Sunday, November 08, 2020

JINSI YA KUBRAND MAISHA YAKO 2.

 HATUA YA PILI 2. GO TO WORK (NENDA KAFANYE ).

Ukiangalia katika hatua ya kwanza tumeona kuwa unahitaji kujua namna vitu vinavyopaswa kufanyika kwa kutumia mawazo yako.Baada ya hapo hatua inayofuata ni kuwa unapaswa kuchukua hatua kwa kile ulichoanzisha,hatua hizi ndizo zinazokuwa zinakupa nguvu na kukuonesha kuwa wewe ni mtu mwenye uthubutu mkubwa katika utendaji wako wa kazi.

Watu wengine wanapokuwa wanakufundisha labda siku za mwisho wa wiki au siku zingine hakikisha unachukua pointi za msingi sana unaweza kuwa unafundishwa katika uchumi au uwekezaji kamwe “usiruhusu kufanya kazi peke yako” unahitaji pia kupata mawazo ya watu wengine ili kuweza kuyaunganisha na mawazo yako.

Kuna mtu alitaka kuniambia kitu nikamwambiaje kabla ujaniambia nioneshe (don’t tell me, show me) usiniambie nioneshe akimaanisha matendo yanaongea kuliko maneno.Fanya zaidi juu ya kitu unachotaka kufanya.Kadili unavyokuwa unachukua hatua mara kwa mara ndivyo unavyokuwa unapata uzoefu na kuondoa hofu ya kuanza anasema massive action ‘the cure all’kuchukua hatua kunanitbu yote.

Tumia kanuni hii katika kila wazo zuri chukua hatua take good idea –take action , Hakikisha unakuwa na mawazo mengi uwezavyo ili uweze kuwa na nafasi ya kuchambua ya msingi.Usipofanyia kazi kile unachojifunza utakuwa mjinga unakpaswa kujitahidi kuwa mtu wa kuchukua hatua mara zote upatapo wazo zuri.

Tumia maarifa unayojifunza kama njia ya kukupeleka katika utajiri.Utajiri ninaouzungumzia siyo utajiri wa pesa maana pesa ni sehemu tu inayotokana na zao la thamani.Nawajua watu wengi wenye pesa lakini ni maskini.Pesa hazikupangii kitu cha kufanya wewe ndiye unayepaswa kuzipangia kama una mipango mingi pesa yako itazidi kukuua na kuzaa zaidi ila kama huna mipango pesa yako haitaweza kuzaa badala yake itapotea bila kujua.

Usikose sehemu inafuata na ya mwisho.

Mimi ni Lackus Robert 0767702659 karibu sana na mungu kaubariki zaidi.

No comments:

Post a Comment