MORNING MOTIVATION DIARY
Zijue sifa za mjasiriamali bora,
Ndugu,
Ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:
Mtu anayejitahidi kutafuta taarifa,Kama unavyojua sasa hivi tuko kwenye kipindi ambacho teknolojia inakua kwa kasi ,na mambo yanabadilika kila uchao ili kuendanana na kasi hiyo ni muhimu kusaka taarifa zaidi.
Mjasiriamali bora anatafuta taarifa kutoka sehemu mbalimbali kwa watu tofautitofauti kama vile wateja, washindani,kusoma vitu mbali mbali ikiwemo vitabu husika.
Pia hufanya utafiti binafsi wa namna mbalimbali za kuvutia wateja na kuboresha huduma bora ili kuongeza wigo wa wateja na kipato kwa ujumla.
Mjasiriamali Pia uomba ushauri kutoka kwa wataalamu na wadau mbalimbali wa masoko kulingana na biashara anayofanya lengo kubwa ni kuongeza uelewa zaidi.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa, taarifa sahihi zinaleta maarifa sahihi ukiwa na chanzo chenye taarifa sahihi unakuwa na uwezo mkubwa wa kufanikiwa kwenye unachofanya.Je ni taarifa gani unapokea au unaingiza ? Chanzo chako cha taarifa ni kipi? Ukipatia majibu hakika hautabakia hapo ulipo.
Mtu mwenye nidhamu,
Mtaalamu wa mafanikio na mjasiriamali mkubwa Jim Rhon aliwahi kusema "nidhamu binafsi ndiyo daraja la malengo( goals)na unapokwenda")(destination)
Nidhamu ni sifa muhimu sana kwa mjasiriamali kwani itamtenga na mambo mengi yasiyokuwa na umuhimu. Ni lazima mjasiriamali awe na nidhamu ya maswala kama vile matumizi ya muda pamoja na pesa.
Mjasiriamali bora ni yule anayeweza kujinyima na kukataa vitu vyote ambavyo havimwezeshi kufikia malengo yake.
Ndugu yangu mpendwa sijamanisha kujinyima kila kitu ,nachomanisha vitu ambavyo havikufikishi kwenye malengo yakob.Simamia nidhamu yako kwa kutumia muda vizuri,Maana muda uliopoteza hauwezi kujirudia.
Upande wa Pesa unahitaji nidhamu ya hali ya juu sana maana walio wengi hapo pana wasumbua,heshimu sana kilicho kwenye ratiba au kipaombele hakika utakuwa mjasiriamali bora zaidi.Nidhamu yako bora mafanikio yako.
Mtu mwenye uvumilivu,
Kuna ukweli usiopingika kwamba kila jambo lina changamoto zake katika kulitenda. Ujasiriamali una changamoto nyingi ambazo zinahitaji uvumilivu ili kuzimudu na kuyafikia malengo uliyopanga.
Naomba niishie hapo tukutane wakati ingine.
Kwa mawasiliano 0767702659 Lackius Robert. Karibu.

No comments:
Post a Comment