Habari za saa hizi ndugu yangu mpendwa karibu katika mwendelezo wa makala zetu kila siku zenye lengo la kukuongezea maarifa kila siku.Siku ya leo nimekuandalia vitu kadhaa kutoka kwenye kitabu cha 101 Crucial Lesson they dont teach you in your Business School Ways chake Chris Haroun naamini lipo jambo utaweza kujifunza na kuchukua hatua.
Karibu sana,
=•Ipo njia moja ya kupata chochote unachotaka na njia hiyo ni kuomba. Ombeni na mtapewa ni siri muhimu ya mafanikio kwenye biashara. Kama kuna kitu unataka, omba na wengine watakuwa tayari kukupa, Huwezi kupata kitu bila kuomba bila kuomba utapata lakini utachelewa.
=•Biashara ni watu, haijalishi unajua nini, bali unamjua nani na nani anakujua wewe. Hivyo kazana kukuza zaidi mtandao wako wa watu unaowajua na wanaokujua.
=•Mchukulie kila mtu unayekutana naye kama mtu mashuhuri, jua ni mtu muhimu, muoneshe umuhimu na watu watapenda kukutana na wewe.Ili kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kutengeneza marafiki wengi.
=•Tenga muda wa kufanya kazi sana na kisha tenga muda wa mapumziko. Tenga juma moja la kupumzika kila baada ya miezi sita. Na unapotoka kwenye mapumziko, tenga tarehe ya mapumziko yanayofuata. Kadiri unavyofanya kazi sana ndivyo mwili wako unahitaji mapumziko pia, la sivyo utapata uchovu mkubwa utakaokukwamisha.
=•Msongo utakuua. Epuka sana msongo kwenye maisha yako. Msongo unatokana na hofu ambazo mtu anakuwa amejijengea, ondokana na hofu ulizonazo na hutakuwa na msongo. Jua kila kitu kitakwenda vizuri kama utachukua hatua sahihi.
=•Unapogundua una msongo mkali, jipe siku ya mapumziko, hata kama huumwi. Mapumziko haya yatapunguza msongo kwa kujiweka mbali na kazi. Lakini pia yatakuepusha kufanya makosa pale unapofanya maamuzi ukiwa na msongo.
=•Glasi imejaa mara zote. Ipo njia ya kupima mtazamo wa mtu, kwa kuweka maji nusu glasi kisha kumuuliza mtu aeleze glasi na maji. Wenye mtazamo chanya wanasema glasi imejaa nusu, wenye mtazamo hasi wanasema glasi iko tupu nusu. Wenye mtazamo wa kujiamini wanaona glasi imejaa mara zote. Mara zote chukulia kile unachokutana kwa mtazamo chanya na jiulize unawezaje kunufaika nacho zaidi.
=•Sehemu kubwa ya hofu ulizonazo unajidanganya mwenyewe. Akili zetu zipo vizuri sana kwenye kutengeneza hofu, huwa zinatabiri mambo yatakuwa mabaya zaidi. Lakini mara zote mambo huwa hayawi mabaya kama tunavyotegemea. Hivyo usisikilize sana hofu zako.
=•Furahia kushindwa kwako. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa sana bila ya kushindwa. Hivyo unaposhindwa furahia, kwa sababu ni njia ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
=•Fedha siyo sawa na furaha. Lengo lako kuu kwenye kile unachofanya lisiwe fedha, bali anza kwa kupenda kile unachofanya na kutoa mchango wako kwa wengine. Na furaha unayoweza kuipata kwenye fedha ni kuwasaidia wengine.
Asante sana naamini lipo jambo umejifunza kazi kwako kuchukua hatua ,pia nakukaribisha upate chambuzi mbali mbali za vitabu kwa lugh ya kiswahili jiunge nasi ili uweze kujifunza kila siku na uboreshe kazi zako kupitia usomaji wa vitabu,utatumiwa kwenye WhatApp ,email pamoja na Telegram Mungu akubariki tuwasiliane 0767702659 Lackius Robert.
No comments:
Post a Comment