Monday, September 16, 2019

Sifa za mjasiriamali bora

MORNING MOTIVATION DIARY

Ujasiriamali na mafanikio

Ndugu
Karibu katika siku nyingine tulivu kwenye morning motivation diary yenye lengo kubwa la kuing'alisha siku yako na kuifanya kuonekana mpya.

Ujasiriamali ni uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazojitokeza na kugeuza au kutumia changamoto hizo kama fursa.
Mjasiriamali anabuni bidhaa mpya au njia mpya ya uzalishaji wa bidhaa ambayo soka linahitaji bidhaa hiyo au huduma hiyo ambayo haijapata kusambazwa hapo kabla.
Nikumbushe ndugu yangu mpendwa Ili kubobea katika ujasiriamali unatakiwa kuwa MJASIRI Pamoja na kutumia vizuri MALI ULIZONAZO.Kwa kufanya hivyo utakuwa umekamilisha neno zima la MJASIRIAMALI.
mfano katika mtaa au eneo fulani  kuna shida kubwa ya maji basi mjasiriamali atakabiliana changamoto hiyo kwa kuchimba kisima cha maji na hatimaye atakuwa ametatua changamoto hiyo ya maji na kugeuza kuwa fursa.Ambapo atakuwa anawauzia watu maji lakini wakati huo huo anapata kiasi fulani cha fedha.

Kwa hakika ujasiriamali ni chaguo muhimu sana kwenye karne hii ya sasa ili kujiongezea kipato zaidi na zaidi.
Wataalamu wanasema.
 “Siri ya mafanikio yeyote ni kutokukata tamaa katika kazi tunazofanya".Jaribu kuangalia wajasiriamali wadogo wadogo jinsi wanavyofanya kazi bila kujali mazingira yakoje wanavyofanikiwa.Kina mama wauza mbogamboga,migahawa ,watu wanaouza bidhaa za kutembeza wanapata Pesa.Unapochagua kuwa mjasiriamali haupaswi kuwa mtu wa kuyumbishwa na kuendeshwa na watu bali kile unachoona jamii inaweza kunufaika nacho.
Zijue sifa za mjasiriamali
Ili kuwa Mjasiriamali bora /au kujiboresha mwenyewe katika ujasiriamali wako ,sifa zifuatazo ni muhimu kuzifatria na kuzijua kwa undani:

1.Uwezo mkubwa wa kuona fursa na kuifanya kazi,
Mjasiriamali mzuri ni vizuri uwe na jicho la kuona fursa au kuona kitu gani kinahitajika  katika jamii inayokuzunguka.Ndio maana Muasisi wa fursa Lughe Mutahaba aliwahi kusema "Matatizo yetu ndio fursa zenyewe".
 Mjasiriamali ni vema kuziangalia changamoto zinazojitokeza katika jamii yako na kutumia changamoto hiyo kama fursa kwako. Kwa mfano sehemu unayokaa watu wanauhitaji wa huduma za kibenki kama vile (tigo pesa, m-pesa ,airtel money )ukifungua kibanda tayali tatizo umelitatua na umejitengenezea fursa,Mahitaji muhimu ya kutumia nyumbani katika mapishi.Bidhaa za urembo ,dukani kama mafuta vyakula n.k.

2.Unahitaji kuwa mbunifu,UBUNIFU  naweza sema ni  matumizi ya njia bora zaidi zinazokidhi kutatua changamoto mpya, changamoto ambazo tayari zipo lakini hazijapatiwa ufumbuzi bado, au changamoto zilizopo kwenye soko au jamii kwa kipindi husika.Dhana hii hutimilika pale ambapo bidhaa, huduma, teknolojia, mpangilio  wa biashara au njia nyingine yoyote inayoweza kutatua changamoto husika.Unaweza kubuni kitu kipya au kuboresha kilichopo,
Kama mjasiriamali yakupasa uwe mbunifu ,hata kwa bidhaa au huduma ambayo wanaokuzunguka wanayo ,unajaribu kutengeneza utofauti fulani .Kitu kinachomfanya mtu kuja kuchukua bidhaa kwako na sio kwa mwingine kama ni una kibanda cha chips mfano ,mandazi ,chapati au mgahawa,genge, n.k .

Hali hiyo inamfanya mteja kurudi ,Sam Walton ambaye ni mwanzilishi wa  WalMart anasema "Hakuna bosi kama mteja" kwa sababu ndiye anayetulipa hivyo ni jukumu lako kubuni namna ya kumshawishi katika bidhaa au huduma yoyote unayotoa. Nikukumbushe ndugu yangu '''Ubunifu wako ndio mafanikio yako'''.

3.Mtu anayependa kuongeza jitihada katika kutenda (practice),
Mara nyingi ujasiriamali mzuri ni ule wa vitendo,pamoja na kubadilisha mawazo (ideas) kuwa vitendo halisi. Hivyo mjasiriamali ni mtu anaechukua hatua na kutenda bila kujali vikwazo pia hachoki wala kukata tamaa.
Anaposhindwa hili hufanya lile au hubadilisha mbinu ili kufikia malengo aliyokusudia.
Ukijaribu kuangalia watu wengi wanayo mawazo mengi mazuri lakini inapofika wakati wa utendaji kama ni kuanzisha duka ,genge ,mgahawa ndipo utata unapoanzia sababu zinakuwa nyingi.Mara oh kuna mchakato Fulani nausikilizia ,Mipango haijakaa sawa au anasubilia ukamilifu wa kitu Fulani ndo aanze.Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa kesho imewaponza wengi,Anza leo ,majasiriamali bora ni yule anayekubali kuingia katika utendaji sio maneno na sababu nyingi ,Jiulize kama kesho sijui inavyofanana kwa nini nisianze?.

4.Mtu mwenye anayeweka malengo ,Kuna usemi unaosema "" kama hujui unapokwenda basi popote wewe unakuwa umefika""
Ili kujiboresha zaidi mjasriamali bora huweka malengo ya nini anataka afanye kwa muda fulani .
Ninaamini na wewe ndugu yangu mpendwa ambaye ni mjasiriamali kuna malengo umeyaweka.Faida kubwa ya kuweka malengo ni kwamba inakusaidia kukupa mwongozo(guideline) na kufanya uachane na vitu amabavyo sio vya msingi au vilivyopo nje ya malengo.

Malengo anayoweka huwa  ni ya muda mfupi (short term goals ) na  ya muda mrefu (long term goals) baada ya kuyaweka huwa anajituma zaidi ili kuyakamilisha malengo hayo.
Malengo hayo lazima yawe makubwa yanayoweza kufikika yasiwe madogo yanayoweza kukufanya kuwa MZEMBE wala yasiwe makubwa sana yasiyofikika. Kama wengi tunavyojua mafanikio ni mchakato.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Naomba niishie hapo tukutane wakati mwingine.
Lackius Robert unaweza kuwasiliana na Mimi kupitia 0767702659.



No comments:

Post a Comment