Sunday, November 08, 2020

JINSI YA KUBRAND MAISHA YAKO 3.

karibu katika makala ya tatu na ya mwisho kutoka katika moja ya mafundisho ambayo aliwahi kutoa Jim Rhon enzi za uhai wake lipo jambo unaweza kujifunza, 

HATUA YA TATU 3. Usijaribu kwenda nje ya mfumo au kukimbizana na muda (DON’T TRY TO BEAT THE SYSTEM).

Ukweli ni kuwa mafanikio yanapitia mchakato mrefu kuona umeyafanikisha,watu wengi hukata tamaa pale wanapoona mambo hayaendi wamekutana na changamoto mbali mbali wanachoshindwa kujua ni kuwa kila kitu kina mfumo wake kinaenda kadili kilivopangwa.Wewe hupaswi kukimbizana na muda kama unaona umepata wazo na ukaanza kulifanyia kazi usikimbilie matokeo ya haraka tulia nenda taratibu hata kama itakuchukua muda upi kama uko katika njia sahihi matokeo utayona bila shida yoyote.

Unaweza kuwa uanjifunzaharaka lakini haimanishi kuwa ndo utegemee kupata matokeo haraka unahitaji muda na utulivu katika kuyapata matokeo.Niliwahi kuanguka mara 7 katika sehemu moja japo kwa vipindi tofauti watu wakawa wanasema kuwa si uache kile unachofanya maana hatuoni hatua unayopiga.Wengine hawawezi kuona hatua au maendeleo yako haaraka wewe ndiye unayekuwa unaona kwa sababu upo katika mfumo,unahitaji kuwa mtu wa kubadilika na kuenda na hali unayokutana nayo.

Kubali kupoteza pesa,nyumba gari na vinginevyo ila siyo AKILI YAKO maana akili yako ndipo kuna mipango yako yote unayotaka kufanya.Akili yako inaweza kukusaidia katika kutafuta mali zote zilizopotea,chunga sana itunze sana na iboreshe akili yako kila siku kwa kuilisha vitu endelevu na vyenye maana.

Tumia hatua hizi tatu kuyaboresha miasha yako kupitia kazi unazozifanya.

Makala hii imeandaliwa na Lackius Robert 0767702659 karibu tujifunze zaidi.

Pia nakukaribisha upate uchambuzi wa vitabu kwa njia ya kiswahili ili uweze kujifunza zaidi na kuongeza maarifa tuwasiliane zaidi.

No comments:

Post a Comment