Habari za asubuhi ndugu yangu mpendwa karibu katika makala zetu kila siku ambapo unakuwa unapata neno linalokupa hamasa zaidi,leo tunaenda kuangalia hadithi ya muuza maziwa.
Bwana mmoja alipata nafasi ya kuwa anapeleka maziwa katika hoteli fulani hapa mjini.Bwana huyo alikuwa akiwaza sana lini atapata sehemu angalau ya kupeleka bidhaa yake kwa muda mrefu. Alipofanikiwa kuipata hotel ile alifurahi sana akaanza kuimba uku akishangilia kwa nyimbo na vifijo na ndelemo.Akajua utajiri upo njiani! muda sio mrefu nanunua garina mipango mingine mingi.
Aliweza kuelewana na wahusika na akaanza kutoa huduma hiyo ,ila jambo la ajabu na la kushangaza ni kuwa ni aliweza kutoa huduma hiyo miezi miwili tu akawa ameishiwa hakuwa na maziwa tena.Alisahau kuwa "ujasiri hauwezi kukupa mafanikio ila unakupa nguvu ya kupambana na maisha".pia umoja ni nguvu utengano ni udhaifu alihitaji kufanya kazi hiyo peke yake na furaha ikageuka kuwa majuto.
Maziwa alikuwa anatoa kwa Ng'ombe zake mwenyewe zilipoacha kutoa ,tenda ikamshinda .Akapewa mtu mwingine mwenye uwezo na network nzuri ya wauza maziwa mengine kutika sehemu tofauti tofauti waliokuwa wanamletea maziwa.Akawa ana nguvu na support ya kutosha kupeleka maziwa hotelini tofauti na yule wa mwanzo.
Kuna wakati sisi tunalalamika kuwa hatupati fursa ,sisi ni watu wa bahati mbaya lakini ukweli ni kuwa tunazipoteza wenyewe.Mtu huyo alipoteza tenda hivi hivi sababu hakutaka kutengeneza network ya watu watakaomletea maziwa kwa bei nzuri tu ili aboreshe mahusiano na biashara yake.Tuitumie vizuri fursa tunayoipata.
Tunahitaji watu ili kuweza kusonga mbele zaidi ,natumaini lipo jambo umejifunza leo.Mimi ni Lackius Robert karibu tuendelee kujifunza zaidi tuwasiliane 0767702659 mungu akubariki.
No comments:
Post a Comment