MAKALA YA EMOTIONAL INTELLIGENCE KUTOKA KATIKA MAANDISHI YA WATU TOFAUTI TOFAUTI.
Maana kubwa ya emotional intelligence ni kuelewa na kuthibiti hisia zako ili uweze kukabiliana na mazingira yanayokukayokuzunguka.
Watu wengi wanaweza kuanzisha mahusiano lakini siyo kila mmoja anaweza kuendelea nayo katika hali ya amani n afuraha wapo wanaoishia katikati kutokana na kukosea katika vitu fulani fulani.
Tafiti nyingi zinaonesha watu wenye akili nyingi au IQ kubwa Ndio wanaweza kufanikiwa lakini zimekuja na usemi kwamba kuwa na akili nyingi haitoshi bali unatakiwa kuwa na uwezo wa kuthibiti hisia ambazo zinaitwa EQ emotional QuotentI akili ya utambuzi,au Emotional Intelligence akili hisia .
Jinsi ya kuboresha mahusiano yako kwa kutumia Emotioanal intelligence kuna hatua nne ambazo ni vema kuzijua ili uweze kuyaboresha zaidi kama nilivyoelezea hapa chini;
Hatua ya kwanza (Self management) Namna ambavyo wewe unaweza kuthibiti hisia zako ,Mfano unapokuwa na hisia za hasira ,kuvurugwa ,kukataliwa,kukatishwa tamaa,mtu kukusemea kitu ambacho hujafanya unawezaje kuthibiti hisia hizo?.
Ata kama una akili nyingi,vipaji vingi sana ukishindwa kuthibiti hisia zako hutoweza kufika mbali.Mara nyingi tunasema unapokuwa umekasirika sana ili usifanye mambo mabaya unatakiwa uwe na uwezo wa kujizuia licha ya hasira inayokusonga.Kama huwezi kumiliki na kutawala hisia zako huwezi kufika mbali katika maisha yako maana kila wakati utakuwa unagombana na watu.
Hatua ya pili (Self awereness )Namna unavyojitambua,kutambua nguvu ulizonazo kihisia,namna ya kutambua udhaifu ulionao kihisia.
Hii ni nzuri kufahamu maana inakusaidia katika kufanya chaguo kulingana na ubora na udhaifu wako.Kuna watu ambao wakishakuwa na hasira au kukwazwa wakiongea lazima wavuruge,lakini ukiwa unatambua nguvu iliyo katika hisia zako pindi ukiwa na hali fulani itakusaidia kuongea vizuri na watu.Kama una hasira unaweza kunyamaza ili usilete vurugu au kuharibu mipango ya watu,kuna wakati unatakiwa kunyamaza siyo kwamba huna cha kusema ila unaogopa kuharibu mahusiano.Kumbuka unaweza kusema neno moja tu likaharibu mahusiano yako na watu tena uliyojenga kwa muda mrefu.
Hatua ya tatu ni (social awereness)Namna ambavyo unaweza kuchukulia hisia za wengine ,kuthibitbiti hisia zao,uwezo wa kutambua hisia za watu wengine.
Kujua kwa nini mtu fulani anakuwa na hisia za fulani labda hasira au furaha ni vizuri maana utaweza kuongea naye na kumshauri pia uku ukizingatia hisia alizonazo.Ili uweze kufanikiwa unatakiwa kujua namna ya kuenenda na hisia za watu wengine ili uweze kuendana nao vizuri.Kuna wakati unaweza kutamka neno kwako likawa zuri lakini kwa wengine likawa linawakera au kuwabadilisha hali yao kihisia na kuwaletea shida.
Fahamu,jali na uthibiti hisia za watu wengine.
Hatua ya nne(Relationship management) Uwezo wako wewe kuhusiana na watu.
Wezo huu umegawanyika katika sehemu tatu
i.Namna ya kujenga mahusiano
ii.Namna ya kudumisha mahusiano.
iii. Namna ya kukabiliana na mogogoro tofauti inayokuwa inatokea katika mahusiano .Ukiweza mambo haya matatu mahusiano yako na wengine yatakuwa mazuri.
Ukishindwa kufatria hatua hizi nne nilizoainisha bila kujali una maono kiasi gani,malengo,vipaji na uelewa kiasi gani hutoweza kufanikiwa katika maisha yako hasa hasa eneo lako la hisia.
Pia hapa kuna mwendelzo wa namna ya kutumia emotional intelligence kwa watu wa karibu;
-# Kitu kinachomtofautisha binadamu na mnyama ni uwezo wa kufikiri.
Binadamu ana utashi,ana uwezo wa kufikiri,kuamua na kufanya maamuzi sahihi. Kitu kinachomfanya binadamu awe binadamu ni kufikiri. Kufikiri ndio kazi ya binadamu na hiyo ndiyo inayofanya emotional inetelligence yako kuwa kubwa zaidi.
Ndiyo maana kabla ya kuongea binadamu anatumia muda kufikiri. Kufikiri kunaongeza umakini kitu cha kuongea ili kiweze kumfikia mhusika vizuri.
Karibu upate huduma hizi -program za usomaji wa vitabu ambapo kuna huduma ya SOMA ONLINE WhatsApp na Telegram huduma hizi ni bure na huduma ya NDANI YA KITABU hii channel ipo telegram tu ambapo ina mkusanyiko wa vitabu vinne kila mwezi kwa gharama ya sh.5000/=
1. - Ninatoa huduma ya tasfri(Translation) kutumia lugha ya Kiswahili na kiingereza hii inawasaidia ambao wameandika vitabu ,makala,majarida na wanataka yawekwe katika moja ya lugha tajwa.
2. Kuhifadhi nyaraka ambazo wazungumzaji( speakers ) wanakuwa wamefundisha katika semina mbali mbali.Hii inawasaidia wale ambao hawajaweza kuhudhulia semina hiyo kushiriki kwa njia ya usomaji.Kwa hiyo unapokuwa umeandaa semina yako hakuna unachopoteza mafunzo yaliyotolewa yanaendelea kuwepo na yanaweza kutumiwa kama testimony.
3. -Kubadili (sound) maneno na kuyaweka katika (word) maandishi yaani transcription ambapo unapata document ikiwa katika manual transcript.Hii inawasaidia sana watu wanaohitaji kuandika vitu mbali mbali lakini wanakosa muda wa kuandika vitu hivyo inaweza kuwa ni report za kazini,vitabu au makala.Ambapo unanitumia voice note au audio mimi ninachofanya ni kuiweka katika maandishi.
4. -Pia natoa huduma ya kundaa report au kuandika majina kwenye excel hii sana sana inatumika kwa watu ambao wapo bize sana kiasi kwamba wanakosa muda wa kukaa na kuandaa report au kuingiza majina hayo kwenye document husika.
5. - Ninatoa mafundisho katika nyanja za ushawishi,ufanisi, conflict management,malengo na maswala mazima ya kujitambua(self awereness) pia naweza kubadilika kuendana na aina ya mfundisho ambayo mhusika anataka yatolewe
kukuna huduma zinazohitaji tuonane na kuna ambazo hazihitaji mimi na wewe tukutane live /ana kwa ana zote zinatumika kwa njia ya mtandao unaweza kupata huduma hizi popote pale ulipo kwa bei nafuu.Njia ya mawasiliano ni WhatsApp , Email au telegram tuwasiliane zaidi 0767702659 au email maarifarobert@gmail.com au bonyeza link hii kujiunga na gruop letu la telegram https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM .
Karibu sana na mwenyezi mungu akubariki.
No comments:
Post a Comment