Habari za asubuhi ndugu yangu mpendwa karibu katika mwendelezo wa makala zetu kila siku ,leo tunaenda kuangalia namna unavyoweza kubrand maisha yako na kuwa mapya hizi zilitolewa na Jim Rohn katika mfululuzo wa mafundisho yake.
HATUA YA KWANZA 1.FIND HOW THINGS WORK(TAFUTA KUJUA NAMA
VITU VINAVYOFANYIKA).
Katika mchakato wa kujua namna gani vitu hufanyika unahitaji kuwa na( IDEA )wazo.Mawazo ya jinsi gani unaweza kutengeneza pesa,namna gani unaweza kufanya kazi zako kwa ubora na vitu vingine vya msingi.Katika hilo ni kwamba mawazo yoyote unayoyapata kuhusu kitu chochote kizuri unahitaji kuyaandika mahali au katika kijitabu chako kidogo ili ukiyahitaji iwe ni rahisi kuyapata anasema “Usitumie kichwa chako kutafuta mafaili yaliyojaa mawazo yako” anachomaanisha ni kuwa unaweza kusahau muda wowote hivyo weka mawazo yako katika maandishi,Ukiyahitaji utayapata haraka na bila kuangaika kwa kukuna kichwa chako uku ukifikiria mawazo uliyoyawaza.
Kwa kutumia mawazo tafuta namna mambo yanavyofanya kazi,
Kama unahitaji kufanikiwa soma mafanikio ya wengine
kupitia usomaji huo unakuwa unapata mawazo mapya na mengi ambayo yanakusaidia
kukuza uelewa wako.
Kama unataka kufurahia soma mawazo
yanayofurahisha.
Kama unataka kuwa na afya njema soma makala
zinazofundisha afya njema.
Usimalize siku bila kusoma chochote, unapaswa kusoma vitu vitakavyoweza kubalisha uchumi wako,jamii yako,imani yako na maisha yako kiujumla.Inawezekana usifanikishe kupata kila kitu unachokitaka ila ukapata vichache ,kupitia hivyo vichache hakikisha unatafuta na kujua namna kitu kinachofanyika.
Wengi wetu tunapata changamoto ya ukosefu wa habari za muhimu ,hakikisha unapata habari za muhimu na nzuri zitakazo kusaidia kujenga uelewa wako kila siku.
Kuwa na furaha kama watoto hata wakati mgumu,mfano angalia watoto walivyo unaweza kumpiga baada ya dakika chache anakuwa amesahau kuwa umempiga anaruhusu maisha mengine yaweze kuendelea.
Usikose kufatria hatua ya pili katika makala inayofuata.
mimi ni Lackius Robert karibu sana tuendelee kujifunza zaidi 0767702659 au maarifarobert.com.
Mungu akubariki zaidi.
No comments:
Post a Comment