Saturday, September 21, 2019

Zijue kanuni bora za ujasriamali

MORNING MOTIVATION DIARY

Zijue kanuni za ujasriamali

Ndugu,
Leo ni siku nyingine tena tunakutana katika program yetu pendwa ya morning motivation diary yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa na kuing'alisha siku yako na kuiona mpya.

Ujasiriamali una kanuni zake ambazo ni muhimu sana kuzijua na kuzifuata ili kuyafikia mafanikio ya kweli. Ili ufanikiwe katika Ujasiriamali kama ilivyo katika shughuli nyingine yoyote, zipo kanuni na misingi ziliyowekwa ili uzizingatie na kuzifanyia kazi .Mara  nyingi kanuni hizi ni kama mwongozo unaotuongoza katika kufanikisha jambo, kanuni hizi hapa:

Kujituma na kupenda  kazi unayoifanya,
Ni kweli kwamba kuna watu wanafanya kazi ambazo hawazipendi ila wanafanya tu ilimradi tu mtu apate kipato.Kama mjasiriamali ili ufanikiwe katika biashara yoyote, lazima uwe na moyo wa kujituma na uipende kazi unayoifanya. Usisubiri kusukumwa kwa sababu hakuna atakayefanya kazi hiyo. Jifunze kuwahi kuamka asubuhi ili uendane na kasi ya soko, jitume kufanya mambo yatakayoiboresha biashara yako bila kuchoka na fanya kazi kwa moyo wako wote.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa, hakuna kitu kinachompa mtu furaha kama kufanya anachopenda ,mtu wa aina hiyo awezi kuchoka,huwa yuko tayali kufanya kazi muda mwingi hata changamoto zinazojitokeza haziwezi kumnyumbisha.Hii ni kanuni bora kuizingatia kama mjasiriamali ili uweze kufika mbali kama unachofanya bado haujakipenda jitahidi ,ongeza juhudi Kaza """ dunia inakutegemea""".

Kuthubutu,
Mjasriamali bora ni yule mwenye uwezo na utayari wa kufanya maamuzi magumu ya kuingia kwenye biashara au mradi fulani huku akiwa ameondoa nidhamu ya woga na kuanza kupiga kazi.Ukweli ni kwamba kuna watu ambao  ni waoga wa kuchukua hatua ya kuanzisha biashara au  kuingia katika miradi fulani fulani sababu ya woga wa kushindwa mbeleni. Hasa hasa watu wengi huogopa kupata hasara na kuzomewa pindi waangukapo au wanapoyumba katika kuiendesha biashara au mradi walioanzisha.Kama  mjasiriamali bora ni lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya mambo makubwa ,ikiambatana na uelewa mkubwa zaidi baada ya kujiridhisha na kufanya biashara yako.Ili kuepuka kuanguka au kuyumba inabidi uwekeze katika kitu ambacho umefanya angalau utafiti ili ujue hekaheka zake kabla aujaanza kukifanya.
Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa hakuna mbadala wa mafanikio tofauti na kuthubutu na kuongeza juhudi katika kitu unachofanya.

Kuwa na usimamizi mzuri,
Kama mjasiriamali ambaye unahitaji kufika mbali kimafanikio kupitia biashara yako au mradi wowote unaoufanya ni vema zaidi
Kuwa na uwezo wa kuisimamia vizuri.
Hii inaambatana na kutoa maamuzi sahihi mara zote. Katika Ujasiriamali, uwezo wa kusimamia na kuwaongoza watu walio chini yako ni muhimu sana kwani hata kama ukianza na biashara ndogo, lazima baadaye itakuwa kubwa hivyo utalazimika kuajiri watu wengine wa kukusaidia ili kazi zako ziende.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa"

Kwa mawasiliano zaidi 0767702659 Lackius Robert karibu.

No comments:

Post a Comment