Wednesday, November 04, 2020

KANUNI YA P6 NA FAIDA ZAKE.

Tumia kanuni ya "P6".

Habari ndugu yangu mpendwa,natumaini unaendelea vizuri na kazi zako,karibu katika mwendelezo wa masomo yanayolenga kukupa maarifa zaidi ili uweze kusogea mbele katika maisha yako ya kila siku.Leo hii tunaenda kupata somo kidogo kuhusu kanuni ya P6 ambayo wataalamu wengi wanapenda sana kuitumia katika kazi zao ,kanuni hii imekuwa na matokeo chanya kwao karibu ujifunze zaidi.

Kanuni hii inasema Proper Prior Planning Prevents Poor Performance maana yake ni  "Mipango sahihi ya awali huzuia utendaji mbovu" unachohitaji ni kalamu na karatasi, mambo yote kuyaweka katika  orodha ya kufanya kwa  siku. Hata kama kuna jambo linaongezeka liongeze katika orodha hiyo,itakusaidia kupima na kujua nini umekamilisha na kipi bado hujakamilisha. Pia inakusaidia kutathimini maendeleo yako na kukuhamasisha kusonga mbele zaidi katika utendaji wako wa kazi.

Jambo jingine linalosisitizwa ni matumizi ya kanuni ya 10/90 wanayotumia watu makini zaidi. Kanuni hii inamaanisha kuwa kama utatumia asilimia 10 %ya muda wako katika kuweka mipango na kupangilia kazi yako kabla hujaanza, utaokoa asilimia 90% ya muda wa kufanya kazi ukishakuwa umeanza. Alex Mackenzie aliwahi kusema ’’ mipango bila vitendo ni mwanzo wa kushindwa’’.

Hivyo basi kila jambo unalotaka kulifanya lazima utilie mkazo katika mipango kila jukumu au shughuli unayotaka kuifanya kwa siku fulani lazima uiwekee muda maalumu wa kujiandaa. Ujue utafainyaje, wakati gani, kwa rasilimali zipi, ni akina nani utafanya nao, nani atafanya nini, muda gani?.Chukua hatua juu ya maisha yako maana wewe ndiye dereva mkuu wala hakuna mtu mwingine.

Naamini kuna jambo umejifunza karibu tuendelee kujifunza zaidi kupitia program zangu za usomaji wa vitabu ambazo ninazifanya kutumi lugha ya kiswahili,Tuwasiliane zaidi mimi ni Lackius Robert 0767702659 au email maarifarobert@gamil.com. au bonyeza link ya telegram uweze kupata vitabu zaidi   https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM .
Karibu tujifunze zaidi na mungu akubariki.

 






No comments:

Post a Comment