Wednesday, September 18, 2019

Zijue sifa za mjasriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue sifa za mjasiriamali bora

Ndugu
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:

Mtu mwenye kuongeza bidii,
Moja kati ya msemo unaopendwa kutumiwa na mwandishi na muhamasishaji Rodrick Nabe ni huu "Mafanikio ni mchakato" hivyo mafanikio huja kwa wale ambao wanakuwa na bidii kubwa kuyatafuta.Kama mjasiriamali ni vema kuongeza juhudi katika mambo mbali mbali ambayo yanaweza kukuvusha kutoka hatua moja hadi nyingine ,ikiwemo kuongeza bidii katika kujifunza vitu vipya ili kuenenda na kasi ya mabadiliko kwenye ulimwengu huu.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa
Bidii ni msingi wa kufanikiwa kwenye jambo au shughuli yoyote,pia ni muhimu kukumbuka kuwa mjasiriamali ni mwajiri na ni boss wake yeye mwenyewe. Ni vema kuongeza bidii binafsi pamoja na  kujituma katika kufanya kazi bila ya kusukumwa na mtu yeyote.

 Kujifunza kutokana na makosa,
Kuna ukweli usiopingika kuwa "makosa ni shule muhimu kwa kila mtu", ndivyo ilivyo pia kwa mjasiriamali ambaye ana malengo ya kufika mbali.
Mjasiriamali anapaswa kuwa na sifa ya kupenda kujifunza kutokana na makosa ili asiyarudie tena mbeleni na wala si kuyaogopa au kuyakimbia.
Kama uliwekeza pesa zako zikapotea, basi usiache ujasiriamali bali baini ni nini kilisababisha ukapoteza pesa zako ili ukiepuke mbeleni.
Kuanza biashara kutoka kiwango cha kidogo mpaka kuwa mjasiriamali mkubwa siyo kazi ya mchezo mambo mengi inabidi uyafanye.Kama mjasiriamali utakutana na changamoto nyingi. Hili haliwezi kuwa tatizo ikiwa uko tayari kujifunza kutokana na makosa na kufahamu njia za kuyaepuka huko mbeleni. Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wanavyojifunza na kukua zaidi na zaidi.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa usemi wa kosa siyo kosa bali kurudia kosa ndilo kosa,hivyo unapokuwa kwenye biashara au kazi yoyote ni lazima ufahamu makosa ambayo yanaweza kuathiri biashara au uwekezaji wako ,mfano makosa kama ,kujifanya unajua kila kitu,kutaka wateja wakufuate,matumizi yasiyo mazuri ya fedha,kupuuza baadhi ya mambo.Hii inakusaidia kuongeza umakini katika mambo yako mwisho wa siku inakusaidia kulitimiza lengo lako.

Mtu ambaye ni dynamic (anayeenda na mabadiliko),Mjasiriamali bora ni yule asiye static kwa maana ya kubakia tu na kitu alichonacho miaka nenda miaka rudi bali ni yule ambaye anaenda na mabadiliko.Kwa sababu kuna mabadiliko makubwa kiuchumi,kiteknolojia ,kisiasa ,kimazingira pia na kimahitaji.
Ili kuenenda vizuri ni vema kuongeza juhudi ya kuangalia nini kinahitajika ,na nini kiboreshwe zaidi ili uhutaji wake uendele.Hasa hasa katika utoaji bidhaa mbalimbali kwenda kwa watumiaji hivyo unavyokuwa unabadilika kuenenda na mabadiliko ndivyo unavyozidi kuwa sokoni tofauti na wale wasio na mabadiliko katika utoaji wa huduma.

Ndugu yangu mpendwa ni imani yangu kuwa sifa za ujasriamali bora umezielewa zaidi na utazifanyia kazi.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert.
Karibu.

No comments:

Post a Comment