Monday, September 30, 2019

Jinsi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara au mradi

 MORNING MOTIVATION DIARY

Jinsi ya kupata mtaji

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika programu yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako kwa kukuongezea maarifa na kuifanya kuonekana mpya.

Kujiwekea akiba wewe mwenyewe (saving),Akiba ni sehemu ya mapato ya ambayo huwekwa kando kama akiba ya dharura na mahitaji yasiyotarajiwa,mara nyingi akiba hutegemea sana jinsi mtu alivyojithatiti katika kuwekeza.Ukiweka akiba kubwa utakuwa na faida kubwa ,ukiwekeza kidogo utakuwa na faida kidogo.
Hii ndiyo sehemu ya kwanza na muhimu sana ambayo kila mmoja wetu anaweza kuanzia. Japo wengi hukosa nidhamu katika fedha na akiba zao, lakini unapaswa kujua hii ni sehemu nzuri ya kuanzia kupata mtaji wa kuanza au kukuza biashara yako.

Mara nyingi unashauriwa kukigawa kipato kabla hujakipata na mara unapokipata unakigawa kabla ujakitumia baada ya kukigawa kipato na kuweka akiba ndo unafanya matumizi mengine.
Njia hii ya kujiwekea akiba  umuwezesha mtu kuanza biashara akiwa na mani na bila ya usumbufu wowote wa kwamba ataanzia wapi .Hivyo mi nakushauri anza leo kujifunza kuweka akiba, ni ngumu sana kufika juu bila kuweka akiba.Angalia ni kiasi gani unapata kisha tenga faida au tumia ,kanuni ya asilimia 10 tu ya kipato chako na huo ni mtaji wako wewe mwenyewe.Mfano unapokea 100000/= kwa mwezi tenga 10000/= kama umepata 50000/= tenga 5000/= Mara nyingi mwanzo wa kujiwekea kipato huwa ni mgumu hivyo unajitahidi kufanya hivyo angalau miezi mitatu ya mwanzo ili uweze kuzoea.

Kama bado hujaanza ni muda wa kuanza ,kama tayali ushaanza jitahidi uyashinde majaribu maana saving inazo changamoto zake.

Kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki,
Ukiacha njia ya kwanza ya kuweka akiba(saving),njia nyingine inayoweza kukusaidia kupata mtaji ni kutoka kwa ndugu na marafiki.
Zama hizi watu wapo tayali kutoa pesa nyingi kwenye harusi ila ukiwaambia kuhusu biashara mtakimbizana,na watakukwepa utasikia yaani kama ungenambia jana au leo asubuhi  maana kuna mtu nimemwazima kiasi fulani.Mwingine atasema njoo ijumaa,jumamosi lengo ni kutaka kukukwepa lakini nakushauri usisite kumfatria atakupa tu ila wengi wamekuwa hawathubutu kuwabana vizuri.
Unaweza kuwatumia ndugu, jamaa na marafiki kupata mchango wa kuanza au kukuza biashara yako. Jambo lingine la msingi ni kuandaa vizuri wazo la biashara yako, na kuonesha ni kiasi gani cha fedha unahitaji ,ahadi zote utakazopewa jitahidi uzifatrie amini usiamini watu wengi wametajirika kupitia ndugu, jamaa na marafiki, mfano mtu tajiri kuliko wote barani Afrika kutoka Nigeria Dangote yeye wakati anaanza ujasiriamali aliomba msaada kwa ndugu, na kwa sasa tunaona maendeleo yake amekuwa bilionea ambaye amewekeza sana barani Afrika kwa vitu mbalimbali anavyouza kama  unga , mchele, mafuta, sukari,cement.Wakati anaomba hakuona haya kama wengi wetu tulivyo.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa Unapoomba usitegemee msaada wa fedha tu bali wapo watakaokupa msaada wa mawazo ushauri.Kuwa makini sana 'ongea na wote wasikilze wachache'  wengine watakupa msaada wa kifedha na uo utakuwa ni mwanzo wa wewe kusimama imara katika mradi/biashara.

Unaweza tumia mwekezaji wa biashara,
Mwekezaji ni mtu ambaye ana fedha ambazo anaweza kuziweka kwenye biashara mbalimbali na zikazalisha. Huwa hatoi fedha kama mkopo, bali naye huwa anakuwa sehemu ya umiliki wa biashara.
Kigezo kikubwa kinachohitajika ni kuwa na mpangilio mzuri unaoonesha mchanganuo wa biashara inahusu nini, wateja ni kina nani, wanapatikanaje na mipango ya ukuaji wake,jinsi utakavyokuwa ujalipa kodi.  katika hali hiyo unaweza kumshawishi mwekezaji kuwekeza kwenye biashara au mradi wako.

Anapowekeza kwenye biashara yako maana yake unampa hisa, hivyo unapopata faida na yeye anapata faida kulingana na mtaji alioweka katika biashara au mradu wako.Ikitokea hasara imepatikana na yeye hasara anapata hasara pia.
Kwenye hili unahitaji kuwa makini kwa mwekezaji unayemchagua inabidi awe  wa kuaminika na awe tayari kusubiri biashara hiyo ifanye vizuri. Pia wewe binafsi unahitaji kujituma sana kuhakikisha biashara inafanya vizuri ili usije kumwangusha yule anayekusaidia.

Kwanini ninasema unahitaji kuwa makini ni kwa sababu
biashara isipotengeneza faida kwa muda mliokubaliana inaweza sababisha kushitakiana na hatimaye biashara na mali zako kufilisiwa,ili kukwepa hiyo inabidi uwe unampatia taarifa ili ajue kinachoendelea.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.



No comments:

Post a Comment