Tuesday, November 10, 2020

UKIANGUKA MARA 7 INUKA YA 8,Hadithi ya muigizaji wa movie ya TITANIC 1998.

Ndugu Karibu katika mwendelezo wa masomo yetu yanayolenga kukuongea maarifa zaidi,leo tunaenda kuangalia hadithi ya muigizaji wa movie ya TITANIC.

Ukianguka Mara 7 mara ya 8 amka uendelee na safari.Huo ni msemo uliojitokeza kwa muigizaji maarufu duniani Leonard Di Caprio ambaye aliigiza movies maarufu kama vile  Titanic,Aviator,Blood Diamond. Kwa mara ya kwanza aliandika historia kama best male actor,  kabla ya hapo aliwahi kuchaguliwa kuingia kwenye kinyanganyilo cha best male actor  zaidi ya mara tano tangu 1994 lakini alikuja kufanikiwa kupata tuzo hiyo mwaka 2016 baada ya miaka 22 kupita.

Wakati wote alikuwa anasubira ya kuwa siku moja atakuja kuipata tuzo hiyo na ilipofika watazamaji walidhani kitu cha  kwaida lakini haikuwa hivyo kwake ilikuwa ni heshima kubwa.Alichoka kushiriki na wenzake katika kinyanganyilo hicho.Lakini siku ilifika akaweza kupata tuzo hiyo aliyoifukuzuia kwa miaka zaidi ya 22.

Nikukumbushe ndugu yangu mpendwa kama bahati imeandikwa utaipata tu haiwezi kupotea kitu cha muhimu na msingi ni kuipalilia njia ili bahati ikutane na maandalizi.Haijalishi muda gani utapita ila utaipata tu,Jifunze uelimike zaidi ili uchukue hatua dhidi maisha yako kukata tamaa ni mwiko songa mbele amini katika ushindi.Pia tuache hali ya kualalamika maana kualalamika hakuwezi kuwa masaada kwetu ata siku moja.

Tafakari ndugu yangu mapendwa na uweze kuchukua ahtua juu ya amisha yako.
Makala hii imeandaliwa na Lackius Robert tuwasiliane zaidi 0767702659 karibu mungu akubariki zaidi.

Monday, November 09, 2020

UMOJA NI NGUVU,Hadithi ya muuza maziwa.

Habari za asubuhi ndugu yangu mpendwa karibu katika makala zetu kila siku ambapo unakuwa unapata neno linalokupa hamasa zaidi,leo tunaenda kuangalia hadithi ya muuza maziwa. 

Bwana mmoja alipata nafasi ya kuwa anapeleka maziwa katika hoteli fulani hapa mjini.Bwana huyo alikuwa akiwaza sana lini atapata sehemu angalau ya kupeleka bidhaa yake kwa muda mrefu. Alipofanikiwa kuipata hotel ile alifurahi sana akaanza kuimba uku akishangilia kwa nyimbo na vifijo na ndelemo.Akajua utajiri upo njiani! muda sio mrefu nanunua garina mipango mingine mingi.

Aliweza kuelewana na wahusika na akaanza kutoa huduma hiyo ,ila jambo la  ajabu na la kushangaza ni kuwa ni aliweza kutoa huduma hiyo miezi miwili tu akawa ameishiwa hakuwa na maziwa tena.Alisahau kuwa "ujasiri hauwezi kukupa mafanikio ila unakupa nguvu ya kupambana na maisha".pia umoja ni nguvu utengano ni udhaifu alihitaji kufanya kazi hiyo peke yake na furaha ikageuka kuwa majuto.

Maziwa alikuwa anatoa kwa Ng'ombe zake mwenyewe zilipoacha kutoa ,tenda ikamshinda .Akapewa mtu mwingine mwenye uwezo na network nzuri ya wauza maziwa mengine kutika sehemu tofauti tofauti waliokuwa wanamletea maziwa.Akawa ana nguvu na support ya kutosha kupeleka maziwa hotelini tofauti na yule wa mwanzo.

Kuna wakati sisi tunalalamika kuwa hatupati fursa ,sisi ni watu wa bahati mbaya lakini ukweli ni kuwa tunazipoteza wenyewe.Mtu huyo alipoteza tenda hivi hivi sababu hakutaka kutengeneza network ya watu watakaomletea maziwa kwa bei nzuri tu ili aboreshe mahusiano na biashara yake.Tuitumie vizuri fursa tunayoipata.

Tunahitaji watu ili kuweza kusonga mbele zaidi ,natumaini lipo jambo umejifunza leo.Mimi ni Lackius Robert karibu tuendelee kujifunza zaidi tuwasiliane 0767702659 mungu akubariki.

Sunday, November 08, 2020

JINSI YA KUBRAND MAISHA YAKO 3.

karibu katika makala ya tatu na ya mwisho kutoka katika moja ya mafundisho ambayo aliwahi kutoa Jim Rhon enzi za uhai wake lipo jambo unaweza kujifunza, 

HATUA YA TATU 3. Usijaribu kwenda nje ya mfumo au kukimbizana na muda (DON’T TRY TO BEAT THE SYSTEM).

Ukweli ni kuwa mafanikio yanapitia mchakato mrefu kuona umeyafanikisha,watu wengi hukata tamaa pale wanapoona mambo hayaendi wamekutana na changamoto mbali mbali wanachoshindwa kujua ni kuwa kila kitu kina mfumo wake kinaenda kadili kilivopangwa.Wewe hupaswi kukimbizana na muda kama unaona umepata wazo na ukaanza kulifanyia kazi usikimbilie matokeo ya haraka tulia nenda taratibu hata kama itakuchukua muda upi kama uko katika njia sahihi matokeo utayona bila shida yoyote.

Unaweza kuwa uanjifunzaharaka lakini haimanishi kuwa ndo utegemee kupata matokeo haraka unahitaji muda na utulivu katika kuyapata matokeo.Niliwahi kuanguka mara 7 katika sehemu moja japo kwa vipindi tofauti watu wakawa wanasema kuwa si uache kile unachofanya maana hatuoni hatua unayopiga.Wengine hawawezi kuona hatua au maendeleo yako haaraka wewe ndiye unayekuwa unaona kwa sababu upo katika mfumo,unahitaji kuwa mtu wa kubadilika na kuenda na hali unayokutana nayo.

Kubali kupoteza pesa,nyumba gari na vinginevyo ila siyo AKILI YAKO maana akili yako ndipo kuna mipango yako yote unayotaka kufanya.Akili yako inaweza kukusaidia katika kutafuta mali zote zilizopotea,chunga sana itunze sana na iboreshe akili yako kila siku kwa kuilisha vitu endelevu na vyenye maana.

Tumia hatua hizi tatu kuyaboresha miasha yako kupitia kazi unazozifanya.

Makala hii imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659 karibu tujifunze zaidi.

Pia nakukaribisha upate uchambuzi wa vitabu kwa njia ya kiswahili ili uweze kujifunza zaidi na kuongeza maarifa tuwasiliane zaidi.

JINSI YA KUBRAND MAISHA YAKO 2.

 HATUA YA PILI 2. GO TO WORK (NENDA KAFANYE ).

Ukiangalia katika hatua ya kwanza tumeona kuwa unahitaji kujua namna vitu vinavyopaswa kufanyika kwa kutumia mawazo yako.Baada ya hapo hatua inayofuata ni kuwa unapaswa kuchukua hatua kwa kile ulichoanzisha,hatua hizi ndizo zinazokuwa zinakupa nguvu na kukuonesha kuwa wewe ni mtu mwenye uthubutu mkubwa katika utendaji wako wa kazi.

Watu wengine wanapokuwa wanakufundisha labda siku za mwisho wa wiki au siku zingine hakikisha unachukua pointi za msingi sana unaweza kuwa unafundishwa katika uchumi au uwekezaji kamwe “usiruhusu kufanya kazi peke yako” unahitaji pia kupata mawazo ya watu wengine ili kuweza kuyaunganisha na mawazo yako.

Kuna mtu alitaka kuniambia kitu nikamwambiaje kabla ujaniambia nioneshe (don’t tell me, show me) usiniambie nioneshe akimaanisha matendo yanaongea kuliko maneno.Fanya zaidi juu ya kitu unachotaka kufanya.Kadili unavyokuwa unachukua hatua mara kwa mara ndivyo unavyokuwa unapata uzoefu na kuondoa hofu ya kuanza anasema massive action ‘the cure all’kuchukua hatua kunanitbu yote.

Tumia kanuni hii katika kila wazo zuri chukua hatua take good idea –take action , Hakikisha unakuwa na mawazo mengi uwezavyo ili uweze kuwa na nafasi ya kuchambua ya msingi.Usipofanyia kazi kile unachojifunza utakuwa mjinga unakpaswa kujitahidi kuwa mtu wa kuchukua hatua mara zote upatapo wazo zuri.

Tumia maarifa unayojifunza kama njia ya kukupeleka katika utajiri.Utajiri ninaouzungumzia siyo utajiri wa pesa maana pesa ni sehemu tu inayotokana na zao la thamani.Nawajua watu wengi wenye pesa lakini ni maskini.Pesa hazikupangii kitu cha kufanya wewe ndiye unayepaswa kuzipangia kama una mipango mingi pesa yako itazidi kukuua na kuzaa zaidi ila kama huna mipango pesa yako haitaweza kuzaa badala yake itapotea bila kujua.

Usikose sehemu inafuata na ya mwisho.

Mimi ni Lackus Robert 0767702659 karibu sana na mungu kaubariki zaidi.

JINSI YA KUBRAND MAISHA YAKO 1.

Habari za asubuhi ndugu yangu mpendwa karibu katika mwendelezo wa makala zetu kila siku ,leo tunaenda kuangalia namna unavyoweza kubrand maisha yako na kuwa mapya hizi zilitolewa na Jim Rohn katika mfululuzo wa mafundisho yake. 

HATUA YA KWANZA 1.FIND HOW THINGS WORK(TAFUTA KUJUA NAMA VITU VINAVYOFANYIKA).

Katika mchakato wa kujua namna gani vitu hufanyika unahitaji kuwa na( IDEA )wazo.Mawazo ya jinsi gani unaweza kutengeneza pesa,namna gani unaweza kufanya kazi zako kwa ubora na vitu vingine vya msingi.Katika hilo ni kwamba mawazo yoyote unayoyapata kuhusu kitu chochote kizuri unahitaji kuyaandika mahali au katika kijitabu chako kidogo ili ukiyahitaji iwe ni rahisi kuyapata anasema “Usitumie kichwa chako kutafuta mafaili yaliyojaa mawazo yako” anachomaanisha ni kuwa unaweza kusahau muda wowote hivyo weka mawazo yako katika maandishi,Ukiyahitaji utayapata haraka na bila kuangaika kwa kukuna kichwa chako uku ukifikiria mawazo uliyoyawaza.

Kwa kutumia mawazo tafuta namna mambo yanavyofanya kazi,

*      Kama unahitaji kufanikiwa soma mafanikio ya wengine kupitia usomaji huo unakuwa unapata mawazo mapya na mengi ambayo yanakusaidia kukuza uelewa wako.

*      Kama unataka kufurahia soma mawazo yanayofurahisha.

*      Kama unataka kuwa na afya njema soma makala zinazofundisha afya njema.

Usimalize siku bila kusoma chochote, unapaswa kusoma vitu vitakavyoweza kubalisha uchumi wako,jamii yako,imani yako na maisha yako kiujumla.Inawezekana usifanikishe kupata kila kitu unachokitaka ila ukapata vichache ,kupitia hivyo vichache hakikisha unatafuta na kujua namna kitu kinachofanyika.

Wengi wetu tunapata changamoto ya ukosefu wa habari za muhimu ,hakikisha unapata habari za muhimu na nzuri zitakazo kusaidia kujenga uelewa wako kila siku.

 Kuwa kama mtoto pale unapotaka kujua kitu.

Kuwa na furaha kama watoto hata wakati mgumu,mfano angalia watoto walivyo unaweza kumpiga baada ya dakika chache anakuwa amesahau kuwa umempiga anaruhusu maisha mengine yaweze kuendelea.

Usikose kufatria hatua ya pili katika makala inayofuata.

mimi ni Lackius Robert karibu sana tuendelee kujifunza zaidi 0767702659 au maarifarobert.com.

Mungu akubariki zaidi.

IPO NJIA MOJA YA KUPATA,Usikazanie zingine:

Habari za saa hizi ndugu yangu mpendwa karibu katika mwendelezo wa makala zetu kila siku zenye lengo la kukuongezea maarifa kila siku.Siku ya leo nimekuandalia vitu kadhaa kutoka kwenye kitabu cha 101 Crucial Lesson they dont teach you in your Business School Ways  chake Chris Haroun naamini lipo jambo utaweza kujifunza na kuchukua hatua.

Karibu sana,

=•Ipo njia moja ya kupata chochote unachotaka na njia hiyo ni kuomba. Ombeni na mtapewa ni siri muhimu ya mafanikio kwenye biashara. Kama kuna kitu unataka, omba na wengine watakuwa tayari kukupa, Huwezi kupata kitu bila kuomba bila kuomba utapata lakini utachelewa.

=•Biashara ni watu, haijalishi unajua nini, bali unamjua nani na nani anakujua wewe. Hivyo kazana kukuza zaidi mtandao wako wa watu unaowajua na wanaokujua.

=•Mchukulie kila mtu unayekutana naye kama mtu mashuhuri, jua ni mtu muhimu, muoneshe umuhimu na watu watapenda kukutana na wewe.Ili kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kutengeneza marafiki wengi.

=•Tenga muda wa kufanya kazi sana na kisha tenga muda wa mapumziko. Tenga juma moja la kupumzika kila baada ya miezi sita.  Na unapotoka kwenye mapumziko, tenga tarehe ya mapumziko yanayofuata. Kadiri unavyofanya kazi sana ndivyo mwili wako unahitaji mapumziko pia, la sivyo utapata uchovu mkubwa utakaokukwamisha.

=•Msongo utakuua. Epuka sana msongo kwenye maisha yako. Msongo unatokana na hofu ambazo mtu anakuwa amejijengea, ondokana na hofu ulizonazo na hutakuwa na msongo. Jua kila kitu kitakwenda vizuri kama utachukua hatua sahihi.

=•Unapogundua una msongo mkali, jipe siku ya mapumziko, hata kama huumwi. Mapumziko haya yatapunguza msongo kwa kujiweka mbali na kazi. Lakini pia yatakuepusha kufanya makosa pale unapofanya maamuzi ukiwa na msongo.

=•Glasi imejaa mara zote. Ipo njia ya kupima mtazamo wa mtu, kwa kuweka maji nusu glasi kisha kumuuliza mtu aeleze glasi na maji. Wenye mtazamo chanya wanasema glasi imejaa nusu, wenye mtazamo hasi wanasema glasi iko tupu  nusu. Wenye mtazamo wa kujiamini wanaona glasi imejaa mara zote. Mara zote chukulia kile unachokutana kwa mtazamo chanya na jiulize unawezaje kunufaika nacho zaidi.

=•Sehemu kubwa ya hofu ulizonazo unajidanganya mwenyewe. Akili zetu zipo vizuri sana kwenye kutengeneza hofu, huwa zinatabiri mambo yatakuwa mabaya zaidi. Lakini mara zote mambo huwa hayawi mabaya kama tunavyotegemea. Hivyo usisikilize sana hofu zako.

=•Furahia kushindwa kwako. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa sana bila ya kushindwa. Hivyo unaposhindwa furahia, kwa sababu ni njia ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

=•Fedha siyo sawa na furaha. Lengo lako kuu kwenye kile unachofanya lisiwe fedha, bali anza kwa kupenda kile unachofanya na kutoa mchango wako kwa wengine. Na furaha unayoweza kuipata kwenye fedha ni kuwasaidia wengine.

Asante sana naamini lipo jambo umejifunza kazi kwako kuchukua hatua ,pia nakukaribisha upate chambuzi mbali mbali za vitabu kwa lugh ya kiswahili jiunge nasi ili uweze kujifunza kila siku na uboreshe kazi zako kupitia usomaji wa vitabu,utatumiwa kwenye WhatApp ,email pamoja na Telegram Mungu akubariki tuwasiliane 0767702659 Lackius Robert.


Thursday, November 05, 2020

HUWEZI KUFANANA NA SISI,Hadithi ya Mbwa Mwitu na Digidigi.

Habari za asubuhi ndugu yangu mpendwa karibu katika mwendelezo wa makala za kila siku kupitia blog hii,lengo kuu ni kukuongezea maarifa zaidi.

Leo tunaenda kupata funzo kutoka kwenye hadithi ya Digidigi pamoja na Mbwa Mwitu lipo jambo utajifunza karibu,

Siku moja Mbwa mwitu alikuwa katika harakati za mawindo msituni,Mara gafla akakutana na kundi moja la Digidigi wametulia wanakula majani kwa sababu alikuwa ana njaa kali ikabidi aanze kunyatia nyatia ili aweze kumshika mmoja wapo ajipatie kitoweo.Lakini kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndivyo wanyama wale walivyokuwa hawaachani watoto mbele wakubwa nyuma.Walikuwa wanakula pamoja na kuchezacheza kwa pamoja kwa kiashiria cha ishara ya upendo .

Hali ile ilimfanya Mbwa mwitu na njaa yake kuachana na jambo lake badala yake alitamani kuwa kama wao,kuishi kama wao maana alipenda sana aina ya maisha waliyonayo Digidigi 

Kwakuwa Mbwa mwitu alitamani sana maisha yale ,akaomba kuongea na kiongozi wao ili aweze kujiunga nao ili waishi pamoja.Kiongozi akamuuliza mbona hufanani na sisi?,Mbwa mwitu akasema ndiyo ila naweza jitahidi kufanana na nyinyi.Kiongozi akamwambia kapunguze mkia wako uchonge vizuri ili ufanane nasisi kisha chongesha vipembe vidogo vidogo uviweke kichwani kisha uje.Mbwa mwitu akafanya kama alivyoambiwa aliporudi kwa kiongozi, akaambiwa ondoka hapa huwezi kufanana na sisi .

Mkia wako ,miguu,kichwa na masikio bado havijaweza kufafana na sisi huna budi kutuacha.Mbwa mwitu aliondoka kwa hasira na majonzi kurudi kwa Mbwa mwitu wenzake na wao walimkataa maana tayali hafanani nao.Aliondoka akatokomea pasipojulikana huku akiwa na majonzi makubwa.

Kuna watu tunafanya vitu kama hivyo tunataka kufanana na kina fulani lakini haiwezi kuwezekana.Baki wewe kama wewe jipende jithamini na kujijali kuna upekee mkubwa upo ndani yako achana na habari za kutaka kuwa kama fulani badala yake kuwa wewe maisha yako yatakuwa bora zaidi.Tafakari chukua hatua juu ya maisha yako.

Nakukaribisha katika huduma ninazotoa ili uweze kufaidika zaidi,natoa huduma ya uandishi wa vitabu,makala na majrida huna hana ya kusema sina muda wa kuandika ninayo program nzuri ambayo itakusaidia.Program ya kubadili sauti kuwa katika maandishi hii itakusaidia sana unachotakiwa ni kuwasiliana na mimi ili uweze kujifunza zaidi 0767702659   email.maarifarobert@gamil.com Lackius Robert karibu tujifunze zaidi.

Mungu akubariki sana .

 

HATUA 6 ZA KUCHUKUA ILI KUBADILI MAISHA YAKO.

Habari za asubuhi ndugu yangu mpendwa,

 Karibu katika siku nyingine tena ambapo tunakutana katika blog yetu pendwa  yenye lengo la kukuongezea maarifa na kuifanya siku yako kuonekana mpya.

Napoleon Hill aliwahi kusema"Kuna sifa moja ambayo mtu anayependa  kushinda anapaswa kuwa nayo , nayo ni kuweka kusudi  na ujuzi wa kile kitu ambacho ana hamu ya kukifanikisha. ”.Hapa chini nimejaribu kukushirikisha maambo hatua kadhaa za kuchukua kutoka kwenye maarifa niliyoyapata kwenye kitabu cha Eat that Frog chake Brian Trace.

Katika kitabu hicho anaelezea jinsi unavyopaswa kumaliza kazi zako kwa wakati huku akitumia neno chura kama kazi yako.Anasema kabla ya kuamua kumla "chura" wako ili uendelee na kazi, lazima uamue unataka kufikia wapi kwenye  maisha yako.Utafiti unaonesha kuwa asilimia 3% ya walioweka malengo ndio waliofanikisha na wengine asilimia 97% walishindwa kuyafanikisha. Kuna hatua zifuatazo unapaswa  kuzizingatia :

1.Amua unataka uwe nani ,kaa chini tafakari chagua eneo ambalo unaona linakufaa lifanyie kazi.''kabla hujaamza kupanda ngazi ya mafanikio hakikisha ,ngazi imeninginia katika sehemu sahihi ya jengo".Lengo ni kukusaidia kufika salama katika safari yako.

2.Andika sehemu.Chukua kipande cha karatasi andika malengo yako ,wakati unaandika hakikisha unaandika malengo ambayo yanaweza kutimizika.kosa kubwa tunalofanya wengi ni kuandika malengo ambayo yapo nje ya uwezo wetu mfano mtu hana hata baiskeli anasema ninataka kununua Ndege yaani Aeroplane hiyo inakuwa ni ngumu.Kwanza kipato chako,kazi unayofanya inawezekana hairuhusu kuipata mpaka utakapokufa.Inapendeza uweke lengo ambalo unaamini ndani ya muda fulani utalitimiza.

3.Weka ukomo wa malengo yako.Maamuzi au malengo yasiyo na ukomo yanakuwa hayana uharaka ,hivyo unapopanga malengo hakikisha yanakuwa na ukomo ili kuepusha kughairisha mara kwa mara.Pia ukomo huo utakusaidia sana katika kukupa hamasa ya ufanyaji wa kazi hiyo ili uimalize kwa wakati.

4.Andika vitu vyote ambavyo unahisi ukiwa navyo vinaweza kukusaidia kuyafikia malengo yako.Hili ni muhimu maana linakusaidia wewe kuweza kuhakikisha unaweka sawa na kuwa na utayali mkubwa katika kufanya kitu hicho.

5. Pangilia vizuri mahitaji yako,weka vipaumbele/ pangilia vitu vya msingi na uenende navyo.

6. Chukua hatua.Hapa unashauriwa kufanya chochote, kumbuka "mpango wa wastani uliotekelezwa kwa nguvu ni bora zaidi kuliko mipango mingi  ambayo hakuna kitu kilichofanyika". 

Naamini lipo jambo utalichukua na kulifanyia kazi.
Wish you all the best mungu akubariki.Tuwasiliane zaidi 0767702659 Lackius Robert

Wednesday, November 04, 2020

USISHINDWE KUKAMILISHA REPORT AU KITABU CHAKO TIBA KAMILI HII HAPA.

 Habari ndugu yangu mpendwa ni matumaini yangu uanendelea vizuri na utendaji kazi wako wa kila siku,siku ya leo ninayo furaha kubwa ya kukutangazia huduma ninazotoa ni matumaini yangu utaweza kuguswa kwa namna moja au nyingine.

Lackius Robert ni kijana wa kitanzania aliyedhamilia kuleta mapinduzi makubwa hasa hasa kwenye eneo zima linaohusu fikra na mawazo chini ya program ya “Transorming the Idea” ambayo inahusika na uandishi pamoja na ufundishaji.Ambapo kupitia program hiyo unapata huduma zifuatazao 


1.  1. Ninatoa huduma ya tasfri(Translation) kutumia lugha ya Kiswahili na Kiingreza hii inawasaidia ambao wameandika vitabu ,makala,majarida na wanataka yawekwe katika moja ya lugha tajwa.

Kupitia huduma hii nimekuwa nafanya uchambuzi wa vitabu kutumia lugha ya kiswahili kwa hiyo huna haja ya kuendelea kulalamika au kusema huju namna ya kupangilia vitu vya muhimu katia usomaji wako wa viatbu tayali huduma hivyo ninaitoa kwa bei nafuu.Unaweza kubonyza link kujiunga na grup letu la telegram ili uendelee kujifunza zaidi https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM

2.     2. Kuhifadhi nyaraka ambazo wazungumzaji( speakers ) wanakuwa wamefundisha katika semina mbali mbali.Hii inawasaidia wale ambao hawaja weza kuhudhulia semina hiyo kushiriki kwa njia ya usomaji.Kwa hiyo unapokuwa umeandaa semina yako hakun aunachopoteza mafunzo yaliyotolewa yanaendelea kuwepo na yanaweza kutimiwa kama testimony.

3.      3.  Kubadili (sound) maneno na kuyaweka katika (word) maandishi yaani transcription ambapo unapata document ikiwa katika manual transcript.Hii inawasaidia sana watu wanaohitaji kuandika vitu mbali mbali lakini wanakosa muda wa kuandika vitu hivyo inaweza kuwa ni report za kazini,vitabu au makala.Ambapo unanitumia voice note au audio mimi ninachofanya ni kuiweka katika maandishi.

4.      4.  Pia natoa huduma ya kundaa report au kuandika majina kwenye excel hii sana sana inatumika kwa watu ambao wapo bize sana kiasi kwamba wanakosa muda wa kukaa na kuandaa report au kuingiza majina hayo kwenye document husika.

5.       5. Ninatoa mafundisho katika nyanja za ushawishi,ufanisi,conflict management,malengo na maswala mazima ya kujitambua(self awereness) lakini ninaweza kubadilika kuendana na huduma anahitaji mhusika.

Huduma zote hizi hazihitaji mimi na wewe tukutane live /ana kwa ana kila siku mara nyingi zinatumika kwa njia ya mtandao unaweza kupata huduma hizi popote pale ulipo kwa bei nafuu.Njia ya mawasiliano ni WhatsApp ,Email au telegram tuwasiliane zaidi 0767702659 au email  maarifarobert@gmail.com

Karibu sana na mwenyezi mungu akubariki.


KANUNI YA P6 NA FAIDA ZAKE.

Tumia kanuni ya "P6".

Habari ndugu yangu mpendwa,natumaini unaendelea vizuri na kazi zako,karibu katika mwendelezo wa masomo yanayolenga kukupa maarifa zaidi ili uweze kusogea mbele katika maisha yako ya kila siku.Leo hii tunaenda kupata somo kidogo kuhusu kanuni ya P6 ambayo wataalamu wengi wanapenda sana kuitumia katika kazi zao ,kanuni hii imekuwa na matokeo chanya kwao karibu ujifunze zaidi.

Kanuni hii inasema Proper Prior Planning Prevents Poor Performance maana yake ni  "Mipango sahihi ya awali huzuia utendaji mbovu" unachohitaji ni kalamu na karatasi, mambo yote kuyaweka katika  orodha ya kufanya kwa  siku. Hata kama kuna jambo linaongezeka liongeze katika orodha hiyo,itakusaidia kupima na kujua nini umekamilisha na kipi bado hujakamilisha. Pia inakusaidia kutathimini maendeleo yako na kukuhamasisha kusonga mbele zaidi katika utendaji wako wa kazi.

Jambo jingine linalosisitizwa ni matumizi ya kanuni ya 10/90 wanayotumia watu makini zaidi. Kanuni hii inamaanisha kuwa kama utatumia asilimia 10 %ya muda wako katika kuweka mipango na kupangilia kazi yako kabla hujaanza, utaokoa asilimia 90% ya muda wa kufanya kazi ukishakuwa umeanza. Alex Mackenzie aliwahi kusema ’’ mipango bila vitendo ni mwanzo wa kushindwa’’.

Hivyo basi kila jambo unalotaka kulifanya lazima utilie mkazo katika mipango kila jukumu au shughuli unayotaka kuifanya kwa siku fulani lazima uiwekee muda maalumu wa kujiandaa. Ujue utafainyaje, wakati gani, kwa rasilimali zipi, ni akina nani utafanya nao, nani atafanya nini, muda gani?.Chukua hatua juu ya maisha yako maana wewe ndiye dereva mkuu wala hakuna mtu mwingine.

Naamini kuna jambo umejifunza karibu tuendelee kujifunza zaidi kupitia program zangu za usomaji wa vitabu ambazo ninazifanya kutumi lugha ya kiswahili,Tuwasiliane zaidi mimi ni Lackius Robert 0767702659 au email maarifarobert@gamil.com. au bonyeza link ya telegram uweze kupata vitabu zaidi   https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM .
Karibu tujifunze zaidi na mungu akubariki.

 






Tuesday, November 03, 2020

HATUA KADHAA ZA KUKUWEZESHA KUWA NA MAISHA BORA.

 HATUA KADHAA ZA KUKUWEZESHA KUWA NA MAISHA BORA KUTOKANA NA UCHAMBUZI WA DR.MAKIRITA AMANI.

 VOLUME 1.CHUKUA HATUA

Ø  -Tengeneza akili ya kibilionea. Huwezi kuwa na maisha mazuri kama huna maarifa mazuri unayoingiza kwenye akili yako. Jifunze kila siku kwa kusoma vitabu, kuhudhuria semina na mikutano, kuangalia video, kusikiliza vitabu na kila fursa inayojitokeza mbele yako ya kujifunza.

Ø  -Tengeneza mageuzi yanayokuwezesha kufanikiwa. Charles Darwin aligundua kwamba, viumbe hai wenye nguvu ndiyo walioweza kuishi na kuzaliana, wale waliokuwa dhaifu walikufa. Ili uweze kuwa na maisha mazuri, lazima uweze kutengeneza mageuzi ambayo yatakuwezesha kuendelea kuwepo wakati wote. Uwe tayari kubadilika, usibaki pale ulipo wakati wote.

Ø  -Kuwa mnyenyekevu. Jua kwamba huwezi kujua kila kitu, unahitaji msaada wa wengine kufanikiwa.
Ø  Kuwa na mtu/watu ambaye unamwangalia na anakuhamasisha kuchukua hatua. Watu hawa wanaitwa mamenta, ni watu ambao watakuwezesha kupiga hatua kubwa zaidi ya ulipo sasa.
Ø  Tofauti ya watu masikini na matajiri ni nidhamu. Wote wanapata fedha, matajiri wana nidhamu ya kudhibiti matumizi, kuweka akiba na kuwekeza. Masikini wanatumia fedha yote mpaka iishe, na wanaenda kukopa.

Ø  -Ondokana na mawazo ya bahati nasibu/kamari. Hakuna kitu kizuri kinachotokea kwa bahati na kwa haraka au njia ya mkato. Wapo ambao wamekuwa wakifikiria wanahitaji kushinda bahati nasibu au kamari ili wafanikiwe, dunia haifanyi kazi hivyo. Hata wanaoshinda bahati nasibu au kamari, haiwachukui muda, wanarudi kwenye umasikini.

Ø  -Ondokana na hali ya kuona kwamba huwezi. Tumefundishwa woga na kuona peke yetu hatuwezi, mpaka tufanyiwe kile ambacho wengine wamekuwa wanatufanyia. Unahitaji kuondokana na hali hiyo, na kujua kwamba una uwezo mkubwa wa kufanya makubwa. Utumie.

Ø  Usizichukie jumatatu na kuzipenda ijumaa. Kwa maisha ya mafanikio, siku zote zinapaswa kuwa sawa. Lakini wasio na mafanikio, huchukia jumatatu na kuziita blue Monday na kuzipenda ijumaa na kuziita TGI (Thank God It’s Friday). Fanya kile unachopenda, ambacho utakifanya kila siku ya maisha yako.

Ø - Unaweza kusoma kitabu kimoja kila siku. Kusoma vitabu ni njia ya kutengeneza timu yako ya washauri kwenye kila unachofanya. Tai Lopez amekuwa na utaratibu wa kusoma kitabu kimoja kila siku, kwa kutafuta yale maarifa muhimu ya kitabu na kukazana na hayo. Anasema vitabu vingi vina maelezo mengi ambayo huyahitaji, ukishajua unataka nini, ni rahisi kusoma vitabu vingi.

Ø  -Kugeuza makaa kuwa almasi. Almasi ndiyo kitu kigumu kuliko vitu vyote duniani, lakini inatengenezwa na makaa ambayo siyo magumu sana. kinachotokea ni makaa hayo kuwekwa kwenye presha kubwa mpaka yanakuwa almasi. Hivyo kama wewe unataka kuwa almasi, lazima upitie mazingira magumu, yanayokutengeneza na kukufanya kuwa bora zaidi.

Ø - Jiandae kwa matokeo mabaya, lakini tegemea matokeo mazuri. Mara nyingi mambo hutokea kwenye maisha na kujikuta hatujajiandaa. Hii ni kwa sababu huwa tunafikiri kila kitu kitaenda kama tunavyotaka. Ukweli ni kwamba mambo hayaendi kama tunavyotaka sisi, bali yanaenda kama yanavyoenda yenyewe. Hivyo ni muhimu ujiandae kwenye lolote unalofanya, ili matokeo yakija mabaya, uwe na maandalizi, na yakija mazuri, ufurahie.

Ø  -Nguvu za asili. Jua kwamba kuna nguvu za asili, ambazo huwezi kuzivunja na ukabaki salama. Kama ambavyo ukipanda kwenye jengo refu na kujiachia lazima uanguke chini na uumie, japo ndege hawaumii kwa kufanya hivyo. Kila unachofanya, usilazimishe mambo ambayo yatakwenda kinyume na nguvu za asili. Mfano usitake kuanza biashara leo halafu kesho ikawa ina mafanikio makubwa, kila kitu kinachukua muda.

Ø  -Tengeneza mfumo bora wa kupanga mambo yako. Kupanga kuna faida kuliko kutokupanga. Lakini kupanga pekee hakuna msaada mkubwa. Unahitaji kuwa na mfumo wa mipango, ambapo unakuwa na mpango zaidi ya mmoja. Unakuwa na mpango wa mambo yakienda vizuri, unakuwa na mpango wa mambo yakienda vibaya, halafu unakuwa na mpango wa mambo yanavyoweza kwenda. Kwa kuwa na mipango hiyo mitatu, hutakwama pale mambo yanavyokwenda tofauti na ulivyotegemea.

Ø  -Tengeneza kundi la kukusaidia kufanikiwa. Hakuna mtu anaweza kufanikiwa kwa nguvu zake yeye mwenyewe, kila mtu anahitaji msaada wa watu wengi ili kuweza kupiga hatua kubwa. Unahitaji kuwa na kundi la watu ambao unawategemea na wanakusaidia kupiga hatua. Unahitaji kuwa na marafiki ambao wanakupa hamasa ya kupiga hatua na kukushauri vizuri. Unahitaji kuwa na kundi la washauri (mastermind) ambao wanakufuatilia kwa karibu kwa kila unachofanya. Pia unahitaji wasaidizi kwenye yale unayofanya.

Ø  -Zima ujinga wako. Watu wengi hufikiri wanajua sana kumbe hata hawajui, wengine wanaamini wapo sahihi zaidi kumbe hawapo sahihi. Ili uweze kujifunza, lazima ukubali kuzima ujinga wako. Lazima ukubali kwamba hujui ndiyo ujifunze, lazima ukubali kwamba huenda unakosea ili uwe sahihi. 
Ukiamini unajua na uko sahihi mara zote, utakuwa na ujinga wako milele.

Ø  -Kuwa mmoja kati ya mia moja. Allen Nation aliwahi kunukuliwa kusema siri ya mafanikio kwenye maisha ni kuwapuuza watu 99 kati ya watu 100 na kumsikiliza mtu mmoja. Tafuta yule anayekufaa, yule anayejua na anayekupa hamasa ya kupiga hatua, na msikilize huyo, wapuuze wengine kwa sababu huna muda, fedha wala nguvu za kumsikiliza kila mtu. Kwa upande wa pili, wewe pia unahitaji kuwa mmoja kati ya 100 wanaofanya kile unachofanya wewe, ukifanye kwa ubora na tofauti kubwa sana.

Ø  -Chagua eneo dogo unaloweza kulitumikia vizuri. Watu wengi wamekuwa wakifikiria kuanza na eneo kubwa, kuhudumia kila mtu na kuishia kushindwa kabisa. Chochote unachotaka kufanya, anza kulenga eneo dogo, chagua kikundi cha watu ambao utawatumikia vizuri, ambacho utatawala kwa kile unachofanya, na hapo utatengeneza mafanikio makubwa kuliko kutaka kumfikia kila mtu.

Ø  -Tengeneza makosa madogo na Kila mtu anakosea kwenye maisha, lakini kukosea kwenye mambo madogo na machache, kunakuwezesha kujifunza na kutokurudia makosa hayo. Kukosea kwenye mambo makubwa na mengi, kunaweza kukuondoa kabisa kwenye safari ya mafanikio. Kwa mfano kama hujawahi kuanza biashara kabisa si vyema kuchukua mkopo mkubwa na kwenda kuanza biashara, utakosea halafu utapata hasara kubwa. Badala yake unahitaji kuanza na biashara ndogo na kukua, utajifunza kupitia makosa madogo utakayofanya, ambayo hayataua kabisa biashara yako.

Ø  -Nguvu ya mawasiliano. Siyo unachosema, bali unakisemaje ndiyo kina nguvu. Unahitaji kutengeneza mawasiliano yenye nguvu, ambayo yatakuwezesha kufikisha ujumbe wowote ambao unataka uwafikie watu na waweze kuchukua hatua. Unapotoa ujumbe, wafikirie wale unaowapa ujumbe, na jua kitu gani kinawahamasisha kuchukua hatua. Kwa kujua hayo, utaweza kuwahamasisha kuchukua hatua.

Ø  Kila mtu ashinde au usikubaliane kabisa. Kuna aina tatu za makubaliano, moja mmoja ashinde na mwingine ashindwe, mbili, wote washinde, tatu wote washindwe. Unapoingia kwenye makubaliano yoyote na mtu yeyote, hakikisha kila upande unashinda, kama hilo haliwezekani basi ondoka kwenye makubaliano hayo, hata kama wewe unashinda na upande mwingine unashindwa. Njia pekee ya kujijengea sifa bora na ushirikiano na wengine, ni kumwezesha kila mtu anayejihusisha na wewe kushinda.

NI Nimatumaini yangu makubwa kuwa kuna kitu umeweza kujifunza ,karibu upate uchambuzi wa vitabu kwa lugha ya kiswahili tena kwa bei nafuu vitabu kama Rich dad poor dad,think and grow rich na vitabu vingine kadha wa kadha tayali tumevichambua tayali tuwasiliane kupitia 0767702659 Lackius Robert au bonyeza link kujiunga katika kundi letu la telegram 


MMungu akubariki zaidi.
N

USIKATE TAMAA,Hadithi ya Chura.

 

Karibu ndugu yangu mpendwa upate kuijua zaidi hadithi ya Chura kiziwi lipo jambo utaweza kujifunza.

Ndugu ,

Walikuwepo Vyura waliokuwa wakisafikiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine gafra vyura wawili kutoka katika kundi hilo wakaanguka shimoni.Wenzao walipoangalia urefu wa shimo lile wakawa wanashangilia kwa kuwambia msijisumbue kutoka humo maana shimo ni kubwa ,kubali tu kufa amna namnana ya kujitoa.

Waliobaki juu walianza kuwashangilia huku wakiwaambia acheni kujisumbue eti kuruka kutoka katika shimo hilo ,kubali tu kufa.

Mmoja akakubali kukata tamaa mwishowe akafa akiwa katika shimo hilo.Mwingine akazidi kujitahidi kuluka ili ajitoe katika shimo ,mwishowe akabahatika kujitoa.

Wenzake wakaanza kushangaa kwa jinsi alivyoweza kujitoa katika shimo lile,Kumbe chura yule alikuwa ni kiziwi hivyo hakuwa anasikia waliyokuwa wanasema badala yake alijua wanakazana kumshangilia kwa jitihada anazofanya kujiokoa.

Katika maisha yetu ya kila siku kuna wakati tunahitaji ukiziwi fulani hivi ili mambo yaende wakati ,wengine wanakazana kukukatisha tamaa wewe songa mbele ,ukiwasikia mazuri hutoyafikia utaishia njiani.

Tafakari Chukua hatua juu ya maisha yako.Wish you all the best.

Mimi ni Lackius Robert karibu katika program yetu ya usomaji wa vitabu ambapo tunachambua vitabu kwa lugha ya kiswahili bonyeza link kujiunga katika grup letu la telegram  https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM  .

Karibu tujifunze zaidi vitabu vyote tunavichambua kwa lugha ya kiswahili au tuwasiliane zaidi kupitia 0767702659 mungu akubariki zaidi.

MAKALA YA EMOTIONAL INTELLIGENCE

MAKALA YA EMOTIONAL INTELLIGENCE KUTOKA KATIKA MAANDISHI YA WATU TOFAUTI TOFAUTI.

Maana kubwa ya emotional intelligence ni kuelewa na kuthibiti hisia zako ili uweze kukabiliana na mazingira yanayokukayokuzunguka.

Watu wengi wanaweza kuanzisha mahusiano lakini siyo kila mmoja anaweza kuendelea nayo katika hali ya amani n afuraha wapo wanaoishia katikati kutokana na kukosea katika vitu fulani fulani.

Tafiti nyingi zinaonesha watu wenye akili nyingi au IQ kubwa Ndio wanaweza kufanikiwa lakini zimekuja na usemi kwamba kuwa na akili nyingi haitoshi bali unatakiwa kuwa na uwezo wa kuthibiti hisia ambazo zinaitwa EQ emotional QuotentI akili ya utambuzi,au Emotional Intelligence akili hisia .

Jinsi ya kuboresha mahusiano yako kwa kutumia Emotioanal intelligence kuna hatua nne ambazo ni vema kuzijua ili uweze kuyaboresha zaidi kama nilivyoelezea hapa chini;

Hatua ya kwanza (Self management) Namna ambavyo wewe unaweza kuthibiti hisia zako ,Mfano unapokuwa na hisia za hasira ,kuvurugwa ,kukataliwa,kukatishwa tamaa,mtu kukusemea kitu ambacho hujafanya unawezaje kuthibiti hisia hizo?.

Ata kama una akili nyingi,vipaji vingi sana ukishindwa kuthibiti hisia zako hutoweza kufika mbali.Mara nyingi tunasema unapokuwa umekasirika sana ili usifanye mambo mabaya unatakiwa uwe na uwezo wa kujizuia licha ya hasira inayokusonga.Kama huwezi kumiliki na kutawala hisia zako huwezi kufika mbali katika maisha yako maana kila wakati utakuwa unagombana na watu.

Hatua ya pili (Self awereness )Namna unavyojitambua,kutambua nguvu ulizonazo kihisia,namna ya kutambua udhaifu ulionao kihisia.

Hii ni nzuri kufahamu maana inakusaidia katika kufanya chaguo kulingana na ubora na udhaifu wako.Kuna watu ambao wakishakuwa na hasira au kukwazwa wakiongea lazima wavuruge,lakini ukiwa unatambua nguvu iliyo katika hisia zako pindi ukiwa na hali fulani itakusaidia kuongea vizuri na watu.Kama una hasira unaweza kunyamaza ili usilete vurugu au kuharibu mipango ya watu,kuna wakati unatakiwa kunyamaza siyo kwamba huna cha kusema ila unaogopa kuharibu mahusiano.Kumbuka unaweza kusema neno moja tu likaharibu mahusiano yako na watu tena uliyojenga kwa muda mrefu.

Hatua ya  tatu ni (social awereness)Namna ambavyo unaweza kuchukulia hisia za wengine ,kuthibitbiti hisia zao,uwezo wa kutambua hisia za watu wengine.

Kujua kwa nini mtu fulani anakuwa na hisia za fulani labda hasira au furaha ni vizuri maana utaweza kuongea naye na kumshauri pia uku ukizingatia hisia alizonazo.Ili uweze kufanikiwa unatakiwa kujua namna ya kuenenda na hisia za watu wengine ili uweze kuendana nao vizuri.Kuna wakati unaweza kutamka neno kwako likawa zuri lakini kwa wengine likawa linawakera au kuwabadilisha hali yao kihisia na kuwaletea shida.

Fahamu,jali na uthibiti hisia za watu wengine.

Hatua ya nne(Relationship management) Uwezo wako wewe kuhusiana na watu.

Wezo huu umegawanyika katika sehemu tatu

i.Namna ya kujenga mahusiano

ii.Namna ya kudumisha mahusiano.

iii. Namna ya kukabiliana na mogogoro  tofauti inayokuwa inatokea katika mahusiano .Ukiweza mambo haya matatu mahusiano yako na wengine yatakuwa mazuri.

Ukishindwa kufatria hatua hizi nne nilizoainisha bila kujali una maono kiasi gani,malengo,vipaji na uelewa kiasi gani hutoweza kufanikiwa katika maisha yako hasa hasa eneo lako la hisia.

Pia hapa kuna mwendelzo wa namna ya kutumia emotional intelligence kwa watu wa karibu;

-# Kitu kinachomtofautisha binadamu na mnyama ni uwezo wa kufikiri.

Binadamu ana utashi,ana uwezo wa kufikiri,kuamua na kufanya maamuzi sahihi. Kitu kinachomfanya binadamu awe binadamu ni kufikiri. Kufikiri ndio kazi ya binadamu na hiyo ndiyo inayofanya emotional inetelligence yako kuwa kubwa zaidi.

Ndiyo maana kabla ya kuongea binadamu anatumia muda kufikiri. Kufikiri kunaongeza umakini kitu cha kuongea ili kiweze kumfikia mhusika vizuri.

Karibu upate huduma hizi -program za usomaji wa vitabu ambapo kuna huduma ya SOMA ONLINE WhatsApp na Telegram huduma hizi ni bure na huduma ya NDANI YA KITABU hii channel ipo telegram tu ambapo ina mkusanyiko wa vitabu vinne kila mwezi kwa gharama ya sh.5000/=

1.      - Ninatoa huduma ya tasfri(Translation) kutumia lugha ya Kiswahili na kiingereza hii inawasaidia ambao wameandika vitabu ,makala,majarida na wanataka yawekwe katika moja ya lugha tajwa.

2.       Kuhifadhi nyaraka ambazo wazungumzaji( speakers ) wanakuwa wamefundisha katika semina mbali mbali.Hii inawasaidia wale ambao hawajaweza kuhudhulia semina hiyo kushiriki kwa njia ya usomaji.Kwa hiyo unapokuwa umeandaa semina yako hakuna unachopoteza mafunzo yaliyotolewa yanaendelea kuwepo na yanaweza kutumiwa kama testimony.

3.      -Kubadili (sound) maneno na kuyaweka katika (word) maandishi yaani transcription ambapo unapata document ikiwa katika manual transcript.Hii inawasaidia sana watu wanaohitaji kuandika vitu mbali mbali lakini wanakosa muda wa kuandika vitu hivyo inaweza kuwa ni report za kazini,vitabu au makala.Ambapo unanitumia voice note au audio mimi ninachofanya ni kuiweka katika maandishi.

4.      -Pia natoa huduma ya kundaa report au kuandika majina kwenye excel hii sana sana inatumika kwa watu ambao wapo bize sana kiasi kwamba wanakosa muda wa kukaa na kuandaa report au kuingiza majina hayo kwenye document husika.

5.     - Ninatoa mafundisho katika nyanja za ushawishi,ufanisi, conflict management,malengo na maswala mazima ya kujitambua(self awereness) pia naweza kubadilika kuendana na aina ya mfundisho ambayo mhusika anataka yatolewe

kukuna huduma zinazohitaji tuonane na kuna ambazo hazihitaji mimi na wewe tukutane live /ana kwa ana zote zinatumika kwa njia ya mtandao unaweza kupata huduma hizi popote pale ulipo kwa bei nafuu.Njia ya mawasiliano ni WhatsApp , Email au telegram tuwasiliane zaidi 0767702659 au email  maarifarobert@gmail.com au bonyeza link hii kujiunga na gruop letu la telegram  https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM  .

Karibu sana na mwenyezi mungu akubariki.


Saturday, April 25, 2020

UCHAMBUZI WA KITABU CHA KITABU CHA THINK ANDA GROW RICH NAPOLEON HILL

KARIBU KATIKA SEHEMU INAYOFUATA YA UCHAMBUZI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH  NAPOLEON HILL.


4.Kanuni ya nne kuelekea utajiri ni kupata MAARIFA MAALUMU
Kuna aina mbili za maarifa moja ni ujuzi wa jumla na mwingine ujuzi maalumu.Ujuzi wa jumla pasipo kujali ni mkubwa kiasi gani au ni mwingi kiasi gani una matumizi kidogo sana katika kujipatia pesa.Ujuzi aupati pesa kama haujapangiliwa  na kuongozwa kwa akili kupitia mipango inayotekeleka ya kivitendo kuelekea kwenye lengo lililokuwa dhahiri la kujipatia pesa unayoitaka.Hapa watu wengi waga  wanachanganya na kusemea ujuzi ni nguvu ya kufanya upate unachotaka ,hii haiwezi kutimizika endapo auna mipango mizuri inayotekelezeka.

Mfano ukiangali katika vitengo mbalimbali vyuoni vimejaa watu wenye elimu kubwa,wastarabu na wabobezi lakini linapokuja swala la ujuzi bado hawajabobea katika kuyapanga na kuyatumia maarifa zaidi na kuwafanya wawe matajiri.Ukija kuangalia mtu aliyeelimika siyo lazima awe ni Yule mwenye ujuzi mwingi wa jumla au maalumu.Bali ni wale walioelimika na wamejenga vitivo vya vya akili zao kusudi ziweze kupokea kitu chochote wanachotaka mfano Henry Ford hakuwa na elimu kubwa lakini alikuwa ana uwezo mkubwa wa kuthubutu kufanya jambo pasipo kurudi nyuma tofauti na wengine wanavyoishia njiani.Mtu yeyote aliyeelimika  ni Yule ambaye anaweza kupata maarifa anayoyahitaji,najinsi ya kuyapangilia hayo maarifa katika mipango dhahiri ya kivitendo kupitia sehemu mbali mbali inaweza kuwa kundi lake la kushauriana n.k. 
 
Kabla hujaweza kuwa na uhakika wa uwezo wako wa kubadilisha shauku kuwa katika kiwango chake cha fedha kinacholingana nayo,unahitaji ujuzi maalumu wa huduma,bidhaa au utaalamu unaokusudia kuutoakwa ajili ya kupata utajiri.Pengine unaweza kuhitaji ujuzi maalumu zaidi kuliko vile ulivyokuwa nauwezo au mwelekeo wa kuupata na kama hii itakuwa kweli,unaweza ukauziba udhaifu wako kupitia kundi lako la kushauriana.Mfano Endrew Carnegie hakuwa  anajua kitu kuhusu biashara ya chuma cha pua na hakujisumbua bali ujuzi aliouhitaji aliupata kutoka kwa mmoja kati ya kundi lake la kushauriana.Ukihitaji kuwa tajiri inabidi uongeze jitihada kupitia ujuzi maalumu uliopangiliwa vizuri sana.

Amua juu ya aina ya aina ya ujuzi unaohitaji kuwa nao lengo unalofanyia kazi ili kulifikia na hapa inabidi ujiulize kuhusu taarifa na vyanzo sahihi vya maarifa unayopata;
(i)Uzoefu na elimu ya mtu mwenyewe
(ii)Uzoefu na elimu vinavyopatikana kupitia ushirikiano na watu wengine
(iii)Makataba za umma au kupitia  vitabu na majarida mbalimbali
(iv) Kozi maalumu za mafunzo kama kupiti mafunzo ya madarasa ya jioni na zaidi mfumo wa njia za posta.Hivyo ujuzi maalumu,pamoja na ubunifu  ni viungo bora vya kukufanya wewe kufanikiwa katika kila kitu aunachokifanya.

5.Kanuni ya tano kuelekea utajiri ni kuwa na UBUNIFU
Ubunifu maana yake ni karama ambayo mipango yote inayopangwa na mtu hutengenezwa.Msukukumo shauku hupewa umbo au vitendo kupitia msada wa kitengo cha ubunifu wa akili.
Kuna msemo wa kuwa ,tunaweza kutengeneza  chochote kile ambacho tunakifikiria.Katika zama zote za ustarabu,hizi ndiyo zama zinazofaa zaidi kwa ajili ya ukuzaji na ubunifu kwa sababu ndiyo zama za mabadiliko ya haraka sana.Karibia kila mahali tunakutana na vichocheo vinavyotufanya tuweze kubuni vitu mbalimbali.

Kwa sasa wapo wabunifu mbalimbali mbao wamefanya mambo makubwa ya kuishangaza dunia pia na kuisaidia dunia,hsahasa katika kutatua baadhi ya matatizo mfano waliobuni ndege,meri ,Gaari,vifaa vya mawasiliano kama simu tarakirishi na vitu vnginevyo vingi.Ndugu yangu mpendwa unawezaa ukabuni kitu kwa sasa na kisakusaidia wewe lkutataua baadhi ya matatizo yanayoikumba jamii na kukusaidia wewe mwenyewe.

Mwandishi anaonesha aina mbili za ubunifu:
1.Ubunifu sanisi,Hapa mtu anaweza akapanga fikra za zamani,mawazo au mchanganyiko mpya.Kitivo hiki akiumbi kitu chochote, bali hufanya tu kazi na vitu kama uzoefu,elimu na ushuhuda ambavyo kinalishwa.Kinatumika sana an wagunduzi,ukiacha watu wenye akili nyingi sana ambao hutumia ubunifu wanaposhindwa kutatua tatizo kupitia ubunifu sanisi.

2.Ubunifu wa kujenga,Kupitia kitivo cha ubunifu wa kujenga,akili ya mwanadamu  inayo mawasilianao ya moja kwa moja na nguvu ya uumbaji,hiki ni kitivo ambacho hutumia hisia na ufunuo unaopokelewa yaani hapa mtu anaweza kuwasiliana na akili za watu wengine mfano( mzuri angalia mafundisho ya dini yalivyo unaweza kuelewe ufunuoni nini).Kitivo hiki huwa makini kwa sababau kinahusiana na uwezo wa kutuia hisi za wngine na mara nyingi hufanya kazi chenyewe lakini katika umakini mkubwa sana.

Hivyo kadili kitivo chako cha ubunifu kinavyotumika ndivyo kinavyozoidi kuwa bora na kisivyotumika ndivyo kinavyokuwa dhaifu.Kumbuka kuibadili shauku ya kuwa na pesa siyo jambo linalofanyika siku moja au kwa akauli moja inabidi lifanyike mara nyingi   ili akili na viungo vyako vya mwili vizoee.Viongozi wakubwa wa biashara makampuni,viwanda fedha wasanii waandishi wakubwa wameweza kufanikiwa kwa sababu walikuza vitivo vyao vya ubunifu.Shauku ni wazo tu ,msukumo ni kama nyota ya mbali sana au wingu la muda mfupi sana,nikitu kisichoshikika ni kitu kisocho na thamanimpaka kigeuzwe kuwa kitu kinachoshikika.Hapa ubunifu sanisi ndio unaotumika mara nyingi zaidi katika mchakato huu wa kubadilisha msukumo wa shauku kuwa pesa.Unapaswa kuelekeza umakini wako katika kubdili ubunifu wako sanisi kuwa unaoshikikia maana unahitaji pesa an pesa ni kitu kinachoshukika.Una mipango mbalimbali pesa inabidi itumike uwezi kumwambia mtu ninamipango mbalimbali lakini pesa sina kwa sasa ntakulipa nikiipata ,hapo mtu hawezi kukuelewa. Kila kitu uanweza ukakifanya kwa sababu kimeshawahi kufanyika kabla.

Jiulize ningefanya kitu gani kama ningepewa dola milioni moja
Penye nia pana njia’ Nilisimuliwa na yule mpendwa mwalimu na mchungaji, Frank W. Gunsaulus, ambaye alianza kazi yake ya kuhubiri katika eneo la Stockyards la Kusini mwa Chicago.Wakati Dr. Gunsaulus alipokuwa chuoni, aligundua mapungufu mengi katika mfumo wetu wa elimu, mapungufu ambayo aliamini angeliweza kuyarekebisha ikiwa kama angelikuwa Mkuu wa Chuo. Shauku yake kubwa kabisa ilikuwa ni kuwa kiongozi mkuu wa chuo cha elimu ambacho vijana wadogo wa kiume na wa kike wangeweza kufundishwa “kujifunza kwa vitendo”.

Alifanya uamuzi wa kuanzisha chuo kipya ambacho angeweza kutekeleza wazo lake jipya pasipo kulemazwa na njia za jadi za utoaji elimu. Alihitaji Dolla Milioni moja ili kutekeleza mradi ! Ni wapi angelaza mikono yake kwa kiasi kikubwa hivyo cha pesa? Hilo lilikuwa ni swali lililotawala sehemu kubwa ya mawazo ya mhubiri huyu kijana aliyekuwa na malengo makubwa.
Lakini hakuweza kuonekana kupiga hatua yeyote.

Kila siku aliingia kitandani na lile wazo. Aliamka nalo asubuhi alitembea nalo kila mahali alipokwenda. Aliligeuza tena na tena katika akili yake mpaka likageuka kuwa shauku isiyotulizika. Dolla Millioni moja ni fedha nyingi. Alitambua ukweli huo lakini pia aligundua ukweli kwamba kikwazo pekee ni kile ambacho mtu hujiwekea katika akili yake mwenyewe
Alikuwa mwanafilosofia na pia mhubiri, Dr.Gunsaulus alitambua, kama wafanyavyo wale  wote wanaofanikiwa maishani kuwa, udhahiri wa lengo ndiyo kituo ambapo mtu ni lazima aanzie. Alitambua pia kwamba udhahiri wa lengo huchukua umbo, uhai na nguvu unaposaidiwa na Shauku kubwa kulibadilisha lengo hilo kuwa katika kitu kinacholingana nalo.Alifahamu ukweli wote huu mkubwa, lakini bado hakujua ni wapi au ni jinsi gani angeweza kuweka mikono yake kwenye dola milioni moja. Utaratibu wa asili ingeliweza kuwa ni kukata tamaa na kuacha, akisema , ‘Ah sawa, wazo langu ni zuri lakini siwezi kufanya nalo chochote kwa sababu kamwe siwezi kupata dolla millioni moja zinazohitajika’. Hivyo ndivyo hasa ambavyo watu wengi wangeliweza kusema, lakini sivyo Dr. Gunsaulus alivyosema.Alichosema yeye, na alichokifanya, ni muhimu kiasi kwamba sasa namtambulisha na kumuacha azungumze, mwenyewe.

Siku moja Jumamosi mchana nilikuwa chumbani kwangu nikifikiria njia na namna ya kupata fedha ili kutekeleza mipango yangu. Kwa karibu miaka niwili nilikuwa nikifikiria, lakini sikuwa nimefanya chochote zaidi ya kufikiria.
Muda ulikuwa umewadia wa kuchukua hatua !
Niliamua mara moja kwamba ningeweza kupata dolla milioni moja zilizohitajika, ndani ya wiki moja. Ki vipi? Sikujali kuhusiana na hilo. Jambo kubwa na la muhimu lilikuwa ni uamuzi wa kuzipata fedha ndani ya muda uliopangwa. Dakika niliyofikiria uamuzi huo, hisia ya ajabu ya kujiamini ilinijia kwa namna ambayo kamwe sikuwahi kuhisi hapo kabla. Kitu ndani yangu kilionekana kusema, “Kwanini hukufikia uamuzi huo muda mrefu? Pesa zilikuwa zikikusubiri muda wote !”
Mambo yalianza kutokea kwa haraka. Niliita magazeti na kutangaza kuwa ningeweza kutoa mahubiri(hotuba) asubuhi ya siku iliyofuata yanayohusu, “Ningefanya nini kama ningepata Dola million moja”.‘Nilikwenda kuifanyia kazi hotuba ile mara moja. Ni lazima nikueleze, ukweli haikuwa kazi ngumu kwasababu nilikuwa nikiiandaa hotuba hiyo kwa karibu miaka miwili. Roho yake ilikuwa sehemu yangu !muda kabla ya usiku wa manane nilikuwa nimemaliza kuandika hotuba. Niliingia kitandani na kulala na hisia za kujiamini kwani niliweza kuona mwenyewe kama tayari nilikuwa nazo dolla milioni moja.

Asubuhi iliyofuata niliamka mapema, nikaenda bafuni, nikasoma hotuba, kisha nikapiga magoti na kusali ili hotuba yangu iweze kusikika na mtu ambaye angeliweza kutoa pesa zilizohitajika.‘Wakati nikiwa nasali, tena nilijiwa na zile hisia za kujiamini, kwamba pesa zingeliweza kupatikana haraka. Kwa taharuki niliondoka bila kuchukua hotuba yangu, na sikugundua kosa hilo mpaka nilipokuwa kwenye mimbari yangu na karibu kuanza kuhutubia.

‘Muda ulishakwenda mno kurudi tena kuchukua karatasi, Baraka iliyojea akili yangu ilifikiria vyote ninavyohitaji niakavisema nilipomaliza mikakati ,wakati nimeketi mwanamme mmoj alikuja mbele akanishika mkono akaseam nimeipenda hotuba yako unaweza kupata kiasi hicho ukichokihitaji naitwa Philip Armour.Kesho asubhu alienda ofisini kwake akapewa hicho kiasi cha pesa akaanzisha taasisi ya teknolojia Armor.Dola milioni moja zilipatikana kutokan ana wazo liliotokana ana shauku aliyokuwa nayo muda mrefu,Ndani ya dakika 36 mpango wake ulikamilika na kufanikiwa kupatab kila alicho kihitaji.
Unaweza kupata chochote unachokihitaji kwa kutumia ubunifu wako.

6. Kanuni ya sita kuelekea utajiri ni KUWEKA MIPANGO MATHUBUTI
Umeshajifunza kuwa kila kitu kinachoumbwa na kumilikiwa ukianza na shauku.Shauku hiyo huchukua safari yake ya mwanzo pasipokuwa na kitu chochote mpaka kwenye kitu kinachoweza kushikika katika karakana ya ubunifu mahali ampapo mipango kwa ajili ya mabadiliko huandaliwa.
Katika sura ya pili ulielekezwa kuchukua hatua kama hizi  za kivitendo amabayo kupitia hizo mageuzi haya yanaweza kufanyika.Hapa uanelekezwa namna ya kutengeneza mipango kuwa vitendo:
1.Shirikiana wewe mwenyewe na kundi la watu wengi kadili utakavyohitaji kwa ajili y kutengeneza na kutekeleza mpango wako au mipango yako ya kujichumia fedha,ukitumia kanuni ya ‘’ushirika wa kushirikiana unaleta maendeleo’’.

2.Kabla ujaunda ushirika wako wa kushauriana amua faida zipi na manufaa unayoweza kutoa kwa mwanachama mmoja mmoja wa kundi lako kama malipo ushirikiano wao,hakuna mtu atakayefanya kazi milele pasipokuwa na malipo au kumtegemea mwingine afanye kazi pasipokuwa na malipo yanayofaa ingawaje malipo yale yanaweza yasiwe ya pesa moja kwa moja.
3.Panga kukutana ana wanachama awa kundi lako la kushauriana anagalau mara mbili kwa juma au zaidi kwa malengo makubwa ya kuwezesha uwezekano wakuchuma zaidi pesa.
4.Dumisha masikilizano kati yako na wengine amabao ni wana kikundi cha kushauriana,maana popote pasipo na kusikilizana amna  kitu chochote kinachoendelea,Katika hili zingatia kuyatenda majukumu yako kikamilifu pia kuangalia uezo na ubunifu wao.
Hakuna mtu yeyote mwenye uzoefu wa kutosha,elimu,uwezo wa asili wa kuhakikisha anajipatia utajiri pasipokuwa na ushirikianao na wengine.Mipango mingi inafanikiwa mkiwa katika kundi kubwa la kushauriana pamoja na kuchangiana mada mbalimbali ,maana kuna mipango utakayopanga .Hii itaangaliwana wengine ambao mko nao katika kikundi cha kushauriana.

Ukitengeneza mpango ukashindwa usiache anza upya na mara nyingi zaidi ili ifike hatua ufanikiwe.Mfano Thomas Edison alishindwa zaidi ya mara 1000 kabla hajafanikisha kuunda balbu ya umeme,katika hali hiyo alikutana na vikwazo vingi sana mpaka kufikia hatua ya kubwa ya kuiwasha balbu hiyo.Henry Ford alipata utajiri si kwa sababu alikuwa na akili nyingi bali alikubali kufuata mipango mathubuti mpaka akafanikiwa ,lakini wapo wengi wanaopewa elimu bora kuliko ya Ford lakini bado ni maskini kwa sababu hawana mipango mizuri.
Hakuna mfuasi wa falsafa hii anayeweza kwa makusudi kutegemea kupata utajiri pasipo kukutana na anguko fulani,Anguko linapokuja ni ishara kwamba mipango yako siyo mizuri tengeneza upya mipango yako vizuri usiachie njiani.’’Muachaji kamwe hashindi ,mshindi kamwe haachi’’.
Unapokuwa unachagua watu wa kushirikiana naoa jaribu kuangalia watu wanajari ,wasiopenda kuanguka anguka.wajasiri,amabo wanaweza kujizuia binafsi,matazamo ,uwezo wa kuamua wanaoweza kutengeneza mipango mathubuti hao ndio wanaoweza kukupatia mafanikio/utajiri.

7.Kanuni ya saba kuelekea utajiri ni MAAMUZI

Katika sura hii mwandishi anasema utafiti wa kweli uliofanyika kwa watu zaidi ya 25000 unaonesha wengi wao kitu kinachofanya wanashidwa kufanikiwa ni kushindwa kufanya maamuzi.Wengi wao wanashindwa kufanya maamuzi ya haraka na kuyaghairisha kitu kinachowaletea madhara baadae.
Kuna wakati tunaona fursa ila kutokana na kwamba adui mkubwa kughairisha ametuzingira hivyo tunajikuta tunaipoteza fursa ile.Mfano wa mtu ambaye alikuwa na uharaka katika kutoa maamuzi alikuwa ni Henry Ford amabaye alikuwa ni mkurugenzi wa magari ya “Ford”ambayo yaliamika kuwa na kasi sana.

Watu wengi hushindwa kupata mahitaji yao ya msingi hasa hasa ya kifedha kutokana na kusikiliza maoni ya watu na kuruhusu majungu kutoka kwa ndugu na majirani na kujikuta wanashindwa kufanya maamuzi mazuri wakiofia kuwapoteza.Ili kuweza kuwa na maamuzi mazuri badala ya kufungua mdomo na kuanza kuwaambia yaliyo yako ,Funga modomo fungua macho na masikio ukiufuata ushauri huu utakusaidia sana kuufikia utajiri.Simamia maamuzi yako ,simamia imani yako.Maamuzi ni baba wa IMANI na UJASIRI
Socrate aliona bora kunywa sumu kuliko kubadilisha imani yake na huu ulikuwa ni uamuzi wa busara kwa sababu mengi aliyoyafanya yameisaidia dunia hata na vizazi vinavyokuja.Jiulize je! Maamuzi yangu kuelekea utajiri ni yapi?.

8.Kanuni ya nane kuelekea utajiri ni  UVUMILIVU
Mwandishi anajaribu kuelezea kwa jinsi Uvumilivu ulivyo kitu cha msingi sana  ambacho msingi wake unaleta hamu nia katika ushindi.
Amejaribu kuonesha dalili za mtu mwenye uvumilivu na vitu anavyokuwa amepanga kama ifuatavyo;
(i)malengo ya vitu anavyotaka kuvipata kwa kipindi Fulani. (ii) Hamu ya kufanya kazi yake muda wote. (iii) Anayejitegemea. (iv) Mipango mizuri ya kazi zote anazotaka kuzifanya ili kuufikia utajiri. (v) Anatumia ujuzi  alionao katika kuyatatua magumu anayopitia. (vii)Ushirikiano. (viii) Yuko tayali kubadili tabia mpya lengo kuu ni kuufikia utajiri .
Pia mwandishi amejaribu kuonesha dalili za mtu anayekosa uvumilivu vitu anavyokuwa navyo au anavyoonesha;

(i) Kushindwa kuwa dhahiri kuwa na kitu anachokitaka hapa unamkuta mtu mara anataka kile,ajakaa sawa anataka kingine yeye muda wake wote ni kutaka vitu vingi pasipokuwa na msimamao wa kitu kikbwa kimoja anachotaka.(ii)Mtu wa kughairisha mambo bila kuwa na sababu yoyote. (iii)Anakosa hamu ya kupata maarifa mengine zaidi. (iv)Anakosa kuwa na maamuzi ya msingi mara kwa mara. (v) Tabia ya kuwategemea wengine badala ya kutengeneza njia za kutatua changamoto. (vii) Anakosa matumaini katika kile anachofanya (viii) Anapenda kulalamika kwa makosa madogo madogo yanayofanyika. (ix) Anakosa nia na ni mtu wa majuto muda wote .(xi) Anakosa mipango imara. (xii) Analalamikia umasikini badala ya kuwazia utajiri (xiii) Anapenda kupata badala ya kutoa .(xiv) Anatufa njia za mkato kuupata utajiri (xv) Anaofia sana kukosolewa .

9.Kanuni ya tisa kuelekea utajiri  NGUVU YA AKILI
Mastermind ni kuwa na timu ya watu mahali, ambayo kazi yake ni kukusaidia kufanikiwa na kutekeleza mipango yako. Katika hali hii unachagua watu wanaoendene na wewe kimawazo ili muweze kusaidiana. Hakuna mtu anayeweza kupata nguvu  kubwa ya mafanikio bila ya kuwa na nguvu ya akili yaani mastermind. Kusudi la mastermind ni kubadili maarifa kuwa nguvu, kwa kupanga mipango kuwa  dhahiri  kisha kutafsiri mipango hiyo katika matendo.Jiulize je !watu wangu ninaoungana nao kila siku ni wakina nani?, Majibu yako yafanyie kazi.

10. Kanuni ya kumi kuelekea utajiri SIRI YA USAMBAZAJI WA NGONO
Kitendo hiki huleta furaha kubwa miongoni wa wawili wafanyao kwa wakati sahihi maana huleta hali ya ujasiri, utashi, uvumilivu na uwezo wa ubunifu ambao haujulikani na watu wakati mwingine.Pia ameizungumzia siri ya usambazaji wa ngono katika makundi makubwa matatu;
(i) Utangulizi wa wanadamu
(ii) Utunzaji wa afya
(iii) Mabadiliko ya upatanishi kuwa fikra.
Japokuwa ngono ni nzuri lakini anasema inabidi ifanyike kwa wakati sahihi maana ikiendekeza inaweza kumpoteza mtu kufika katika safari yake ya mafanikio.

11.  Kanuni ya kumi na moja kuelekea utajiri AKILI YA CHINI YA UFAHAMU
Akili ya chini ya fahamu (sub conscious mind ) ni kiunga kinachounganisha kati ya akili laini ya mwanadamu na akili isiyo na mipaka. Akili ya chini ya ufahamu inaweza kutumika kama njia ya kupitisha tamaa zako kuwa sawa na za mwili au pesa.lakini, ukishindwa kupanda matamanio yako ndani yako hautapata matokeo mazuri.
Ili kupata udhibiti wa akili yako unapaswa kutumia faida hizi zifuatazo kuu za hisia zifuatazo: Tamaa, Imani, Upendo, Jinsia, Ushirikiano na Tumaini.
Unapaswa kupata ufahamu zaidi katika vitu hivi ili kuweza kuifikia safari yako ya utajiri Hofu, Wivu, chuki, kulipiza kisasi, Penzi, Ushirikina, Hasira.Tumia ufahamu wako vizuri kwa ajiri ya manufaa yako.

12. Kanuni ya kumi na mbili kuelekea utajiri  ni UBONGO
Mwandishi analinganisha ubongo kama kituo cha Utangazaji ,Kupokea na Kufikiria,Kila ubongo wa mwanadamu ni kituo cha utangazaji na kupokea kwa mtetemeko wa mawazo kutoka sehemu tofauti tofauti.Ubongo wetu na wanyama wengine hauna tofauti kubwa ila tumewashinda tu kwenye kufikiria na kuchukua hatua lakini wao wanaendeshwa kwa hisia tu.Hivyo kama mtu unayetaka kuwa na utajiri kifedha lazima kuruhusu ubongo wako kufikiria kisawa sawa na kuchukua hatua juu ya maisha yako.Kufikiria kunapaswa kuambatana na ubunifu mkubwa wa mawazo mbalimbali yatakayo kupelekea kuupata utajiri.

13. Kanuni ya kumi na tatu kuelekea utajiri  HISIA YA SITA
Mwandishi anailinganisha sixth sense (akili ya sita) kama lango Kwa Hekalu la Hekima
Uelewa wa akili ya sita unakuja tu kwa kutafakari, kupitia maendeleo ya akili kutoka ndani.Mara tu unapofahamu hisia ya sita, utakuwa na uwezo wa kupokea maonyo juu ya hatari zinazokuja kwa wakati ili kuziepuka na kujulishwa fursa za kukumbatia.Akili ya sita haitaweza kamwe kufanya kazi ikiwa mawazo, shaka, na woga zitabaki akilini mwako.
Hofu 6 za msingi ni; Umasikini, Ukosoaji, Afya mbaya, Upotevu wa upendo, uzee, Kifo anaongezea ya saba ambayo ni  ushawishi mbaya. Ili kujikinga na adui huyu, kama watu wote wanaokusanya utajiri mkubwa, lazima uweke matumizi yako ya nguvu kila wakati, hadi ujenge kinga dhidi ya ushawishi mbaya katika akili yako mwenyewe,Tafuta kwa hiari kampuni ya watu wanaokushawishi kufikiria na kutenda kwa mtazamo mzuri, na Tumia nguvu yako ya dhabiti kupata udhibiti wa mawazo yako na ushawishi akili yako ndogo.
Tambua hofu ni hali ya akili tu. Imewekwa chini ya udhibiti na mwelekeo. Tumia maarifa haya kwa faida yako.

MWISHO KWA MAELEZO ZAIDI NA JINSI YA KUJIUNGA NA GRUOP LETU TUMA UJUMBE KUPITIA 0767702659 LACKIUS ROBERT.
KARIBU TUJIFUNZE ZAIDI au bonyeza link hii https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM

Saturday, April 04, 2020

UCHAMBUZI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH (FAKIRI NA KUA TAJIRI.Napoleon Hill

Karibu sana katika program ya uchambuzi wa vitabu program inaitwa "SOMA ONLINE'Improve yourself.

JINA LA KITABU THINK AND GROW RICH, (Fikiri na kua tajiri).
MWANDISHI : NAPOLEON HILL
MCHAMBUZI : LACKIUS ROBERT.

KUHUSU KITABU:
Mwandishi Napoleon Hill japokuwa aliandika vitabu vingi kuhusu mafanikio binafsi lakini kitabu hiki chaThink and Grow Rich ( Fikiri na Kua Tajiri ) alichokiandika mwaka 1937 hakujua kama kinaweza kuwa kizuri na  kubadilisha maisha ya watu wengi. Alitarajia kitabadilisha maisha ya watu wachache ila haikuwa hivo kimebadilisha maisha ya wengi.Mimi na wewe tupo bado tunaendelea kujifunza zaidi,naamini hata vizazi vijavyo watajifunza pia. Kuanzia kuchapishwa kitabu cha kwanza mnamo 1937 hadi kifo cha Napoleon Hill mnamo 1970. Kitabu cha Fikiria na Kua Tajiri kimetolewa nakala zaidi ya milioni 20 na tayali nakala hizo zilikuwa zimeuzwa. Tangu wakati huo mauzo yameongezeka mara nyingi zaidi na ni kitabu kilichoorodheshwa miongoni mwa vitabu bora zaidi hata katika karne ya 21.

Mwandishi anasema mawazo yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa yakawa ya kushikika kama vile mali mfano  pesa kwa kutumia kanuni mbalimbali endapo mtu akiamua.Chanzo kikubwa cha kuanguka miongoni mwa watu wengi ni  kukata tamaa muda mfupi baada  ya kukutana na vikwazo mbalimbali pindi  waanzapo kazi zao walizopanga.Baadhi wanapoanguka wanashindwa kunyanyuka huku wakianza kutoa lawama kwa watu wengine badala ya kutumia anguko ilo kama funzo.
Mafanikio siku zote humjia mtu ambaye anatumia muda wake kuwaza sio yule asiyewaza na mara nyingi kitu kama utajiri kikija unajiuliza sana kwa nini hakikuja mapema ukiangalia ulivyongaika kuupata lakini utajiri huo unaanza na wazo kichwani mwako.

Lengo kuu la kitabu hiki ni kukuelezea siri za utafutaji fedha,Lakini anasisitiza kuwa siri hiyo uanzia kwenye FIKRA ndiyo maana anasema Fikiri na kua tajiri.
Mwandishi anasema watu wote waliofanikiwa ni wale waliokubali kuchukua hatua za kubadili mawazo yao,Kupitia (semina/warsha)conference mbalimbali walizowahi kuhudhulia.
Pindi wapatapo tatizo hulitatua huru kwa kutafuta suruhu ili kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri.

Hivyo inabidi muda wote uanze kufikiria utajiri ili tayali ata ubongo wako uwe na mazoea ya kufikiria hivyo ili siku ukikutana na magumu isiwe rahisi kuyakubali yakurudishe nyuma.
Mwisho.

Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha Think and Grow Rich ,Fikiri kua Tajiri. Kitabu kinafundisha njia za kuelekea kuutafuta utajiri.

Sehemu ya kwanza
1.Hatua ya kwanza kuelekea utajiri ni kuwa na SHAUKU/Tamaa.

Katika sura hii mwandishi anajaribu kumuelezea Bwana mmoja aitwaye Edwin C Barnes ambaye watu walipokuwa wanamuona mtaani walikuwa wanamchukulia kama mzululaji, lakini yeye moyoni mwake alikuwa na shauku kubwa ya kuingia ubia kibiashara na mgunduzi mkubwa wa umeme Thomas Edisoni.
Wakati anaenda ofisi kwa Thomas alikuwa anawaza kama tayali yupo ofisini anafanya kazi licha ya kwamba bado hajafika ofisini na halikuwa anahisi kama tayali yupo mbele ya Edisoni wakizungumza fursa mbalimbali za kibiashara.Miaka michache baadae shauku aliyokuwa nayo kubwa ,au tunaweza kusema ndoto kubwa aliyokuwa nayo Barnes ilikuja kuwa kweli baada ya kuwa katika ofisi moja na Edisoni wakifanya shughuli zao za  kibiashara.Hali hiyo ilipelekea watu wengi waliokuwa wanamjua awali kuanza kumuonea wivu baada ya mafanikio aliyoyapata kutokana ufanyaji biashara na bwana Edison.

Lakini ukija kuangalia Bwana Barnes alitumia muda wake mwingi kuwaza swala hilo na kulichukulia kama kitu ambacho kinaweza kumpatia kile anachokihitaji kwenye maisha yake ,alikataa roho ya woga wa kuzungumza na Bwana Edison.Na haikuwa rahisi kumpata bwana Edison takribani miaka mitano ilipata kabla hajakutana naye ,alikuwa yuko tayali kuanzia chini lakini apate japo nafasi ya kuonana na Edisoni.Hakuwahi kumapata mtu wa kumwambia utaweza labda yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akiamini itawezekana.
Unaweza kuona nikwa jinsi gani shauku inavyoweza kukusababisha kuwa tajiri baada ya kutumia jitihada.

Karibu katika sehemu ya pili ya uchambuzi wa Think and grow Rich Fikiri na kua tajiri.


KANUNI YA PILI KUELEKEA UTAJIRI:
Ni Kuwa na  IMANI.

Imani ndio mkemia mkuu wa akili,imani inapochanganywa na msisimuko wa fikra iliyo  ndani mara moja huchukua msisimuko kuutafsiri na kuusafirisha kwenda kwa nguvu kubwa isiyo ya kawaida.Mfano ukiangalia imani ,mapenzi na ngono ndivyo vitu vyenye nguvu zaidi kushinda mihemuko yote mikubwa.vitu hivi vinapochanganywa vina athari za kufungua moja kwa moja msitali wa mawasiliano baina ya akili ya kawaida  ya kufikiria na ule uwezo usiokuwa wa kawaida.

JINSI YA KUJENGA IMANI
Imani ni hali ya akili ambayo inaweza kuambukizwa kupitia kukiri au maelekezo  yanayojirudia kwenye akili ya ndani kutona na uwepo wa kanuni za kujishauri wewe mwenyewe,Mfano unaamini kuwa ukifanya kazi yako vizuri utapata pesa nyingi zitakazokufanya wewe kuwa tajiri.Hali hii mara nyingi inatokanaa na jinsi unavyoizoesha akili yako kuwa utapata kile unachoiomba mara zote na kwa wakati wowote.
Ni vema uanze mara moja kuitafsiri yenyewe kuwa kitu halisi ambacho kinawezekana , katika hili kuna hatua kadhaa za kuijenga imani yako.
Mara nyingi imani huanzia katika hali ya fikra,ukomo wa utajiri hupangwa na mtu amabaye ndani yake hautawaliwa na vitendo.Imani huondoa ukomo,mfano ukiangalia mtu aliyeanzisha shirika la chuma cha pua la marekani hakuwa maarufu mpaka alikuwa tu msaidizi wa Andrew Carnegie mpaka pale alipozalisha wazo lake ndipo alipokuwa maarufu akaingia madakarani na akapata utajiri.

Licha ya kwamba Napoleon Hill hakuwa mtu wa dini, lakini aliona thamani ya Imani na kuiona ipo karibu na shauku ya kufanikiwa. Kile ambacho Hill huita Imani kwa kweli ni aina ya kujiamini ambayo ina mipaka juu ya udini. Ilikuwa kanuni ambayo mara moja alijifunza kutoka kwa mshauri wake, millionea wa chuma mkubwa Andrew Carnegie.
Kuna watu walikuwa wanamuuliza Andrew Carnegie ni jinsi gani tunaweza kufanikiwa?, alikuwa anawaambia ukishindwa mara moja usikate tamaa wala kuaanza kupunguza imani yako ya kufanikiwa badala yake ongeza juhudi maana viongozi na watu wengi wenye mafanikio waliinuka kutokana na kushindwa miongoni mwao na ndio maana wamefanikiwa zaidi na zaidi.

Kumbuka.
-Kama unaamini umepigwa tayali umepigwa.
-Kama unaamini unashindwa kuthubutu ,hautaweza kweli.
-Kama unafikiri autashinda katika kile uchofanya tayali umeshindwa.
-Kama unafikiri umepoteza tayali umepotea.

Katika dunia mafanikio yoyote tunayafuta kuanzia kwa marafiki wetu unapaswa kulijua hilo.
Kumbuka imani ni chanzo kibubwa cha utajiri ,imani inaanza na wewe mwenyewe kwa kuamini katika kile unachokifanya na kuongeza juhudi zaidi.
Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha Think and Grow Rich ,Fikiri na Kua tajiri.

Dhumuni kubwa ni kukuongezea maarifa juu ya njia za kuzingatia ili uweze kuupata utajiri.

SEHEMU YA TATU: kuelekea utajiri ni KUJISHAURI BINAFSI.

Kujishauri binafsi ni neno linalotumika kwa mawazo yote na vichocheo vyote vinavyosimamiwa binafsi ambavyo hufika katika akili ya mtu kupitia milango mitano ya fahamu.Ni wakala wa mawasiliano kati ya ile sehemu ya akili ambapo fikra za fahamu hutokea na ambayo hudumu kama kiti cha vitendo kwa ajiri ya akili ya ndani.
Kupitia mawazo yanayotawala,mtu huruhusu kubakia katika ufahamu iwe mawazo ni hasi au chanya haijalishi.

Kanuni ya kujishauri binafsi kwa hiyari huifikia akili ya ndani na kuiathiri kwa mawazo hayo.Ukiacha mawazo yanayochukuliwa kutoka angani hakuna mawazo chanya au hasi yanayoweza kuingia akili ya ndani bila msaada wa kanuni  ya  kujishauri binafsi,kwa lugha nyingine maneno yote utambuliwa kupitia milango mitano ya fahamu.
Uwezo wako wa kutumian kanuni hii ya kujishauri binafsi kutategemea nguvu kiasi kikubwa cha ni uwezo uliouweka katika shauku yako ya kupata ile unachokihitaji.

katika sura ya pili kuna hatua sita nilikuelezea  inabidi uweze kuwa imani kubwa ya kile kitu unachokitaka mfano kama unataka pesa nyingi,katika akili yako mwenyewe jione kama una kiasi kamili cha pesa unayoitamani endelea kushikiria mawazo hayo nguvu mpaka utakapoona umbo halisi la pesa.Fanya hivyo kila siku kadri utakavyokuwa uanafanya na imani itakuwa inaongezeka zaidi  fanya mara nyingi uwezavyo usifanye baade ukaacha fanya mpaka uone umezipata.

Katika hatua ya nne kati ya sita kwenye sura ya pili tumefundishwa kuweka mpango kamili kwa ajiri ya kutekeleza shauku yako,anza mara moja kuweka mpango katika vitendo, unapaswa kuanza mara moja usisubilie. Unapowaza akilini mwako fedha ambazo unakusudia kuizipata  jione mwenyewe ukitoa huduma ,au ukianza bidhaa unzokusudi kutoa kama malipo ya hizo fedha hii  hatua muhimu sana kuizingatia.Unavyokuwa unajishauri binafsi unapasw akuzingatia hii ili kuboresha imani yake:

1. Nenda katika sehemu tulivu yenye ukimya inaweza kuwa kitandani au wakati wa usiku,ambapo autasumbuliwa au kukatishwa Fumba macho yako toa sauti yenye kauli ya kiasi cha pesa ulichokusudia kwa jinsi ilivyoandikwa kwenye karatasi.Wakati unafanya hivyo jione kama tayali uko na hicho kiasi,na uweke kwamba labda tarehe 1 mwezi wa kwanza,au baaada ya miaka mitano nitakuwa na kiasi hiki,au kutoa huduma hii,Ninachosubilia ni mpango nitakaoutumia kupata pesa hizi na niatafuata mpango huo nitakapoupokea.

2. Rudia program hii usiku na asubuhi mpaka utakapoweza kuona katika   akili yako pesa unayokusudia kuipata.

3. Weka nakala ya kauli ya maandishi mahali unapoweza kuiona usiku na asubuhi ,Isome kila mara kabla ujalala na wakati unapoamka asubuhi mpaka ikae akilini mwako.Unapokuwa uantumia kanuni hii ujue unatumia kanuni ya kujishuri binafsi,unapaswa kujua imani ndio mhemko wenye nguvu zaidi kushinda zote na wenye faida kubwa zaidi,Uisurusu imani yako iyumbishwa na kitu chochote au kurudi nyuma.

Tukutane siku nyingine.
Nikukumbushe pia unakaribishwa kuchangia pia.
Tuwasiliane kupitia 0767702659 au email maarifarobert @gmai.com
Nakutakia siku njema yenye baraka Mungu akubariki na kukulinda,I'm Lackius Robert karibu.