MORNING MOTIVATION DIARY
Zijue faida za kuwa mjasriamali,
Ndugu,
Karibu katika program nzuri ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa ,kuing'alisha siku yako na kuonekana mpya.Faida za kuwa mjasriamali:
Uhuru wa kifedha,
Ujasiriamali unatajwa moja ya shughuli kubwa ambayo endapo ikitumika vizuri na kwa malengo itakupa uhuru mkubwa wa kifedha.moja kati ya wajasiriamali niliobahatika kusoma makala zao ni Coach Bassanga yeye anasema aliamua kuwa mjasiriamali ili akidhi aweze kupata Uhuru kifedha.Anasema hakuna kitu ambacho kilikuwa kinamuudhi kama ikitokea shida ya pesa halafu huwezi ihimili.Kama ni mfanyakazi mpaka kusubiri mshahara utoke na kama siyo mfanyakazi unaangaika kuipata hiyo pesa .Kwa upande wa mishahara Mara nyingi inapotoka watu wengi huwa wanalipa madeni waliyokopa hivyo ikija kufika tena mwisho wa mwezi tayali Pesa inakuwa imeisha.
Kwa mjasiriamali ambaye ana kitu kingine cha ziada cha kumuingizia kipato inamsaidia kukidhi mahitaji mengine sio kutegemea mshahara.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,tafiti nyingi zinaonesha mshahara hautoshelezi mahitaji ya watu ,hivyo kama unahitaji kupata Uhuru wa kifedha unaweza anzisha kitu cha ziada cha kukuingizia Pesa ili usiwe unategemea mshahara tu.Coach Bassanga anasema "mjasiriamali wa Leo ni tajiri wa kesho".
Ujasiriamali utakupa nafasi ya kufanya kile unachokipenda.
Tafiti na takwimu nyingi zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu,wanafanya kazi ambazo hawazipendi ila wanafanya tu kwa sababu hawana namna nyingine ya kujiingizia kipato. Hivyo uamua kukomaa nazo hivyo hivyo ili kusogeza siku ,lakini kwa wafanyakazi wanaoamua kufanya pia ujasiriamali wanapata fursa ya kuwa na unafuu.Maana kwenye ujasriamali unafanya kilicho moyoni bila kushinikizwa na mtu wala kulazimishwa.
Kupitia ujasiriamali utaamua nini ukifanye na kwa wakati gani,wapi na lini kulingana na matakwa yako.
Hapa wewe mwenyewe unaamua biashara ipi ufanye ,kulingana na nafasi /muda ulionao inaweza kuwa ya nguo,chakula,vinywaji na vingineo.Ili uweze kujipatia kipato cha ziada na kuanza kukidhi baadhi ya mahitaji mengine ambayo kazi uliyokuwa unaifanya awali ilikuwa aijakidhi.
Uwezo wa kupanga ratiba yako binafsi.Sana sana hii ipo kwa watu ambao wameamua kuwa wajasiriamli moja kwa moja.
Pamoja na ukweli kwamba unatakiwa kufanya kazi kwa bidii sana na kuwa na usimamizi thabiti kama mjasiriamali, ukweli ni kwamba unakuwa na uhuru wa kupanga ratiba na muda wake kulingana na vipaumbele ulivyonavyo. Hii ni tofauti kabisa na mtu ambaye yeye huuza muda wake kwa mwajiri ili aweze kujipatia kipato.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa ,kila mtu anawaweza kufanya ujasriamali na kuwa miongoni mwa watu wenye mafanikio makubwa.Kitu ambacho bado kinatukwamisha ni maneno na mipango ,yaani tuna mipango mingi sana.Unaweza kuzungumza na mtu akawambia mipango mpaka ya 2025 lakini ukimuliza ambayo ametimiza kwa sasa utasikia ,unajua kuna mtu namsubilia kidogo,muda sio mrefu ntaanza inafika mpaka mwakani ajaanza.Kama mjasiriamali panga jambo na ulitende muda unao unaweza kuutumia vyovyote unavyoweza.
"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".
Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert
Karibu.

No comments:
Post a Comment