Japo wengi hukosa nidhamu katika fedha na akiba zao, lakini unapaswa kujua hii ni sehemu nzuri ya kuanzia kupata mtaji wa kuanza au kukuza biashara yako.

Mara nyingi unashauriwa kukigawa kipato kabla hujakipata na mara unapokipata unakigawa kabla ujakitumia baada ya kukigawa kipato na kuweka akiba ndo unafanya matumizi mengine.
Njia hii ya kujiwekea akiba  umuwezesha mtu kuanza biashara akiwa na mani na bila ya usumbufu wowote wa kwamba ataanzia wapi .Hivyo mi nakushauri anza leo kujifunza kuweka akiba, ni ngumu sana kufika juu bila kuweka akiba.Angalia ni kiasi gani unapata kisha tenga faida au tumia ,kanuni ya asilimia 10 tu ya kipato chako na huo ni mtaji wako wewe mwenyewe.Mfano unapokea 100000/= kwa mwezi tenga 10000/= kama umepata 50000/= tenga 5000/= Mara nyingi mwanzo wa kujiwekea kipato huwa ni mgumu hivyo unajitahidi kufanya hivyo angalau miezi mitatu ya mwanzo ili uweze kuzoea.

Kama bado hujaanza ni muda wa kuanza ,kama tayali ushaanza jitahidi uyashinde majaribu maana saving inazo changamoto zake.

Kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki,
Ukiacha njia ya kwanza ya kuweka akiba(saving),njia nyingine inayoweza kukusaidia kupata mtaji ni kutoka kwa ndugu na marafiki.
Zama hizi watu wapo tayali kutoa pesa nyingi kwenye harusi ila ukiwaambia kuhusu biashara mtakimbizana,na watakukwepa utasikia yaani kama ungenambia jana au leo asubuhi  maana kuna mtu nimemwazima kiasi fulani.Mwingine atasema njoo ijumaa,jumamosi lengo ni kutaka kukukwepa lakini nakushauri usisite kumfatria atakupa tu ila wengi wamekuwa hawathubutu kuwabana vizuri.
Unaweza kuwatumia ndugu, jamaa na marafiki kupata mchango wa kuanza au kukuza biashara yako. Jambo lingine la msingi ni kuandaa vizuri wazo la biashara yako, na kuonesha ni kiasi gani cha fedha unahitaji ,ahadi zote utakazopewa jitahidi uzifatrie amini usiamini watu wengi wametajirika kupitia ndugu, jamaa na marafiki, mfano mtu tajiri kuliko wote barani Afrika kutoka Nigeria Dangote yeye wakati anaanza ujasiriamali aliomba msaada kwa ndugu, na kwa sasa tunaona maendeleo yake amekuwa bilionea ambaye amewekeza sana barani Afrika kwa vitu mbalimbali anavyouza kama  unga , mchele, mafuta, sukari,cement.Wakati anaomba hakuona haya kama wengi wetu tulivyo.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa Unapoomba usitegemee msaada wa fedha tu bali wapo watakaokupa msaada wa mawazo ushauri.Kuwa makini sana 'ongea na wote wasikilze wachache'  wengine watakupa msaada wa kifedha na uo utakuwa ni mwanzo wa wewe kusimama imara katika mradi/biashara.

Unaweza tumia mwekezaji wa biashara,
Mwekezaji ni mtu ambaye ana fedha ambazo anaweza kuziweka kwenye biashara mbalimbali na zikazalisha. Huwa hatoi fedha kama mkopo, bali naye huwa anakuwa sehemu ya umiliki wa biashara.
Kigezo kikubwa kinachohitajika ni kuwa na mpangilio mzuri unaoonesha mchanganuo wa biashara inahusu nini, wateja ni kina nani, wanapatikanaje na mipango ya ukuaji wake,jinsi utakavyokuwa ujalipa kodi.  katika hali hiyo unaweza kumshawishi mwekezaji kuwekeza kwenye biashara au mradi wako.

Anapowekeza kwenye biashara yako maana yake unampa hisa, hivyo unapopata faida na yeye anapata faida kulingana na mtaji alioweka katika biashara au mradu wako.Ikitokea hasara imepatikana na yeye hasara anapata hasara pia.
Kwenye hili unahitaji kuwa makini kwa mwekezaji unayemchagua inabidi awe  wa kuaminika na awe tayari kusubiri biashara hiyo ifanye vizuri. Pia wewe binafsi unahitaji kujituma sana kuhakikisha biashara inafanya vizuri ili usije kumwangusha yule anayekusaidia.

Kwanini ninasema unahitaji kuwa makini ni kwa sababu
biashara isipotengeneza faida kwa muda mliokubaliana inaweza sababisha kushitakiana na hatimaye biashara na mali zako kufilisiwa,ili kukwepa hiyo inabidi uwe unampatia taarifa ili ajue kinachoendelea.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.



Monday, September 23, 2019

Mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali

 MORNING MOTIVATION DIARY

Mambo usiyoyajua Kuhusu ujasriamali,

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena katika mwendelezo unaoelezea mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali,
Karibu:
Ujasiriamali ndiyo njia yenye hatari ndogo kwenye kipato.
Kuna watu  wameambiwa na  kuaminishwa kwamba  ujasiriamali ni hatari sana kwenye upataji wa  kipato. Kwamba unapokuwa mjasriamali unakuwa huna huakika wa kupata kipato asa pale unapokuwa na uhitaji wa fedha na usiweze kuzipata kwa haraka.Badala yake wameaminishwa kwamba ajira ndiyo njia ya  uhakika na yenye hatari ndogo kwenye upande wa kipato. Kwakuwa kila mwezi mtu anakuwa na  uhakika wa kupokea mshahara wake na hivyo ni kitu anachoweza kukitegemea.Kwa mjasriamali anayechukua tahadhari (take risk ) kwake siyo tatizo kubwa maana anakuwa amejipanga in case lolote likitokea.

Hali hii imekuwa kikwazo kwa wengi kufanikiwa kwenye ujasiriamali kwa sababu wanaingia wakiwa wnajua kwamba, kuingiza kipato siyo ni jambo ambalo kidogo siyo haraka.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa  katika kazi yoyote ile unayoifanya lolote linaweza kutokea kama uko katika ujasriamali unaweza kuyumba kifedha  na kwa aliye kwenye ajira anaweza kusimamishwa kwa hiyo wote  wanakuwa kwenye wakati mgumu kifedha.Ila utafiti unaonesha ujasriamali una hatari kidogo kulinganisha na kazi nyingine yoyote kwa mtu aliye makini.

Ujasiriamali ni asili yetu binadamu,
Watu wamekuwa wanaamini kwamba kuna watu ambao wamezaliwa kuwa wajasiriamali na wengine wamezaliwa kuwa waajiriwa pekee.Hali hii imewafanya wengi kushindwa kwenye ujasiriamali, wakiamini kwamba wao sio wajasriamali.

Lakini ukweli ni kwamba ujasiriamali ni asili yetu kama binadamu, kila mtu ana ujasiriamali ndani yake. Ukiangalia historia ya maisha ya wanadamu hapa duniani, kwa kipindi kirefu tumekuwa tunaendesha maisha yetu kupitia shughuli za kiujasiriamali

Wazee waliotutangulia waliweza kwa kujiusisha na shughuli za kijasiriamali ili kupata mahitaji yao makubwa ambayo mara nyingi yalikuwa ni chakula, mavazi, malazi na usalama.

Kila mmoja anaweza kuwa mjasriamali, Kama nilivyotangulia kuandika somo lililopita kuwa ujasriamali ni asili yetu hivyo ni wazi kwamba kila mtu anaweza kuwa mjasriamali.Kwa kuwa ujasriamali auchagui rangi ,kabila au jinsia au kusema mpaka uwe na elimu kubwa sana.Ujasriamali unategemea kwa jinsi gani ulivyojiandaa na kuingia kwenye shughuli.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,Usiingie kwenye mradi wowote au biashara kwa kufuata mkumbo kisa umeona  fulani kafanya jipange kwanza ili ukianza umeanza.Jiambie Mimi ni mshindi usikubali kurudi nyuma wala kuyumbishwa na mtu mwingine,Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.

Mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali

MORNING MOTIVATION DIARY

Mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika programu yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako kwa kukuongezea maarifa na kuifanya kuwa mpya.

Hakuna njia ya mkato kwenye ujasiriamali,

Watu wengi wamekuwa wanaingia kwenye ujasiriamali kwa mtazamo kwamba ni njia ya mkato na ya haraka ya kupata fedha. Ndiyo maana watu wamekuwa wanatumia muda mwingi kukimbizana na fursa zinazojitokeza ili wapate mafanikio haraka.

Lakini ukweli ni kwamba ujasiriamali unahitaji ufanye  kazi, utumie muda wako kujifunza pia kuwa na uvumilivu katika yale unayofanya.

Ukijaribu kuangalia kuna watu wamedanganywa sana kuhusu fursa mpya mpya ambazo zimekuwa zikijitokeza kila siku. Wamepewa hesabu za kwenye karatasi, zikawahamasisha, wakaingia kichwa kichwa na kupata hasara kubwa sana.Mwishowe kuanza kujilaumu kwa maamuzi waliyoyafanya.

Nikukumbushe ndugu mpendwa ,ujasiriamali unahitaji ujipange kama kweli umeamua kuufanya na kuwa tayali kupambana na kila hali itakayokutokea.

Kama inawezekana anzia sehemu yenye mkusanyiko kidogo,
Malengo makubwa ni kujifunza zaidi maana unapoanzia padogo kuna vitu vingi unavielewa zaidi kuliko kuanzia pakubwa maana kuna baadhi ya changamoto utazifahamu na kujifunza jinsi ya kuzitatu.Sasa Kosa kubwa ambalo watu wamekuwa wanalifanya kwenye ujasiriamali ni kuiga wengine. Mfano wanapoona wengine wanafanya biashara fulani, hujiambia hiyo biashara inalipa na hivyo huamua kuifanya matokeo yake kushindwa kuiendeleza baada ya kutoenda vizuri.

Kama mtu anayetaka kufanikiwa kwenye ujasiriamali, unapaswa kwenda sehemu yenye mkusanyiko mdogo, kwa kufanya kile ambacho hakuna wengine wanaokifanya.na  kama kuna wanaofanya, basi wewe unakuwa na utofauti fulani fulani.
Ambacho wateja wako hawawezi kukipata sehemu nyingine isipokuwa kwako pekee.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,una uwezo wa kufanya kitu kikaonekana cha upekee maana hakuna mtu mwingine ambaye ni bora zaidi yako,na upekee ulionao ni mkubwa kama yupo anakarbia kufanana na wewe ila hawezi kulingana na wewe.

Unapofanikiwa katika biashara moja hakumanishi unajua biashara zote,
Mafanikio kidogo kwenye ujasiriamali kwa wengi imekuwa kikwazo kwa mafanikio makubwa zaidi. Mtu anaanzisha biashara moja, inafanikiwa na kufanya vizuri na hapo ndipo kushindwa kunapoanza. Wengi uamini kwa kiwa wamefanikiwa kwenye biashara moja, basi wanaweza kufanikiwa kwenye kila aina ya biashara zingine.Hivyo huanza kujihusisha na biashara nyingine nyingi na tofauti tofauti kwa kuamini uzoefu wao kwenye biashara moja utawasaidia kwenye biashara nyingine wanazoanzisha.

Hali hii imekuwa inafanya wengine kurudi nyuma kimafanikio maana wanapoanzisha biashara yingine huweka nguvu nyingi kule tofauti na ilivyokuwa awali.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,Biashara zinatofautiana na pia zina changamoto ambazo ni tofauti tofauti ,hivyo unapofanikiwa kwenye biashara ya aina fulani, ni vyema kuendelea kuweka nguvu ili ufanikiwe zaidi.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659

Lackius Robert karibu.

Sunday, September 22, 2019

Zijue kanuni za kuwa mjasriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue kanuni za ujasriamali,

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongeza maarifa na kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.Karibu katika mwendelezo unaoelezea kanuni ambazo mjasiriamali anapaswa kuzizingatia:

Kuwa na umakini,hii ni moja ya kanuni bora kwa sababu ndiyo inayosababisha biashara au mradi wako kusonga mbale maana kila kitakachofanyika kinahitaji umakini mkubwa.Katika kuajiri,katika kusambaza huduma ,katika kuzungumza na wateja n.k
Ukiangalia waliofanikiwa siyo tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi walizokuwa wakifanya. Kama mjasiriamali unatakiwa kuwa mwangalifu kwa kila jambo, unatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe na uelewa wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko, uzalishaji na uendeshaji kwa jumla.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,
Kushika namba moja kwenye kile unachofanya siyo bahati ila ni umakini mkubwa.
CHONDECHONDE "Mazuri ya dunia ni mengi na yapo kila sehemu kuwa makini usipotee njia".

Umuhimu wa kuwa mwaminifu,Kama mjasiriamali mwenye malengo makubwa ya kufika mbali kanuni hii ni muhimu kuifanyia kazi na kuenenda nayo.
Maana uaminifu ni silaha kubwa itakayokulinda mjasiriamali na kuwafanya watu wengi wapende kufanya biashara na wewe au kuwekeza kwenye miradi yako.Ni vema kuwa mwangalifu katika  kulipa madeni hata kama ni madogo unapodaiwa, pia wauzie wateja wako huduma au bidhaa kwa bei halali.Kama tunavyojua serikali yetu inajiendesha kwa kutumia kodi hivyo mjasiriamali ni vema sana kulipia kodi na vibali vyote muhimu vinavyohitajika ili kukuweka katoka hali ya uhuru pindi uwapo kazini .Ili kuboresha huduma zako usiwe unatoa bidhaa zilizokwisha muda ,zingatia kutoa bidhaa bora maana mteja anapokuja kwako anakuwa anakuamini hivyo zidisha uaminifu kwake ili kesho arudi.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa "Uaminifu wako ndio mtaji na mafanikio ya kazi yako wala  huhitaji elimu kubwa ,Pesa n.k uaminifu upo ndani yako kazi kwako kuukuza na kuuboresha.CHONDE CHONDE" Usimuuzie mteja bidhaa kwa kumukomoa utampoteza".

Tumia pesa vyema
,Ukija kuangalia miongoni mwa
changamoto zinazowakabili wengi wakiwemo wajasriamali ni kwenye  matumizi ya pesa.Hii inaanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa, Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.Hivyo kuwa na  matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,Fedha ndio uti wa mgongo wa biashara yako ukiitumia vizuri itakudaidia ukiitumia ndivyosivyo hatamatokeo yake yatakuwa hivyohivyo.

"Ushindi upo mikononi  mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.

Saturday, September 21, 2019

Zijue kanuni bora za ujasriamali

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue kanuni za ujasriamali

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa na kuing'alisha siku yako na kuiona mpya.

Ujasiriamali una kanuni zake ambazo ni muhimu sana kuzijua na kuzifuata ili kuyafikia mafanikio ya kweli. Ili ufanikiwe katika Ujasiriamali kama ilivyo katika shughuli nyingine yoyote, zipo kanuni na misingi ziliyowekwa ili uzizingatie na kuzifanyia kazi .Mara  nyingi kanuni hizi ni kama mwongozo unaotuongoza katika kufanikisha jambo, kanuni hizi hapa:

Kujituma na kupenda  kazi unayoifanya,
Ni kweli kwamba kuna watu wanafanya kazi ambazo hawazipendi ila wanafanya tu ilimradi tu mtu apate kipato.Kama mjasiriamali ili ufanikiwe katika biashara yoyote, lazima uwe na moyo wa kujituma na uipende kazi unayoifanya. Usisubiri kusukumwa kwa sababu hakuna atakayefanya kazi hiyo. Jifunze kuwahi kuamka asubuhi ili uendane na kasi ya soko, jitume kufanya mambo yatakayoiboresha biashara yako bila kuchoka na fanya kazi kwa moyo wako wote.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa, hakuna kitu kinachompa mtu furaha kama kufanya anachopenda ,mtu wa aina hiyo awezi kuchoka,huwa yuko tayali kufanya kazi muda mwingi hata changamoto zinazojitokeza haziwezi kumnyumbisha.Hii ni kanuni bora kuizingatia kama mjasiriamali ili uweze kufika mbali kama unachofanya bado haujakipenda jitahidi ,ongeza juhudi Kaza """ dunia inakutegemea""".

Kuthubutu,
Mjasriamali bora ni yule mwenye uwezo na utayari wa kufanya maamuzi magumu ya kuingia kwenye biashara au mradi fulani huku akiwa ameondoa nidhamu ya woga na kuanza kupiga kazi.Ukweli ni kwamba kuna watu ambao  ni waoga wa kuchukua hatua ya kuanzisha biashara au  kuingia katika miradi fulani fulani sababu ya woga wa kushindwa mbeleni. Hasa hasa watu wengi huogopa kupata hasara na kuzomewa pindi waangukapo au wanapoyumba katika kuiendesha biashara au mradi walioanzisha.Kama  mjasiriamali bora ni lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya mambo makubwa ,ikiambatana na uelewa mkubwa zaidi baada ya kujiridhisha na kufanya biashara yako.Ili kuepuka kuanguka au kuyumba inabidi uwekeze katika kitu ambacho umefanya angalau utafiti ili ujue hekaheka zake kabla aujaanza kukifanya.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa hakuna mbadala wa mafanikio tofauti na kuthubutu na kuongeza juhudi katika kitu unachofanya.

Kuwa na usimamizi mzuri,
Kama mjasiriamali ambaye unahitaji kufika mbali kimafanikio kupitia biashara yako au mradi wowote unaoufanya ni vema zaidi
Kuwa na uwezo wa kuisimamia vizuri.
Hii inaambatana na kutoa maamuzi sahihi mara zote. Katika Ujasiriamali, uwezo wa kusimamia na kuwaongoza watu walio chini yako ni muhimu sana kwani hata kama ukianza na biashara ndogo, lazima baadaye itakuwa kubwa hivyo utalazimika kuajiri watu wengine wa kukusaidia ili kazi zako ziende.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.

Friday, September 20, 2019

Faida za kuwa mjasriamali bora

 MORNING MOTIVATION DIARY

Faida za ujasriamali

Ndugu,
Leo ni  siku nyingine tena kwenye program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuiboresha siku yako na kuifanya iwe mpya.Karibu tujifunze faida za kuwa mjasiriamali:

Kuongeza kipato,
Hii ndiyo dhana ambayo kila mmoja wetu anahihitaji.Unapokuwa mjasiriamali unakuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza kipato chako na kukudhi baadhi ya mahitaji ambayo pengine mshahara ulikuwa auyatimizi.
Kila mmoja ana ndoto nyingi ambazo anataka kuzitimiza,Kama ulikuwa unajiuliza utawezaje kuzitimiza basi jibu mojawapo ni kuwa mjasriamali ambaye anajituma na kufanya kazi kwa bidii.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,ili kuweza kuongeza kipato chako lazima uwe mpambanaji ,mbunifu inabidi uwe  mjasriamali ambaye anaenda na wakati.Tofauti na hapo utachukua muda mrefu kutimiza ndoto zako kama bado  auna vyanzo imara vya kipato chako.Hali ambayo itaendelea kukunyima Uhuru wako kifedha,Kumbuka mjasriamali wa Leo ni tajiri wa kesho.

Kuwasaidia watu wengine,
Katika kitabu cha My philosophy of success chake Jim Rhom katika sura ya pili kwenye "Falsafa ya utendaji na uzalishaji " anasema ili kufanikisha utajiri na ukuu katika dunia hii inabidi utafute namna ya kuwasaidia watu wengine.Tumia ujuzi wako kuhakikisha watu wanapata msaada wako, hivyo                     hutaweza kufanikiwa katika maisha yako kama bado auwasaidii watu wengine.Hapa ndipo watu wengi hufa wakiwa masikini bila wao kujua,kwa sababu ya kushindwa kuwasaidia watu wengine katika nyanja / kazi mbali mbali.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa unapokuwa kuwa mjasiriamali unakuwa na uwezo wa kuwaajiri watu,kuwapatia huduma bora na ukizingatia katika kanuni za biashara kwamba mteja siku zote ndiye bosi.Hivyo unapokuwa unatoa huduma bora kama mjasiriamali unakuwa unajihakikishia ukuu na utajiri unaunyemelea.Angalia wajasiriamali wakubwa jinsi wanavyowasaidia watu mbali mbali wenye uhitaji,na wanapowasaidia ndivyo kazi zao zinavyozidi kusonga mbele zaidi.Unachotoa ndicho unachopata ni sawa na unavuna ulichopanda,kupitia ujasriamali wako waoneshe wengine jinsi ya wao kufika pale hakika utakuwa katika nafasi kubwa ya kufanikiwa zaidi.

Kutatua matatizo na kutumia fursa,
Malengo makubwa ya watu kuingia kwenye ujasriamali ni kutoa huduma bora kwa watu , kwa kuwasaidia kuwapatia hudumabora.
Kama tunavyojua fursa nyingi zinatokana na matatizo tuliyonayo au mahitaji mbalimbali tunayoyahitaji katika maisha yetu ya kila siku.
Mfano kama kuna watu wana uhitaji wa maji katika jamii /mtaa uliopo ,kama mjasiriamali ukitengeneza mfumo wa kuwapatia watu maji tayali umetatua tatizo la maji na umetumia fursa hio.Hivyo unawapatia maji na wao wanakupatia Pesa,inakuwa ni win win situation.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa mafanikio yoyote tunayoyata yanategea sana kwa jinsi gani tunatoa huduma zilizobora kwa watu wanaotuzunguka.Hasa hasa kwa kutatua matatizo mbalimbali yanowakumba.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659
Lackius Robert karibu.

Thursday, September 19, 2019

Faida za kuwa mjasriamali

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue faida za kuwa mjasriamali,

Ndugu,
Karibu katika program nzuri ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa ,kuing'alisha siku yako na kuonekana mpya.Faida za kuwa mjasriamali:

Uhuru wa kifedha,
Ujasiriamali unatajwa moja ya shughuli kubwa ambayo endapo ikitumika vizuri na kwa malengo itakupa uhuru mkubwa wa kifedha.moja kati ya wajasiriamali niliobahatika kusoma makala zao ni Coach Bassanga yeye anasema aliamua kuwa mjasiriamali ili akidhi aweze kupata Uhuru kifedha.Anasema hakuna kitu ambacho kilikuwa kinamuudhi kama ikitokea shida ya pesa halafu huwezi ihimili.Kama ni mfanyakazi mpaka kusubiri mshahara utoke na kama siyo mfanyakazi unaangaika kuipata hiyo pesa .Kwa upande wa  mishahara Mara nyingi inapotoka watu wengi huwa wanalipa madeni waliyokopa hivyo ikija kufika tena mwisho wa mwezi tayali Pesa inakuwa imeisha.
Kwa mjasiriamali ambaye ana kitu kingine cha ziada cha kumuingizia kipato inamsaidia kukidhi mahitaji mengine sio kutegemea mshahara.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,tafiti nyingi zinaonesha mshahara hautoshelezi mahitaji ya watu ,hivyo kama unahitaji kupata Uhuru wa kifedha unaweza anzisha kitu cha ziada cha kukuingizia Pesa ili usiwe unategemea mshahara tu.Coach Bassanga anasema "mjasiriamali wa Leo ni tajiri wa kesho".

Ujasiriamali utakupa nafasi ya kufanya kile unachokipenda.
Tafiti na takwimu nyingi zinaonyesha kuwa asilimia kubwa  ya watu,wanafanya kazi ambazo hawazipendi ila wanafanya tu kwa sababu hawana namna nyingine ya kujiingizia kipato. Hivyo uamua kukomaa nazo hivyo hivyo  ili kusogeza siku ,lakini kwa wafanyakazi wanaoamua kufanya pia ujasiriamali wanapata fursa ya kuwa na unafuu.Maana kwenye ujasriamali unafanya kilicho moyoni bila kushinikizwa na mtu wala kulazimishwa.
Kupitia ujasiriamali utaamua nini ukifanye na kwa wakati gani,wapi na lini kulingana na matakwa yako.
Hapa wewe mwenyewe unaamua biashara ipi ufanye ,kulingana na nafasi /muda ulionao inaweza kuwa ya nguo,chakula,vinywaji na vingineo.Ili uweze kujipatia kipato cha ziada na kuanza kukidhi baadhi ya mahitaji mengine ambayo kazi uliyokuwa unaifanya awali ilikuwa aijakidhi.

Uwezo wa kupanga ratiba yako binafsi.Sana sana hii ipo kwa watu ambao wameamua kuwa wajasiriamli moja kwa moja.
Pamoja na ukweli kwamba unatakiwa kufanya kazi kwa bidii sana na kuwa na usimamizi thabiti kama mjasiriamali, ukweli ni kwamba unakuwa na  uhuru wa kupanga ratiba na muda wake kulingana na vipaumbele ulivyonavyo. Hii ni tofauti kabisa na mtu ambaye yeye huuza muda wake kwa mwajiri ili aweze kujipatia kipato.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,kila mtu anawaweza kufanya ujasriamali na kuwa miongoni mwa watu wenye mafanikio makubwa.Kitu ambacho bado kinatukwamisha ni maneno na mipango ,yaani tuna mipango mingi sana.Unaweza kuzungumza na mtu akawambia mipango mpaka ya 2025 lakini ukimuliza ambayo ametimiza kwa sasa utasikia ,unajua kuna mtu namsubilia kidogo,muda sio mrefu ntaanza inafika mpaka mwakani ajaanza.Kama mjasiriamali panga jambo na ulitende muda unao unaweza kuutumia vyovyote unavyoweza.
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert
Karibu.

Wednesday, September 18, 2019

Zijue sifa za mjasriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue sifa za mjasiriamali bora

Ndugu
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:

Mtu mwenye kuongeza bidii,
Moja kati ya msemo unaopendwa kutumiwa na mwandishi na muhamasishaji Rodrick Nabe ni huu "Mafanikio ni mchakato" hivyo mafanikio huja kwa wale ambao wanakuwa na bidii kubwa kuyatafuta.Kama mjasiriamali ni vema kuongeza juhudi katika mambo mbali mbali ambayo yanaweza kukuvusha kutoka hatua moja hadi nyingine ,ikiwemo kuongeza bidii katika kujifunza vitu vipya ili kuenenda na kasi ya mabadiliko kwenye ulimwengu huu.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa
Bidii ni msingi wa kufanikiwa kwenye jambo au shughuli yoyote,pia ni muhimu kukumbuka kuwa mjasiriamali ni mwajiri na ni boss wake yeye mwenyewe. Ni vema kuongeza bidii binafsi pamoja na  kujituma katika kufanya kazi bila ya kusukumwa na mtu yeyote.

 Kujifunza kutokana na makosa,
Kuna ukweli usiopingika kuwa "makosa ni shule muhimu kwa kila mtu", ndivyo ilivyo pia kwa mjasiriamali ambaye ana malengo ya kufika mbali.
Mjasiriamali anapaswa kuwa na sifa ya kupenda kujifunza kutokana na makosa ili asiyarudie tena mbeleni na wala si kuyaogopa au kuyakimbia.
Kama uliwekeza pesa zako zikapotea, basi usiache ujasiriamali bali baini ni nini kilisababisha ukapoteza pesa zako ili ukiepuke mbeleni.
Kuanza biashara kutoka kiwango cha kidogo mpaka kuwa mjasiriamali mkubwa siyo kazi ya mchezo mambo mengi inabidi uyafanye.Kama mjasiriamali utakutana na changamoto nyingi. Hili haliwezi kuwa tatizo ikiwa uko tayari kujifunza kutokana na makosa na kufahamu njia za kuyaepuka huko mbeleni. Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wanavyojifunza na kukua zaidi na zaidi.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa usemi wa kosa siyo kosa bali kurudia kosa ndilo kosa,hivyo unapokuwa kwenye biashara au kazi yoyote ni lazima ufahamu makosa ambayo yanaweza kuathiri biashara au uwekezaji wako ,mfano makosa kama ,kujifanya unajua kila kitu,kutaka wateja wakufuate,matumizi yasiyo mazuri ya fedha,kupuuza baadhi ya mambo.Hii inakusaidia kuongeza umakini katika mambo yako mwisho wa siku inakusaidia kulitimiza lengo lako.

Mtu ambaye ni dynamic (anayeenda na mabadiliko),Mjasiriamali bora ni yule asiye static kwa maana ya kubakia tu na kitu alichonacho miaka nenda miaka rudi bali ni yule ambaye anaenda na mabadiliko.Kwa sababu kuna mabadiliko makubwa kiuchumi,kiteknolojia ,kisiasa ,kimazingira pia na kimahitaji.
Ili kuenenda vizuri ni vema kuongeza juhudi ya kuangalia nini kinahitajika ,na nini kiboreshwe zaidi ili uhutaji wake uendele.Hasa hasa katika utoaji bidhaa mbalimbali kwenda kwa watumiaji hivyo unavyokuwa unabadilika kuenenda na mabadiliko ndivyo unavyozidi kuwa sokoni tofauti na wale wasio na mabadiliko katika utoaji wa huduma.

Ndugu yangu mpendwa ni imani yangu kuwa sifa za ujasriamali bora umezielewa zaidi na utazifanyia kazi.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert.
Karibu.

Tuesday, September 17, 2019

Sifa za mjasiriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue sifa za mjasiriamali bora,

Ndugu,
Ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:

Mtu anayejitahidi kutafuta taarifa,Kama unavyojua sasa hivi tuko kwenye kipindi ambacho teknolojia inakua kwa kasi ,na mambo yanabadilika kila uchao ili kuendanana na kasi hiyo ni muhimu kusaka taarifa zaidi.
Mjasiriamali bora anatafuta taarifa kutoka sehemu mbalimbali kwa watu tofautitofauti kama vile wateja, washindani,kusoma vitu mbali mbali ikiwemo vitabu husika.
Pia hufanya utafiti binafsi wa namna mbalimbali za kuvutia wateja na kuboresha huduma bora ili kuongeza wigo wa wateja na kipato kwa ujumla.
Mjasiriamali Pia uomba ushauri kutoka kwa wataalamu na  wadau mbalimbali wa masoko kulingana na biashara anayofanya lengo kubwa ni kuongeza uelewa zaidi.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa, taarifa sahihi zinaleta maarifa sahihi ukiwa na chanzo chenye taarifa sahihi unakuwa na uwezo mkubwa wa kufanikiwa kwenye unachofanya.Je ni taarifa gani unapokea au unaingiza ? Chanzo chako cha taarifa ni kipi? Ukipatia majibu hakika hautabakia hapo ulipo.

Mtu mwenye nidhamu,
Mtaalamu wa mafanikio na mjasiriamali mkubwa Jim Rhon aliwahi kusema "nidhamu binafsi ndiyo daraja la malengo( goals)na unapokwenda")(destination)
Nidhamu ni sifa muhimu sana  kwa mjasiriamali kwani itamtenga na mambo mengi yasiyokuwa na umuhimu. Ni lazima mjasiriamali awe na nidhamu ya maswala kama vile matumizi ya muda pamoja na pesa.
Mjasiriamali bora ni yule anayeweza  kujinyima na kukataa vitu vyote ambavyo havimwezeshi kufikia malengo yake.
Ndugu yangu mpendwa sijamanisha kujinyima kila kitu ,nachomanisha vitu ambavyo havikufikishi kwenye malengo yakob.Simamia nidhamu yako kwa kutumia muda vizuri,Maana muda uliopoteza hauwezi kujirudia.
Upande wa Pesa unahitaji nidhamu ya hali ya juu sana maana walio wengi hapo pana wasumbua,heshimu sana kilicho kwenye ratiba au kipaombele hakika utakuwa mjasiriamali bora zaidi.Nidhamu yako bora mafanikio yako.

Mtu mwenye uvumilivu,
Kuna ukweli usiopingika kwamba kila jambo lina changamoto zake katika kulitenda. Ujasiriamali una changamoto nyingi ambazo zinahitaji uvumilivu ili kuzimudu na kuyafikia malengo uliyopanga.

Naomba niishie hapo tukutane wakati ingine.
Kwa mawasiliano 0767702659 Lackius Robert. Karibu.

Monday, September 16, 2019

Sifa za mjasiriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Ujasiriamali na mafanikio

Ndugu
Karibu katika siku nyingine tulivu kwenye morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.

Ujasiriamali ni uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazojitokeza na kugeuza au kutumia changamoto hizo kama fursa.
Mjasiriamali anabuni bidhaa mpya au njia mpya ya uzalishaji wa bidhaa ambayo soka linahitaji bidhaa hiyo au huduma hiyo ambayo haijapata kusambazwa hapo kabla.
Nikumbushe ndugu yangu mpendwa Ili kubobea katika ujasiriamali unatakiwa kuwa MJASIRI Pamoja na kutumia vizuri MALI ULIZONAZO.Kwa kufanya hivyo utakuwa umekamilisha neno zima la MJASIRIAMALI.
mfano katika mtaa au eneo fulani  kuna shida kubwa ya maji basi mjasiriamali atakabiliana changamoto hiyo kwa kuchimba kisima cha maji na hatimaye atakuwa ametatua changamoto hiyo ya maji na kugeuza kuwa fursa.Ambapo atakuwa anawauzia watu maji lakini wakati huo huo anapata kiasi fulani cha fedha.

Kwa hakika ujasiriamali ni chaguo muhimu sana kwenye karne hii ya sasa ili kujiongezea kipato zaidi na zaidi.
Wataalamu wanasema.
 “Siri ya mafanikio yeyote ni kutokukata tamaa katika kazi tunazofanya".Jaribu kuangalia wajasiriamali wadogo wadogo jinsi wanavyofanya kazi bila kujali mazingira yakoje wanavyofanikiwa.Kina mama wauza mbogamboga,migahawa ,watu wanaouza bidhaa za kutembeza wanapata Pesa.Unapochagua kuwa mjasiriamali haupaswi kuwa mtu wa kuyumbishwa na kuendeshwa na watu bali kile unachoona jamii inaweza kunufaika nacho.
Zijue sifa za mjasiriamali
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:

1.Uwezo mkubwa wa kuona fursa na kuifanya kazi,
Mjasiriamali mzuri ni vizuri uwe na jicho la kuona fursa au kuona kitu gani kinahitajika  katika jamii inayokuzunguka.Ndio maana Muasisi wa fursa Lughe Mutahaba aliwahi kusema "Matatizo yetu ndio fursa zenyewe".
 Mjasiriamali ni vema kuziangalia changamoto zinazojitokeza katika jamii yako na kutumia changamoto hiyo kama fursa kwako. Kwa mfano sehemu unayokaa watu wanauhitaji wa huduma za kibenki kama vile (tigo pesa, m-pesa ,airtel money )ukifungua kibanda tayali tatizo umelitatua na umejitengenezea fursa,Mahitaji muhimu ya kutumia nyumbani katika mapishi.Bidhaa za urembo ,dukani kama mafuta vyakula n.k.

2.Unahitaji kuwa mbunifu,UBUNIFU  naweza sema ni  matumizi ya njia bora zaidi zinazokidhi kutatua changamoto mpya, changamoto ambazo tayari zipo lakini hazijapatiwa ufumbuzi bado, au changamoto zilizopo kwenye soko au jamii kwa kipindi husika.Dhana hii hutimilika pale ambapo bidhaa, huduma, teknolojia, mpangilio  wa biashara au njia nyingine yoyote inayoweza kutatua changamoto husika.Unaweza kubuni kitu kipya au kuboresha kilichopo,
Kama mjasiriamali yakupasa uwe mbunifu ,hata kwa bidhaa au huduma ambayo wanaokuzunguka wanayo ,unajaribu kutengeneza utofauti fulani .Kitu kinachomfanya mtu kuja kuchukua bidhaa kwako na sio kwa mwingine kama ni una kibanda cha chips mfano ,mandazi ,chapati au mgahawa,genge, n.k .

Hali hiyo inamfanya mteja kurudi ,Sam Walton ambaye ni mwanzilishi wa  WalMart anasema "Hakuna bosi kama mteja" kwa sababu ndiye anayetulipa hivyo ni jukumu lako kubuni namna ya kumshawishi katika bidhaa au huduma yoyote unayotoa. Nikukumbushe ndugu yangu '''Ubunifu wako ndio mafanikio yako'''.

3.Mtu anayependa kuongeza jitihada katika kutenda (practice),
Mara nyingi ujasiriamali mzuri ni ule wa vitendo,pamoja na kubadilisha mawazo (ideas) kuwa vitendo halisi. Hivyo mjasiriamali ni mtu anaechukua hatua na kutenda bila kujali vikwazo pia hachoki wala kukata tamaa.
Anaposhindwa hili hufanya lile au hubadilisha mbinu ili kufikia malengo aliyokusudia.
Ukijaribu kuangalia watu wengi wanayo mawazo mengi mazuri lakini inapofika wakati wa utendaji kama ni kuanzisha duka ,genge ,mgahawa ndipo utata unapoanzia sababu zinakuwa nyingi.Mara oh kuna mchakato Fulani nausikilizia ,Mipango haijakaa sawa au anasubilia ukamilifu wa kitu Fulani ndo aanze.Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa kesho imewaponza wengi,Anza leo ,majasiriamali bora ni yule anayekubali kuingia katika utendaji sio maneno na sababu nyingi ,Jiulize kama kesho sijui inavyofanana kwa nini nisianze?.

4.Mtu mwenye anayeweka malengo ,Kuna usemi unaosema "" kama hujui unapokwenda basi popote wewe unakuwa umefika""
Ili kujiboresha zaidi mjasriamali bora huweka malengo ya nini anataka afanye kwa muda fulani .
Ninaamini na wewe ndugu yangu mpendwa ambaye ni mjasiriamali kuna malengo umeyaweka.Faida kubwa ya kuweka malengo ni kwamba inakusaidia kukupa mwongozo(guideline) na kufanya uachane na vitu amabavyo sio vya msingi au vilivyopo nje ya malengo.

Malengo anayoweka huwa  ni ya muda mfupi (short term goals ) na  ya muda mrefu (long term goals) baada ya kuyaweka huwa anajituma zaidi ili kuyakamilisha malengo hayo.
Malengo hayo lazima yawe makubwa yanayoweza kufikika yasiwe madogo yanayoweza kukufanya kuwa MZEMBE wala yasiwe makubwa sana yasiyofikika. Kama wengi tunavyojua mafanikio ni mchakato.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Naomba niishie hapo tukutane wakati mwingine.
Lackius Robert unaweza kuwasiliana na Mimi kupitia 0767702659.



Wednesday, September 11, 2019

Mti kukua vizuri unahitaji ukomavu

MORNINGS MOTIVATION DIARY

Ili mti uzae vizuri mizizi inahitaji ukomavu na maji.

Ndugu,
Karibu katika siku nyigine tena ambapo tunakuatana katika program ya morning motivation diary ,yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa na kuing'alisha asubuhi yako.

Katika maisha yetu ya kila siku ili kuwa na ufanisi mzuri katika shughuli tunazofanya tunahitaji kuwa na ukomavu mzuri.Ukomavu unaoendana na maarifa ya kutosha katika kile tunachofanya.

Ukiangalia fishing law inasema "kamwe huwezi kupata samaki wakubwa katika sehemu yenye kina kifupi" .Hivyo basi ili tuwe na ukomavu mzuri katika shughuli tunazofanya na kutimiza malengo yetu .Lazima tupanue mawazo na kuanza kuwa na ndoto kubwa.

Maana Ukiwaza kidogo utapata kidogo,
Ukiwaza kikubwa utapata kikubwa maana mwili,akili,fikra zako zote zinawaza kikubwa na hautachoka.Lakini ukiwaza kidogo ndivyo mwili utakavyolegea maana kitu kidogo mara nyingi ni cha muda mfupi.

Mti mdogo mizizi yake hata umwage maji mengi kiasi gani haiwezi kwenda mbali sana lakini mti mkubwa mizizi yake husambaa na kwenda mbali zaidi.

Usisubili upewe kila kitu ndo ufanye jambo,Imwagilie akili yako kwa kuendelea kujifunza kitu kipya kila siku.
Anza na kidogo vingine vitakukuta njiani.Usiwe na mawazo kama ya  mtu anayesema kama napewa maziwa kila siku yanini kufuga Ng'ombe'''.Anaamini siku zote ataendelea kupewa ,anashindwa kuwaza yajayo anawazia yaliyopo na yanayoonekana mbele yake.
Wish you all the best.

 " Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa ".

Nikukaribishe ili uzidi kujifunza zaidi na zaidi pia tembelea page yangu ya Instagram jina lackius Robert.Karibu

Saturday, August 17, 2019

Vijue vichocheo vya mgogoro ili uishinde migogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Vichocheo vya migogoro:

Ndugu,
Ni siku nyingine tena tunakutana katika morning motivation diary yenye lengo kubwa kuongezea maarifa na kuing'alisha siku yako.
Karibu katika mwendelezo wa vichocheo vya migogoro:

Ubaguzi (Descrimination) Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakibaguliwa miongoni mwa sehemu za kazi kutokana hali fulani fulani.
Ukiangalia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu kidogo cha 7 inakataza ubaguzi wa aina yoyote katika sehemu za kazi iwe rangi,ugonjwa ,dini,kabila,.
Hivyo katika sehemu ya kazi ikitokea mtu kubaguliwa mgogoro mkubwa unaibuka kwa sababu ,inaonesha thamani yake aionekani ,pia mchango wake hauonekani kuthaminiwa.Binadamu sote ni sawa tukiondoa tofauti zetu za kikabila kidini.

Matarajio usiyoyatarajia (unrealistic expectations).
,Hali huchochea  migogoro zaidi hasa pale ambapo mmojawapo anapokuwa anatarajia kupata kitu Fulani.Mfano Mshahara labda mwisho wa mwezi ikatokea hajaupata hivyo siku zimeongezwa mbele. Labda ameongeza elimu akitarajia kupandishwa cheo(promotion) na kuongezeka kwa bonus lakini hivyo vyote vikawa havijatendeka.Matarajio yake yanakuwa tofauti na alivyoyanga hivyo usababisha kuongezeka kwa mgogoro kati yake na wshusika ofisini.Inaweza kusababisha presenteism yani mfanyakazi yupo kama hayupo kazini.

Mawasiliano hafifu,
Ili kazi iweze kufanikiwa zaidi inahitaji uwepo wa ushikiriano mzuri unaoambatana na mawasiliano mazuri.
Maana kila mmoja atatimiza wajibu wake ikiwemo kuhudhulia mikutano husika ikihitajika,kubadilisha mawazo na mambo mengine ili kazi ziweze kwenda zaidi.
Mawasiliano yanategemea sana maneno inabidi kuhakikishia kuwa mawasiliano yako yanaenda zaidi ya maneno.Ikiwa unazungumza na mtu mmoja au zaidi tambua maneno pia matendo yanaweza kuathiri uhusiano wako pamoja na ukweli utakaoutoa kutumia maneno sahihi na hisia sahihi, wakati wa kuzungumza na mtu.

Pindi mawasiliano yakosapo kuna baadhi ya kazi hazifanyiki kwa wakati kitu kinachopelekea mgogoro kuibuka.

Kukosekana uaminifu ,Kuna usemi unaosema uaminifu ni mtaji.Hivyo katika sehemu za kazi ata ili ufanisi uongezeke uaminifu inabidi uwepo.Kwa maana ya kwamba mfanyakazi anaweza achiwa kazi zingine kama anaaminiwa akazimalizia bila ofu.

Lakini kama uaminifu aupo miongoni mwa wafanyakazi hali hii husababisha baadhi kukosa fursa,au kutopewa kazi badala yake wanapewa waaminifu.Hali hii huibua mgongano mkubwa kwanini wengine wanaachiwa au kupewa kazi ama pengine kupandishwa vyeo na wengine hawapandishwi. Je hali ikoje katika sehemu unayofanyia kazi?. Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert

Wednesday, August 14, 2019

Vijue vichocheo vya mgogoro ili kuepuka mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Vichocheo vya migogoro:

Ndugu,
Inawezakana katika sehemu ya kazi migogoro isiwepo lakini ni  nadra sana kutoka na asili ya migogoro.
Tunasema migogoro ni "HISIA ZILIZOLALA" ukiziamsha zinaamka.
Karibu tuangalie vichocheo vya migogoro:

Migogoro binafsi
Wapo wafanyakazi wengine  huruhusu  migogoro  yao  binafsi, ambayo  haihusiani ,kuharibu kazi zao.Labda Unakuta mfanyakazi Fulani na fulani wana  mgogoro  wa  kinafsia  ambao unahamishwa  kwa  wafanyakazi wengine na  kusababisha  kutoelewana.  Akitokea mtu  anataka kuwakosoa au  kuwashauri waache hiyo migongano wanakataa kuongea  naye.  Na wakiongea wanaongea kwa ukali  na  matusi hali hiyo inachochea mno usambaaji wa  Mgogoro katika sehemu za kazi .Migogoro hio mara nyingi hutokana na wivu wa maendeleo yaani mtu fulani hataki fulani afanikiwe,Akiona ana maendeleo fulani nafsi inamuuma, kama ni mfanyakazi mwenzie anaanza chokochoko ndogo ndogo baadae mgongano kamili.

Kutomsikiliza mtu (Not hearing not listening).Watafiti wanasema watu wengi wamekuwa wakichochea migogoro bila kujua ,kutokana na kutotoa nafasi ya mtu kujielezea.
Kusheria tunasema kila mtu ana haki ya kusikilizwa" right to be heard" ambayo inampa mtu uhuru kujielezea. Wakati mwingine mtu amechelewa kazini au nyumbani kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake ila akifika unamfokea uku ukimwambia maneno makali na magumu.Akitoka hapo anaona thamani yake aieshimiwi mgogoro tayali unakuwa katika hatamu.
Nakusihi usikose makala ijayo ,wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"
Unaweza kuwasiliana na mimi 0767702659
Au katika page yangu Instagram Lackius Robert.
Karibu

Tuesday, August 13, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

 Jinsi kazi(Workplace conflict) inavyoathiri falimia.

Ndugu,
Kama ilivyo kwenye familia kwamba familia ikiyumba na kazini panayumba pia.
Ndivyo ilivyo kazini na kwenye familia pia panayumba:
Karibu tuone jinsi kazi inavyoleta migogoro katika familia:

Kama mshahara ni mdogo (Insufficient wage),Mfanyakazi anafanya kazi ili apate kipato cha kuisaidia familia kama kipato ni kidogo,alafu anafanya masaa mengi kwa long working hours.Hali hii usababisha migogoro kwa sababu familia itashindwa kumuelewa muhusika kwa kutotoa baadhi ya mahitaji.

Mikutano isiyotarajiwa(unexpected meeting) mfano muda wa kazi unaisha hivi pa! Unaambiwa kuna kikao mnakaa kwa muda kadhaa.Hivyo nyumbani ukitoa taarifa unaambiwa umeanza njia ya pembeni kelele zinaanza mkishindwa kuelewana mapigano kususiana.

Safari nyingi extensive travel hizi pia husababisha mgogoro kwa sababu mmoja wapo anaweza hisi kuna namna fulani.Katika kazi kama ni mwanaume unaweza hisiwa kuwa na nyumba ndogo mkishindwa kuelewana mgogoro tayali unaanza.

Pia vyote hivi husababisha kukosa muda mzuri kwa mazazi  kuzungumza na watoto, mzazi anaondoka usiku anarudi usiku wikend anaudhulia vikao hali inayopelekea watoto kutopata malezi bora kutoka kwa wazazi wote.
Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Unaweza kuwasiliana na Mimi 0767702659
Au ukatembelea page yangu ya Instagram lackius Robert
Karibu.

Monday, August 12, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Hivi ndivyo migogoro ya familia inavyoleta athari katika sehemu za kazi.

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena katika program ya morning motivation diary yenye lengo la kuing'alisha siku yako.

Ni wazi kwamba kila mfanyakazi anatokea kwenye familia,Yaani anatoka nyumbani anaenda kazini hivyo nyumbani kukiwa na amani pia kazini patakuwa na amani.
Chunguza mifano hii katika familia kama uchumi umeyumba mmoja wapo labda mwanaume akauza kitu au Mali bila kutoa taarifa kwa mkewe pindi kile kitu au mali ikija kuchukuliwa mwanamke atokuwa na amani na mgogoro utaanza ,pindi akienda kazini atakama anafanya kazi baadae atakuwa na mawazo maana nyumbani mambo apako sawa.

 Mmojawapo amezaa nje ya ndoa hali itakayoanzishwa hapo ni balaa kelele zitakuwa nyingi sana hadi kufikia hatua ya kupigana katika kupigana kwa bahati mbaya mmoja akiumia kinachofuata ni kwenda hospitali kitu kinachopelekea kutoudhulia kazini sababu ni malumbano na mapigano.

Talaka wawili walikuwa wanapendana pindi wanapotalakiana inachachukua siku zisizopungua angalau 14 ili kuona umeanza kupata unafuu kidogo wa mawazo  pia na kuzoea hio hali ,kipindi chote hicho kinakuwa kinaathili utendaji wa kazi maana mfanyakazi anakuwa yupo kazini  kama hayupo (presenteeism) badala ya kufanya kazi anawaza namna ya kurejesha furaha au amani kwenye moyo wake.

Nikumbushe tena mfanya kazi anatoka kwenye familia hivyo ni wachache wanaoweza kuhimili hekaheka hizo.Familia ikiyumba kazini pia panayumba maana kuna uhusiano mkubwa kati ya familia na kazini .
Kama una maoni au ushauri kuhusu makala hizi  naomba unijulishe. Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kupata makala zilizopita bonyeza hapa
https://www.instagram.com/p/B0kJTHfFJNt/?igshid=17zwddxlmeig5

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Hivi ndivyo migogoro ya familia inavyoleta athari katika sehemu za kazi.

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena katika program ya morning motivation diary yenye lengo la kuing'alisha siku yako.

Ni wazi kwamba kila mfanyakazi anatokea kwenye familia,Yaani anatoka nyumbani anaenda kazini hivyo nyumbani kukiwa na amani pia kazini patakuwa na amani.
Chunguza mifano hii katika familia kama uchumi umeyumba mmoja wapo labda mwanaume akauza kitu au Mali bila kutoa taarifa kwa mkewe pindi kile kitu au mali ikija kuchukuliwa mwanamke atokuwa na amani na mgogoro utaanza ,pindi akienda kazini atakama anafanya kazi baadae atakuwa na mawazo maana nyumbani mambo apako sawa.

 Mmojawapo amezaa nje ya ndoa hali itakayoanzishwa hapo ni balaa kelele zitakuwa nyingi sana hadi kufikia hatua ya kupigana katika kupigana kwa bahati mbaya mmoja akiumia kinachofuata ni kwenda hospitali kitu kinachopelekea kutoudhulia kazini sababu ni malumbano na mapigano.

Talaka wawili walikuwa wanapendana pindi wanapotalakiana inachachukua siku zisizopungua angalau 14 ili kuona umeanza kupata unafuu kidogo wa mawazo  pia na kuzoea hio hali ,kipindi chote hicho kinakuwa kinaathili utendaji wa kazi maana mfanyakazi anakuwa yupo kazini  kama hayupo (presenteeism) badala ya kufanya kazi anawaza namna ya kurejesha furaha au amani kwenye moyo wake.

Nikumbushe tena mfanya kazi anatoka kwenye familia hivyo ni wachache wanaoweza kuhimili hekaheka hizo.Familia ikiyumba kazini pia panayumba maana kuna uhusiano mkubwa kati ya familia na kazini .
Kama una maoni au ushauri kuhusu makala hizi  naomba unijulishe. Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kupata makala zilizopita bonyeza hapa
https://www.instagram.com/p/B0kJTHfFJNt/?igshid=17zwddxlmeig5