Wednesday, December 04, 2019

Uchambuzi wa kitabu cha Ishinde tabia ya kughairisha mambo chake Joel Nanauka


MORNING MOTIVATION DIARY 
PRESENT: UCHAMBUZI WA KITABU
JINA: OVER COMING PROCRASTINATION,  ISHINDE TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO
MWANDISHI : JOEL NANAUKA.
UTANGULIZI:

Moja ya sababu kubwa ambayo inawafanya wengi kushindwa kutimiza malengo yao kwa wakati ni kughairisha mambo.Wengi wetu tunaseam ngoja niache kidogo ntamalizia baadae lakini baadae inapofika tunajikuta tayali tuna mambo mengine ya kufanya ilo tunalisahau.
Mwandishi Nanauka anaanza kwa kuuliza “Unakumbuka wakati watu wametangaziwa kujisajili kwaajili ya kupiga kura? Unakumbuka watu walivyotangaziwa kuhusu usajili wa vitambulisho vya utaifa? Ni siku gani watu walijaa zaidi? Bila shaka, utakumbuka ni siku ya mwisho hata kama waliliona tangazo. Kuna watu kila siku wanatuma maombi ya kazi siku ya mwisho hata kama waliliona tangazo hilo miezi miwili kabla. Kuna watu kila wakati watatuma ripoti yao siku ya mwisho, kuna watu kila wakati kazi waliyopewa kufanya wataiwasilisha dakika za mwisho”.Bila kujua madhara mkubwa yanayotokea baadae ,wengi wao hujikuta katika hali ya kuwa na stress(msongo wa mawazo) maana ata kazi wanapozifanya zinakuwa hazina ubora mzuri na hufanywa kwa kiwango cha chini kabisa na hali hii utokana na tabia ya kughairisha.Anasema alimia 95 ya wazee walipoojiwa walisema tunajuta kwa kughairisha mambo mengi katika maisha yetu ambayo tungeyafanya basi tungekuwa mbali zaidi.Huo ndio ukweli watu wengi wameghairisha mambo mengi tena ya msingi na kujikuta hawawezi kuyafanya tena.

Ndugu karibu tuzichambue sura moja baada ya nyingine ni  matumaini kuwa  utafurahia pamoja na kuchukua hatua baada ya kufika mwisho wa uchambuzi wa  kitabu hiki.

SURA YA KWANZA
Kwa nini watu wanaghairisha mambo?,utafiti wa kisayansi kuhusu kughairisha mambo.

Utafiti uliofanywa na William James ambaye ni mtaalamu wa saikolojia uliochapishwa katika jarida la sayansi ya saikolojia mwaka  1997 akishirikiana na Dianne Tice ambao uliwahusisha wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Western Reserve uligundua kwamba wanafunzi waliokuwa wanaghairisha walikuwa na msongo wa mawazo kuliko wanafunzi wasioghairisha hali hii ilikuwa inatokea hasa hasa katika ukusanyaji wa kazi(assignment) kwa mwalimu husika.Wakati wanafanya hivyo wanakuwa hawaoni Kama ni tatizo lakini baadae linakuja kuwa tatizo ,na mwishowe walijikuta hata kazi zao hazina ubora ukilinganisha na wanafunzi amabo walikuwa hawaghairishi mambo.

Mwandishi amebainisha taswira halisi katika maeneo ya kazi. Anasema wapo wafanyakazi ambao hawapendi kutekeleza kazi zao kwa wakati badala yake wanasubiri hadi dakika za mwisho ndipo waanze kuhaha huko na huko. Kimsingi tabia hizi zinazozungumzwa zinawagusa watu wa kila kaliba. Haijalishi umri wala nasaba au jinsia, Unaweza ukachukua daftari lako kuandika, ama ripoti yako ama hata kusoma kitabu, ukaamua kuwa unafanya unachotaka kwa nusu saa bila kuyumbishwa na kitu chochote, ghafla baada ya dakika 10 unajikuta nunashika simu na unasema ngoja niangalie meseji, kuja kushtuka unajikuta umeshatumia takribani nusu saa kuperuzi mitandao na hamu ya kuendelea na kazi uliyokuwa unaifanya inapotea kabisa. Ama wakati mwingine unasema ngoja niangalie TV kidogo kisha nitalala ama nitasoma kidogo, kuja kugundua unakuwa imeshafika saa 7 usiku na umeshindwa kuondoka kwenye TV yako.

Katika muktadha huo mwandishi anakumbusha kuwa wapo watu wanaoishi kwa kuahirisha. Wengine ambao hadi wakumbushwe ndipo hutekeleza jambo fulani. Wapo watu ambao hawezi kujikita kwenye eneo husika. 

Mwandishi anatumia utafiti wa Profesa Joseph Ferrari ambaye aligundua kuwa takribani asilimia 20 ya watu duniani ni waahirishaji wakubwa wa mambo yao,ambapo ufafanuzi wake umejikita katika mifumo miwili iliyopo kwenye ubongo kwa jinsi inavyoshindana.
Kuna mfumo unaitwa Limbic system huu una sehemu ambayo ndiyo unahusika na wewe kujisikia raha unapofanya jambo Fulani,mfano unapokula chakula kizuri,unapofanya tendo la ndoa na mengineyo.

Mfumo wa Prefrontal Cortex huu ni mfumo upo nyuma ya kipaji chako cha uso kazi yake kubwa ni kukuongoza katika kufanuya maamuzi mbali mbali.Huu ndio mfumo unaokusaidia kujua kipi kizuri na kipi kibaya kupitia tathimini hiyo unaweza kufanya tathimini ya kila kitendo amabacho unakifanya na kupima madhara yake.Hiyo ndiyo vita inayoendelea katika ubongo wako katika mambo mbalimbali unayotaka kufanya.
Unaporuhusu mfumo wa limbic kuwa na nguvu kuliko prefrontal cortex ambao ndio una uwezo wa kufanya maamuzi basi utajikuta unakosa hamasa na kuwa mgairishaji mzuri ambapo madhara yake ni kukosa nidhamu ya muda, kuhisi una mambo mengi yasiyokwisha sababu ya kutotekeleza kwa wakati na kulimbikiza majukumu ,utakosa hamasa ya kufanya jambo pia  utakosa  kuweka vipaumbele.
karibu ujipatie sura ya pili na kuendelea .....

Mchambuzi LACKIUS ROBERT karibu kwa mawasiliano zaidi 0767702659 email maarifarobert@gmail.com Kila kitabu kimoja kilichochochambuliwa ni shilingi 1000/= uchambuzi upo katika  mfumo wa PDF kupitia email ,Whatsup na telegram

No comments:

Post a Comment