Wednesday, December 18, 2019

Uchambuzi wa kitabu cha How successful people think chake John Maxwell


MORNING MOTIVATION DIARY 
PRESENT: UCHAMBUZI WA KITABU
JINA: HOW SUCCESSFUL PEOPLE THINK: Change your thinking,change your life
JINSI WATU WALIOFANIKIWA HUFIKIRIA: Badilisha fikra zako, Badilisha maisha yako.
MWANDISHI : JOHN C.MAXWELL
UTANGULIZI

Wafikiriaji wazuri daima wanaangalia mahitaji,Wanatambua kazi zao za kila siku na kila wakati ni watu wanaojua kwanini wao ni mabosi.Mara zote hutatua shida zinazojitokeza katika sehemu wanazoziongoza iwe ni kwenye kampuni au la kamwe hawapungukiwi na maini jinsi kuendesha uongozi wao,wanakuwa na fikiri za mbali kuhusu kuwa na kesho ambayo ni bora.
Mwandishi John Maxwell anasema ,Nimejifunza zaidi ya miaka  arobaini na kugundua kuwa kinachowatofautisha waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni namna wanavyofikiri,waliofanikiwa mara zote wanajua umuhumu wa kujifunza zaidi na uzidi kujifunza ukilinganisha na watu wasio na mafanikio.

Kwanini unapaswa kubadili fikra zako?
Japokuwa kubadili fikra zako sio rahisi lakini ukiamua unazweza lakini unapswa ujue kwamba kubadili fikra hakuji automatiki lazima kuwe na kichocheo ,hivyo  kubadili fikra zako kunakusaidia kutatua matatizo mbalimbali na kukutengengenezea fursa.Pia unapelekea kuruhusu hisia zako kufanya kazi vizuri maana mfumo uwezo wetu wa kufanya jambo lolote unaanzia katika fikra zetu ndipo matendo yanafatia.Ufikiriaji mzuri unasaidia sana mtu kuyafikia malengo aliyoyaweka katika kazi zake ikiwemo wale anaowaongoza.
Ilii uweze kuboresha zaidi ufikiriaji wako
Tafuta sehemu tulivu ambayo haina mizunguko ya watu ukae utulie na uanze kutafakari kuhusu yale unayoyatamani kuyafanya baada ya kuyafikiria vizuri na kuyaweka katika mipangilio mizuri hatua kubwa inayofuata ni kuyaweka katika matendo.Jambo la kuzigatia ni kuwa unafanya hivyo mara nyingi ili kuweza kuuzoesha ubongo wako ufanye kazi zaidi na zaidi mafanikio yako yanaongozwa na fikra zako.

Ndugu karibu tuzichambue sura moja baada ya nyingine ni  matumaini kuwa  utafurahia pamoja na kuchukua hatua baada ya kufika mwisho wa uchambuzi wa  kitabu hiki.
SURA YA KWANZA

Tengeneza picha kubwa ya kufikiria
David SCHWARTZ aliwahi kusema "Pale ambapo mafanikio yanahusika, watu hawapimwi kwa nchi, pesa walizonazo au digrii za chuo kikuu, au asili ya familia zao bali hupimwa kwa ukubwa wa mawazo na yao. "
Unapokuwa umefikiri katika mapana ya picha kubwa ni njia ambayo itakupa ufanisi wa fikra zako. Sifa kubwa waliyonayo watu wanaofikiri kwa mapana ya picha kubwa ni kwamba daima huwa hawaridhiki na hali inayowakabili muda wote bali wanakuwa macho kwa ajili ya fursa mpya. Watu hawa wanajifunza kila mara kutoka kwa watu wengine na hivyo wanafanya kazi kwa bidii na ubunifu katika shughuli zao kila siku. Watu hawa wanatambua nguvu kubwa iliyopo kwenye usikivu kutoka kwa wengine kuliko kuwa wazungumzaji wakubwa. Pia, watu hawa muda wote wanatazama mbali malengo yao makubwa ni kutafuta fursa mpya ili wazifanyie kazi.
Kwa nini utengeneze picha kubwa ya kufikiria?
·         Kufikiria mapana yenye picha Kubwa inakusaidia kuongoza,Kama kiongozi unapokuwa na picha kubwa katika ufikiriaji wako unakuwa na maono makubwa kabla ya wengine kuyaona,unakuwa unawaza ya kesho kabla yao,unakuwa na mitazamo ya kule mnakoenda tofauti na wao waliyonayo.Ikiwa ni kujenga barabara, kupanga safari za kikazi katika uongozi, mawazo ya picha kubwa hukuruhusu kufurahia mafanikio zaidi. Watu ambao wanaangalia kila wakati picha nzima wana nafasi nzuri ya kufanikiwa kwa juhudi yoyote.
·         Kufikiria picha katika ukubwa Kunakupeleka kwenye mahali ulipolenga,Ili kufanya vitu vizuri, unahitaji kufikiria jambo katika upana wake ikiwemo kulielewa na kulifanyia kazi pasipo kusuburia.
·         Kufikiria jambo  kwa upana kunakusaidia kuona wengine wanapoona ,Moja kati ya ujuzi ambao mtu yeyote anahitaji kuwa nao ni uwezo wa kuona wengine wanapoona ,kwa kufanya hivyo hujikuta anawahudumia wateja wake vizuri tena kwa kuwaridhisha lakini hali hii inaambatana na ufikiriaji mzuri  unaoendana na kuwa unatafakari mambo katika ukubwa.
·         Kufikiri jambo kwa upana kunasaidia kuboresha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa pamoja na kuboresha mahusiano ikiwemo kusaidia na hii upendeza watu wanaofikiria mambo kwa upana zaidi wanapokutana.
Hivyo ili kuweza kuboresha uwezo wako wa kufikiri jambo kwa upana zaidi unatakiwa kujifunza kutoka katika kila uzoefu unaopitia au pale unapokuwa unafanya kazi na wengine mkabadirishana mawazo ya hapa na pale.Unapokuwa na wazo sahihi, unatakiwa uwashirikishe watu sahihi kwa ajili ya wazo husika, wazo pia lazima lishirikishwe katika mazingira sahihi, muda pia unatakiwa uwe sahihi.

SWALI : Je nafikiri zaidi yangu,ulimwengu wangu ili niweze kushughulikia maoni kwa mtazamo kamili?.Karibu upate sura ya pili mpaka mwisho wa kitabu hiki

Kupata uchambuzi zaidi wa kitabu hiki tuwasiliane kupitia 0767702659 Lackius Robert

No comments:

Post a Comment