Thursday, November 05, 2020

HUWEZI KUFANANA NA SISI,Hadithi ya Mbwa Mwitu na Digidigi.

Habari za asubuhi ndugu yangu mpendwa karibu katika mwendelezo wa makala za kila siku kupitia blog hii,lengo kuu ni kukuongezea maarifa zaidi.

Leo tunaenda kupata funzo kutoka kwenye hadithi ya Digidigi pamoja na Mbwa Mwitu lipo jambo utajifunza karibu,

Siku moja Mbwa mwitu alikuwa katika harakati za mawindo msituni,Mara gafla akakutana na kundi moja la Digidigi wametulia wanakula majani kwa sababu alikuwa ana njaa kali ikabidi aanze kunyatia nyatia ili aweze kumshika mmoja wapo ajipatie kitoweo.Lakini kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndivyo wanyama wale walivyokuwa hawaachani watoto mbele wakubwa nyuma.Walikuwa wanakula pamoja na kuchezacheza kwa pamoja kwa kiashiria cha ishara ya upendo .

Hali ile ilimfanya Mbwa mwitu na njaa yake kuachana na jambo lake badala yake alitamani kuwa kama wao,kuishi kama wao maana alipenda sana aina ya maisha waliyonayo Digidigi 

Kwakuwa Mbwa mwitu alitamani sana maisha yale ,akaomba kuongea na kiongozi wao ili aweze kujiunga nao ili waishi pamoja.Kiongozi akamuuliza mbona hufanani na sisi?,Mbwa mwitu akasema ndiyo ila naweza jitahidi kufanana na nyinyi.Kiongozi akamwambia kapunguze mkia wako uchonge vizuri ili ufanane nasisi kisha chongesha vipembe vidogo vidogo uviweke kichwani kisha uje.Mbwa mwitu akafanya kama alivyoambiwa aliporudi kwa kiongozi, akaambiwa ondoka hapa huwezi kufanana na sisi .

Mkia wako ,miguu,kichwa na masikio bado havijaweza kufafana na sisi huna budi kutuacha.Mbwa mwitu aliondoka kwa hasira na majonzi kurudi kwa Mbwa mwitu wenzake na wao walimkataa maana tayali hafanani nao.Aliondoka akatokomea pasipojulikana huku akiwa na majonzi makubwa.

Kuna watu tunafanya vitu kama hivyo tunataka kufanana na kina fulani lakini haiwezi kuwezekana.Baki wewe kama wewe jipende jithamini na kujijali kuna upekee mkubwa upo ndani yako achana na habari za kutaka kuwa kama fulani badala yake kuwa wewe maisha yako yatakuwa bora zaidi.Tafakari chukua hatua juu ya maisha yako.

Nakukaribisha katika huduma ninazotoa ili uweze kufaidika zaidi,natoa huduma ya uandishi wa vitabu,makala na majrida huna hana ya kusema sina muda wa kuandika ninayo program nzuri ambayo itakusaidia.Program ya kubadili sauti kuwa katika maandishi hii itakusaidia sana unachotakiwa ni kuwasiliana na mimi ili uweze kujifunza zaidi 0767702659   email.maarifarobert@gamil.com Lackius Robert karibu tujifunze zaidi.

Mungu akubariki sana .

 

No comments:

Post a Comment