Habari za asubuhi ndugu yangu mpendwa,
Karibu katika siku nyingine tena ambapo tunakutana katika blog yetu pendwa yenye lengo la kukuongezea maarifa na kuifanya siku yako kuonekana mpya.
Napoleon Hill aliwahi kusema"Kuna sifa moja ambayo mtu anayependa kushinda anapaswa kuwa nayo , nayo ni kuweka kusudi na ujuzi wa kile kitu ambacho ana hamu ya kukifanikisha. ”.Hapa chini nimejaribu kukushirikisha maambo hatua kadhaa za kuchukua kutoka kwenye maarifa niliyoyapata kwenye kitabu cha Eat that Frog chake Brian Trace.
Katika kitabu hicho anaelezea jinsi unavyopaswa kumaliza kazi zako kwa wakati huku akitumia neno chura kama kazi yako.Anasema kabla ya kuamua kumla "chura" wako ili uendelee na kazi, lazima uamue unataka kufikia wapi kwenye maisha yako.Utafiti unaonesha kuwa asilimia 3% ya walioweka malengo ndio waliofanikisha na wengine asilimia 97% walishindwa kuyafanikisha. Kuna hatua zifuatazo unapaswa kuzizingatia :
1.Amua unataka uwe nani ,kaa chini tafakari chagua eneo ambalo unaona linakufaa lifanyie kazi.''kabla hujaamza kupanda ngazi ya mafanikio hakikisha ,ngazi imeninginia katika sehemu sahihi ya jengo".Lengo ni kukusaidia kufika salama katika safari yako.
2.Andika sehemu.Chukua kipande cha karatasi andika malengo yako ,wakati unaandika hakikisha unaandika malengo ambayo yanaweza kutimizika.kosa kubwa tunalofanya wengi ni kuandika malengo ambayo yapo nje ya uwezo wetu mfano mtu hana hata baiskeli anasema ninataka kununua Ndege yaani Aeroplane hiyo inakuwa ni ngumu.Kwanza kipato chako,kazi unayofanya inawezekana hairuhusu kuipata mpaka utakapokufa.Inapendeza uweke lengo ambalo unaamini ndani ya muda fulani utalitimiza.
4.Andika vitu vyote ambavyo unahisi ukiwa navyo vinaweza kukusaidia kuyafikia malengo yako.Hili ni muhimu maana linakusaidia wewe kuweza kuhakikisha unaweka sawa na kuwa na utayali mkubwa katika kufanya kitu hicho.
5. Pangilia vizuri mahitaji yako,weka vipaumbele/ pangilia vitu vya msingi na uenende navyo.
6. Chukua hatua.Hapa unashauriwa kufanya chochote, kumbuka "mpango wa wastani uliotekelezwa kwa nguvu ni bora zaidi kuliko mipango mingi ambayo hakuna kitu kilichofanyika".
No comments:
Post a Comment