MORNING MOTIVATION DIARY
Zijue kanuni za ujasriamali,
Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongeza maarifa na kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.Karibu katika mwendelezo unaoelezea kanuni ambazo mjasiriamali anapaswa kuzizingatia:
Kuwa na umakini,hii ni moja ya kanuni bora kwa sababu ndiyo inayosababisha biashara au mradi wako kusonga mbale maana kila kitakachofanyika kinahitaji umakini mkubwa.Katika kuajiri,katika kusambaza huduma ,katika kuzungumza na wateja n.k
Ukiangalia waliofanikiwa siyo tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi walizokuwa wakifanya. Kama mjasiriamali unatakiwa kuwa mwangalifu kwa kila jambo, unatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe na uelewa wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko, uzalishaji na uendeshaji kwa jumla.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,
Kushika namba moja kwenye kile unachofanya siyo bahati ila ni umakini mkubwa.
CHONDECHONDE "Mazuri ya dunia ni mengi na yapo kila sehemu kuwa makini usipotee njia".
Umuhimu wa kuwa mwaminifu,Kama mjasiriamali mwenye malengo makubwa ya kufika mbali kanuni hii ni muhimu kuifanyia kazi na kuenenda nayo.
Maana uaminifu ni silaha kubwa itakayokulinda mjasiriamali na kuwafanya watu wengi wapende kufanya biashara na wewe au kuwekeza kwenye miradi yako.Ni vema kuwa mwangalifu katika kulipa madeni hata kama ni madogo unapodaiwa, pia wauzie wateja wako huduma au bidhaa kwa bei halali.Kama tunavyojua serikali yetu inajiendesha kwa kutumia kodi hivyo mjasiriamali ni vema sana kulipia kodi na vibali vyote muhimu vinavyohitajika ili kukuweka katoka hali ya uhuru pindi uwapo kazini .Ili kuboresha huduma zako usiwe unatoa bidhaa zilizokwisha muda ,zingatia kutoa bidhaa bora maana mteja anapokuja kwako anakuwa anakuamini hivyo zidisha uaminifu kwake ili kesho arudi.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa "Uaminifu wako ndio mtaji na mafanikio ya kazi yako wala huhitaji elimu kubwa ,Pesa n.k uaminifu upo ndani yako kazi kwako kuukuza na kuuboresha.CHONDE CHONDE" Usimuuzie mteja bidhaa kwa kumukomoa utampoteza".
Tumia pesa vyema
,Ukija kuangalia miongoni mwa
changamoto zinazowakabili wengi wakiwemo wajasriamali ni kwenye matumizi ya pesa.Hii inaanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa, Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.Hivyo kuwa na matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa,Fedha ndio uti wa mgongo wa biashara yako ukiitumia vizuri itakudaidia ukiitumia ndivyosivyo hatamatokeo yake yatakuwa hivyohivyo.
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"
Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.

No comments:
Post a Comment