MORNING MOTIVATION
DIARY
PRESENT: UCHAMBUZI WA
KITABU
JINA: EAT THAT FROG,
21 GREAT WAYS TO STOP PROCRASTINATING AND GET MORE DONE IN LESS TIME. KULA HUYO CHURA ,NJIA
21 ZA KUEPUKA UGHAIRISHAJI NA KUFANYA MENGI KWA MUDA MFUPI.
MWANDISHI: BRIAN TRACY.
UTANGULIZI:
Brian Trace ni mwalimu mwenye uzoefu sana katika eneo la
mafanikio. Baadhi ya mambo mengi ambayo Brian anatushirikisha ni yale ambayo
amekuwa akijifunza, kisha anayafanyia kazi yeye binafsi na ndipo
anatushirikisha kupitia vitabu vyake. Katika kitabu hiki ametushirikisha namna
ya kupambana na hali ya kuahirisha mambo uliyopanga kuyafanya.
Ukweli kuhusu Chura
Mark Twain aliwahi kusema jambo kubwa unalopaswa kufanya kila
asubuhi ni kula chura moja kwa moja."Chura"
wako ndiye kazi yako kubwa na muhimu zaidi, ndio iliyo na uwezekano wa
kuchelewesha ikiwa hautafanya jambo fulani juu yake. Pia ni kazi moja
ambayo inaweza kuwa na athari nzuri zaidi maisha yako yote.
Sheria ya kwanza ya
kula chura ni,
"Kama utatakiwa kula vyura wawili, kula mbaya kwanza aliyebaki mmalizie
baadae " ,Hii ni njia nyingine ya kusema kwamba, ikiwa una kazi mbili
muhimu mbele yako, anza na kazi kubwa, ngumu na muhimu zaidi kwanza. Jiridhishe
mwenyewe kuanza mara moja na kisha kuendelea mpaka kazi imekamilika kabla ya
kuendelea na kitu kingine.Fikiria hii kama "jaribio.", Kataa jaribu
la kuanza na kazi rahisi .
Sheria ya pili ya kula
chura ni,
"Ikiwa itabidi kula chura moja kwa moja, hailipi kukaa na kuiangalia kwa
muda mrefu sana. " Ufunguo wa kufikia viwango vya juu vya utendaji na tija
ni kwako kukuza tabia ya maisha yako yote ya kushughulikia kazi yako kuu kwanza
kitu kila asubuhi. Lazima uendeleze utaratibu wa "Kula yako chura
"kabla ya kufanya kitu kingine chochote, na bila kuchukua muda mwingi kufikiria
juu yake.
Ndugu karibu tuzichambue sura moja
baada ya nyingine ni matumaini kuwa
utafurahia pamoja na kuchukua hatua baada ya kufika mwisho wa uchambuzi
wa kitabu hiki.
SURA YA KWANZA,
Panga ratiba
Napoleon Hill aliwahi kusema"Kuna sifa moja ambayo mtu
anayependa kushinda anapaswa kuwa nayo ,
nayo ni kuweka kusudi na ujuzi wa kile
kitu ambacho ana hamu ya kukifanikisha. ”
Kabla ya kuamua kumla "chura" wako ili uendelee na
kazi, lazima uamue unataka kufikia wapi kwenye maisha yako.
Watu wengi wanashindwa kuyafikia malengo yao kwa sababu wanakosa
motisha ya kufanya kazi ,kwa sababu hawana mwongozo ulio imara katika kuyafikia
malengo waliyoweka.Utafiti unaonesha kuwa asilimia 3 ya walioweka malengo ndio
waliofanikisha na wengine asilimia 97 walishindwa kuyafanikisha. Kuna hatua
saba kama unahitaji kufikia malengo yako inabidi uzifahamu na kuzizingatia :
Hatua ya 1.Amua unataka uwe nani ,kaa chini tafakari chagua
eneo ambalo unaona linakufaa lifanyie kazi.Steven Covey aliwahi kusema’’ kabla hujaamza kupanda ngazi ya mafanikio
hakikisha ,ngazi imenininginia katika sehemu sahihi ya jengo’’
Hatua ya 2.Andika shehemu,Chukua kipande cha karatasi andika
malengo yako ,wakati unaandika hakikisha unaandika malengounayoweza kutimizika
,yanayoonekana na kueleweka maana kuwa na malengo yasiyoandikiwa kunakupoteza.
Hatua ya 3.weka ukomo wa malengo yako,Maamuzi au malengo
yasiyo na ukomo yanakuwa hayana uharaka ,hivyo unapopanga malengo hakikisha
yanakuwa na ukomo ili kuepusha kughairisha mara kwa mara.
Hatua ya 4.Andika vitu vyote ambavyo unahisi ukiwa navyo
vinaweza kukusaidia kuyafikia malengo yako.
Hatua ya 5. Pangilia vizuri mahitaji yako,weka vipaumbele/
pangilia vitu vya msingi sana unavyohitji ikifatiwa na vitu vingine amabvyo sio
vya msingi sana.
Hatua ya 6. Chukua hatua,Fanya chochote, Mpango wa wastani
uliotekelezwa kwa nguvu ni bora zaidi kuliko mpango wa kipaji ambao hakuna kitu
kinafanyika .
Hatua ya 7.Amua
kufanya jambo moja kila siku lililo kwenye lengo lako,jitahidi kuzidi
kujifunza zaidi na zaidi.
KUNA NGUVU KUBWA YA
KUANDIKA MALENGO
Malengo ya maandishi yaliyo wazi yana athari nzuri kwa mawazo
yako maana yanakuhamasisha na kukuchochea kuchukua hatua. Malengo ni mafuta katika tanuru ya mafanikio. Fikiria juu ya
malengo yako na kuyapitia kila siku,Kila asubuhi baada ya kuamka, chukua hatua
juu ya kazi muhimu zaidi unayoweza kukamilisha kufikia lengo lako muhimu zaidi
kwa sasa.
SWALI:Je ni malengo yapi uliyojiwekea ili
kufikia ndoto yako?.
Uchambuzi umefanywa na Lackius Robert kwa mawasiliano zaii 0767702659au maarifarobert@gmail.com
karibu utatumiwa kwa njia ya PDF kupia whatsup,email,au tegegram.
No comments:
Post a Comment