Karibu ndugu yangu mpendwa upate kuijua zaidi hadithi ya Chura kiziwi lipo jambo utaweza kujifunza.
Ndugu ,
Walikuwepo Vyura waliokuwa wakisafikiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine gafra vyura wawili kutoka katika kundi hilo wakaanguka shimoni.Wenzao walipoangalia urefu wa shimo lile wakawa wanashangilia kwa kuwambia msijisumbue kutoka humo maana shimo ni kubwa ,kubali tu kufa amna namnana ya kujitoa.
Waliobaki juu walianza kuwashangilia huku wakiwaambia acheni kujisumbue eti kuruka kutoka katika shimo hilo ,kubali tu kufa.
Mmoja akakubali kukata tamaa mwishowe akafa akiwa katika shimo hilo.Mwingine akazidi kujitahidi kuluka ili ajitoe katika shimo ,mwishowe akabahatika kujitoa.
Wenzake wakaanza kushangaa kwa jinsi alivyoweza kujitoa katika shimo lile,Kumbe chura yule alikuwa ni kiziwi hivyo hakuwa anasikia waliyokuwa wanasema badala yake alijua wanakazana kumshangilia kwa jitihada anazofanya kujiokoa.
Katika maisha yetu ya kila siku kuna wakati tunahitaji ukiziwi fulani hivi ili mambo yaende wakati ,wengine wanakazana kukukatisha tamaa wewe songa mbele ,ukiwasikia mazuri hutoyafikia utaishia njiani.
Tafakari Chukua hatua juu ya maisha yako.Wish you all the best.
Mimi ni Lackius Robert karibu katika program yetu ya usomaji wa vitabu ambapo tunachambua vitabu kwa lugha ya kiswahili bonyeza link kujiunga katika grup letu la telegram https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM .
Karibu tujifunze zaidi vitabu vyote tunavichambua kwa lugha ya kiswahili au tuwasiliane zaidi kupitia 0767702659 mungu akubariki zaidi.
No comments:
Post a Comment