MORNING MOTIVATION DIARY
Mambo usiyoyajua kuhusu ujasriamali
Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika programu yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako kwa kukuongezea maarifa na kuifanya kuwa mpya.
Hakuna njia ya mkato kwenye ujasiriamali,
Watu wengi wamekuwa wanaingia kwenye ujasiriamali kwa mtazamo kwamba ni njia ya mkato na ya haraka ya kupata fedha. Ndiyo maana watu wamekuwa wanatumia muda mwingi kukimbizana na fursa zinazojitokeza ili wapate mafanikio haraka.
Lakini ukweli ni kwamba ujasiriamali unahitaji ufanye kazi, utumie muda wako kujifunza pia kuwa na uvumilivu katika yale unayofanya.
Ukijaribu kuangalia kuna watu wamedanganywa sana kuhusu fursa mpya mpya ambazo zimekuwa zikijitokeza kila siku. Wamepewa hesabu za kwenye karatasi, zikawahamasisha, wakaingia kichwa kichwa na kupata hasara kubwa sana.Mwishowe kuanza kujilaumu kwa maamuzi waliyoyafanya.
Nikukumbushe ndugu mpendwa ,ujasiriamali unahitaji ujipange kama kweli umeamua kuufanya na kuwa tayali kupambana na kila hali itakayokutokea.
Kama inawezekana anzia sehemu yenye mkusanyiko kidogo,
Malengo makubwa ni kujifunza zaidi maana unapoanzia padogo kuna vitu vingi unavielewa zaidi kuliko kuanzia pakubwa maana kuna baadhi ya changamoto utazifahamu na kujifunza jinsi ya kuzitatu.Sasa Kosa kubwa ambalo watu wamekuwa wanalifanya kwenye ujasiriamali ni kuiga wengine. Mfano wanapoona wengine wanafanya biashara fulani, hujiambia hiyo biashara inalipa na hivyo huamua kuifanya matokeo yake kushindwa kuiendeleza baada ya kutoenda vizuri.
Kama mtu anayetaka kufanikiwa kwenye ujasiriamali, unapaswa kwenda sehemu yenye mkusanyiko mdogo, kwa kufanya kile ambacho hakuna wengine wanaokifanya.na kama kuna wanaofanya, basi wewe unakuwa na utofauti fulani fulani.
Ambacho wateja wako hawawezi kukipata sehemu nyingine isipokuwa kwako pekee.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,una uwezo wa kufanya kitu kikaonekana cha upekee maana hakuna mtu mwingine ambaye ni bora zaidi yako,na upekee ulionao ni mkubwa kama yupo anakarbia kufanana na wewe ila hawezi kulingana na wewe.
Unapofanikiwa katika biashara moja hakumanishi unajua biashara zote,
Mafanikio kidogo kwenye ujasiriamali kwa wengi imekuwa kikwazo kwa mafanikio makubwa zaidi. Mtu anaanzisha biashara moja, inafanikiwa na kufanya vizuri na hapo ndipo kushindwa kunapoanza. Wengi uamini kwa kiwa wamefanikiwa kwenye biashara moja, basi wanaweza kufanikiwa kwenye kila aina ya biashara zingine.Hivyo huanza kujihusisha na biashara nyingine nyingi na tofauti tofauti kwa kuamini uzoefu wao kwenye biashara moja utawasaidia kwenye biashara nyingine wanazoanzisha.
Hali hii imekuwa inafanya wengine kurudi nyuma kimafanikio maana wanapoanzisha biashara yingine huweka nguvu nyingi kule tofauti na ilivyokuwa awali.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,Biashara zinatofautiana na pia zina changamoto ambazo ni tofauti tofauti ,hivyo unapofanikiwa kwenye biashara ya aina fulani, ni vyema kuendelea kuweka nguvu ili ufanikiwe zaidi.
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"
Kwa mawasiliano zaidi 0767702659
Lackius Robert karibu.

No comments:
Post a Comment