Saturday, April 04, 2020

UCHAMBUZI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH (FAKIRI NA KUA TAJIRI.Napoleon Hill

Karibu sana katika program ya uchambuzi wa vitabu program inaitwa "SOMA ONLINE'Improve yourself.

JINA LA KITABU THINK AND GROW RICH, (Fikiri na kua tajiri).
MWANDISHI : NAPOLEON HILL
MCHAMBUZI : LACKIUS ROBERT.

KUHUSU KITABU:
Mwandishi Napoleon Hill japokuwa aliandika vitabu vingi kuhusu mafanikio binafsi lakini kitabu hiki chaThink and Grow Rich ( Fikiri na Kua Tajiri ) alichokiandika mwaka 1937 hakujua kama kinaweza kuwa kizuri na  kubadilisha maisha ya watu wengi. Alitarajia kitabadilisha maisha ya watu wachache ila haikuwa hivo kimebadilisha maisha ya wengi.Mimi na wewe tupo bado tunaendelea kujifunza zaidi,naamini hata vizazi vijavyo watajifunza pia. Kuanzia kuchapishwa kitabu cha kwanza mnamo 1937 hadi kifo cha Napoleon Hill mnamo 1970. Kitabu cha Fikiria na Kua Tajiri kimetolewa nakala zaidi ya milioni 20 na tayali nakala hizo zilikuwa zimeuzwa. Tangu wakati huo mauzo yameongezeka mara nyingi zaidi na ni kitabu kilichoorodheshwa miongoni mwa vitabu bora zaidi hata katika karne ya 21.

Mwandishi anasema mawazo yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa yakawa ya kushikika kama vile mali mfano  pesa kwa kutumia kanuni mbalimbali endapo mtu akiamua.Chanzo kikubwa cha kuanguka miongoni mwa watu wengi ni  kukata tamaa muda mfupi baada  ya kukutana na vikwazo mbalimbali pindi  waanzapo kazi zao walizopanga.Baadhi wanapoanguka wanashindwa kunyanyuka huku wakianza kutoa lawama kwa watu wengine badala ya kutumia anguko ilo kama funzo.
Mafanikio siku zote humjia mtu ambaye anatumia muda wake kuwaza sio yule asiyewaza na mara nyingi kitu kama utajiri kikija unajiuliza sana kwa nini hakikuja mapema ukiangalia ulivyongaika kuupata lakini utajiri huo unaanza na wazo kichwani mwako.

Lengo kuu la kitabu hiki ni kukuelezea siri za utafutaji fedha,Lakini anasisitiza kuwa siri hiyo uanzia kwenye FIKRA ndiyo maana anasema Fikiri na kua tajiri.
Mwandishi anasema watu wote waliofanikiwa ni wale waliokubali kuchukua hatua za kubadili mawazo yao,Kupitia (semina/warsha)conference mbalimbali walizowahi kuhudhulia.
Pindi wapatapo tatizo hulitatua huru kwa kutafuta suruhu ili kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri.

Hivyo inabidi muda wote uanze kufikiria utajiri ili tayali ata ubongo wako uwe na mazoea ya kufikiria hivyo ili siku ukikutana na magumu isiwe rahisi kuyakubali yakurudishe nyuma.
Mwisho.

Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha Think and Grow Rich ,Fikiri kua Tajiri. Kitabu kinafundisha njia za kuelekea kuutafuta utajiri.

Sehemu ya kwanza
1.Hatua ya kwanza kuelekea utajiri ni kuwa na SHAUKU/Tamaa.

Katika sura hii mwandishi anajaribu kumuelezea Bwana mmoja aitwaye Edwin C Barnes ambaye watu walipokuwa wanamuona mtaani walikuwa wanamchukulia kama mzululaji, lakini yeye moyoni mwake alikuwa na shauku kubwa ya kuingia ubia kibiashara na mgunduzi mkubwa wa umeme Thomas Edisoni.
Wakati anaenda ofisi kwa Thomas alikuwa anawaza kama tayali yupo ofisini anafanya kazi licha ya kwamba bado hajafika ofisini na halikuwa anahisi kama tayali yupo mbele ya Edisoni wakizungumza fursa mbalimbali za kibiashara.Miaka michache baadae shauku aliyokuwa nayo kubwa ,au tunaweza kusema ndoto kubwa aliyokuwa nayo Barnes ilikuja kuwa kweli baada ya kuwa katika ofisi moja na Edisoni wakifanya shughuli zao za  kibiashara.Hali hiyo ilipelekea watu wengi waliokuwa wanamjua awali kuanza kumuonea wivu baada ya mafanikio aliyoyapata kutokana ufanyaji biashara na bwana Edison.

Lakini ukija kuangalia Bwana Barnes alitumia muda wake mwingi kuwaza swala hilo na kulichukulia kama kitu ambacho kinaweza kumpatia kile anachokihitaji kwenye maisha yake ,alikataa roho ya woga wa kuzungumza na Bwana Edison.Na haikuwa rahisi kumpata bwana Edison takribani miaka mitano ilipata kabla hajakutana naye ,alikuwa yuko tayali kuanzia chini lakini apate japo nafasi ya kuonana na Edisoni.Hakuwahi kumapata mtu wa kumwambia utaweza labda yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akiamini itawezekana.
Unaweza kuona nikwa jinsi gani shauku inavyoweza kukusababisha kuwa tajiri baada ya kutumia jitihada.

Karibu katika sehemu ya pili ya uchambuzi wa Think and grow Rich Fikiri na kua tajiri.


KANUNI YA PILI KUELEKEA UTAJIRI:
Ni Kuwa na  IMANI.

Imani ndio mkemia mkuu wa akili,imani inapochanganywa na msisimuko wa fikra iliyo  ndani mara moja huchukua msisimuko kuutafsiri na kuusafirisha kwenda kwa nguvu kubwa isiyo ya kawaida.Mfano ukiangalia imani ,mapenzi na ngono ndivyo vitu vyenye nguvu zaidi kushinda mihemuko yote mikubwa.vitu hivi vinapochanganywa vina athari za kufungua moja kwa moja msitali wa mawasiliano baina ya akili ya kawaida  ya kufikiria na ule uwezo usiokuwa wa kawaida.

JINSI YA KUJENGA IMANI
Imani ni hali ya akili ambayo inaweza kuambukizwa kupitia kukiri au maelekezo  yanayojirudia kwenye akili ya ndani kutona na uwepo wa kanuni za kujishauri wewe mwenyewe,Mfano unaamini kuwa ukifanya kazi yako vizuri utapata pesa nyingi zitakazokufanya wewe kuwa tajiri.Hali hii mara nyingi inatokanaa na jinsi unavyoizoesha akili yako kuwa utapata kile unachoiomba mara zote na kwa wakati wowote.
Ni vema uanze mara moja kuitafsiri yenyewe kuwa kitu halisi ambacho kinawezekana , katika hili kuna hatua kadhaa za kuijenga imani yako.
Mara nyingi imani huanzia katika hali ya fikra,ukomo wa utajiri hupangwa na mtu amabaye ndani yake hautawaliwa na vitendo.Imani huondoa ukomo,mfano ukiangalia mtu aliyeanzisha shirika la chuma cha pua la marekani hakuwa maarufu mpaka alikuwa tu msaidizi wa Andrew Carnegie mpaka pale alipozalisha wazo lake ndipo alipokuwa maarufu akaingia madakarani na akapata utajiri.

Licha ya kwamba Napoleon Hill hakuwa mtu wa dini, lakini aliona thamani ya Imani na kuiona ipo karibu na shauku ya kufanikiwa. Kile ambacho Hill huita Imani kwa kweli ni aina ya kujiamini ambayo ina mipaka juu ya udini. Ilikuwa kanuni ambayo mara moja alijifunza kutoka kwa mshauri wake, millionea wa chuma mkubwa Andrew Carnegie.
Kuna watu walikuwa wanamuuliza Andrew Carnegie ni jinsi gani tunaweza kufanikiwa?, alikuwa anawaambia ukishindwa mara moja usikate tamaa wala kuaanza kupunguza imani yako ya kufanikiwa badala yake ongeza juhudi maana viongozi na watu wengi wenye mafanikio waliinuka kutokana na kushindwa miongoni mwao na ndio maana wamefanikiwa zaidi na zaidi.

Kumbuka.
-Kama unaamini umepigwa tayali umepigwa.
-Kama unaamini unashindwa kuthubutu ,hautaweza kweli.
-Kama unafikiri autashinda katika kile uchofanya tayali umeshindwa.
-Kama unafikiri umepoteza tayali umepotea.

Katika dunia mafanikio yoyote tunayafuta kuanzia kwa marafiki wetu unapaswa kulijua hilo.
Kumbuka imani ni chanzo kibubwa cha utajiri ,imani inaanza na wewe mwenyewe kwa kuamini katika kile unachokifanya na kuongeza juhudi zaidi.
Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha Think and Grow Rich ,Fikiri na Kua tajiri.

Dhumuni kubwa ni kukuongezea maarifa juu ya njia za kuzingatia ili uweze kuupata utajiri.

SEHEMU YA TATU: kuelekea utajiri ni KUJISHAURI BINAFSI.

Kujishauri binafsi ni neno linalotumika kwa mawazo yote na vichocheo vyote vinavyosimamiwa binafsi ambavyo hufika katika akili ya mtu kupitia milango mitano ya fahamu.Ni wakala wa mawasiliano kati ya ile sehemu ya akili ambapo fikra za fahamu hutokea na ambayo hudumu kama kiti cha vitendo kwa ajiri ya akili ya ndani.
Kupitia mawazo yanayotawala,mtu huruhusu kubakia katika ufahamu iwe mawazo ni hasi au chanya haijalishi.

Kanuni ya kujishauri binafsi kwa hiyari huifikia akili ya ndani na kuiathiri kwa mawazo hayo.Ukiacha mawazo yanayochukuliwa kutoka angani hakuna mawazo chanya au hasi yanayoweza kuingia akili ya ndani bila msaada wa kanuni  ya  kujishauri binafsi,kwa lugha nyingine maneno yote utambuliwa kupitia milango mitano ya fahamu.
Uwezo wako wa kutumian kanuni hii ya kujishauri binafsi kutategemea nguvu kiasi kikubwa cha ni uwezo uliouweka katika shauku yako ya kupata ile unachokihitaji.

katika sura ya pili kuna hatua sita nilikuelezea  inabidi uweze kuwa imani kubwa ya kile kitu unachokitaka mfano kama unataka pesa nyingi,katika akili yako mwenyewe jione kama una kiasi kamili cha pesa unayoitamani endelea kushikiria mawazo hayo nguvu mpaka utakapoona umbo halisi la pesa.Fanya hivyo kila siku kadri utakavyokuwa uanafanya na imani itakuwa inaongezeka zaidi  fanya mara nyingi uwezavyo usifanye baade ukaacha fanya mpaka uone umezipata.

Katika hatua ya nne kati ya sita kwenye sura ya pili tumefundishwa kuweka mpango kamili kwa ajiri ya kutekeleza shauku yako,anza mara moja kuweka mpango katika vitendo, unapaswa kuanza mara moja usisubilie. Unapowaza akilini mwako fedha ambazo unakusudia kuizipata  jione mwenyewe ukitoa huduma ,au ukianza bidhaa unzokusudi kutoa kama malipo ya hizo fedha hii  hatua muhimu sana kuizingatia.Unavyokuwa unajishauri binafsi unapasw akuzingatia hii ili kuboresha imani yake:

1. Nenda katika sehemu tulivu yenye ukimya inaweza kuwa kitandani au wakati wa usiku,ambapo autasumbuliwa au kukatishwa Fumba macho yako toa sauti yenye kauli ya kiasi cha pesa ulichokusudia kwa jinsi ilivyoandikwa kwenye karatasi.Wakati unafanya hivyo jione kama tayali uko na hicho kiasi,na uweke kwamba labda tarehe 1 mwezi wa kwanza,au baaada ya miaka mitano nitakuwa na kiasi hiki,au kutoa huduma hii,Ninachosubilia ni mpango nitakaoutumia kupata pesa hizi na niatafuata mpango huo nitakapoupokea.

2. Rudia program hii usiku na asubuhi mpaka utakapoweza kuona katika   akili yako pesa unayokusudia kuipata.

3. Weka nakala ya kauli ya maandishi mahali unapoweza kuiona usiku na asubuhi ,Isome kila mara kabla ujalala na wakati unapoamka asubuhi mpaka ikae akilini mwako.Unapokuwa uantumia kanuni hii ujue unatumia kanuni ya kujishuri binafsi,unapaswa kujua imani ndio mhemko wenye nguvu zaidi kushinda zote na wenye faida kubwa zaidi,Uisurusu imani yako iyumbishwa na kitu chochote au kurudi nyuma.

Tukutane siku nyingine.
Nikukumbushe pia unakaribishwa kuchangia pia.
Tuwasiliane kupitia 0767702659 au email maarifarobert @gmai.com
Nakutakia siku njema yenye baraka Mungu akubariki na kukulinda,I'm Lackius Robert karibu.


No comments:

Post a Comment