KARIBU KATIKA SEHEMU INAYOFUATA YA UCHAMBUZI WA KITABU CHA THINK AND GROW RICH NAPOLEON HILL.
4.Kanuni ya nne
kuelekea utajiri ni kupata MAARIFA
MAALUMU
Kuna aina mbili za maarifa moja ni ujuzi wa jumla na
mwingine ujuzi maalumu.Ujuzi wa jumla pasipo kujali ni mkubwa kiasi gani au ni
mwingi kiasi gani una matumizi kidogo sana katika kujipatia pesa.Ujuzi aupati
pesa kama haujapangiliwa na kuongozwa
kwa akili kupitia mipango inayotekeleka ya kivitendo kuelekea kwenye lengo
lililokuwa dhahiri la kujipatia pesa unayoitaka.Hapa watu wengi waga wanachanganya na kusemea ujuzi ni nguvu ya
kufanya upate unachotaka ,hii haiwezi kutimizika endapo auna mipango mizuri
inayotekelezeka.
Mfano ukiangali katika vitengo mbalimbali vyuoni vimejaa
watu wenye elimu kubwa,wastarabu na wabobezi lakini linapokuja swala la ujuzi
bado hawajabobea katika kuyapanga na kuyatumia maarifa zaidi na kuwafanya wawe
matajiri.Ukija kuangalia mtu aliyeelimika siyo lazima awe ni Yule mwenye ujuzi
mwingi wa jumla au maalumu.Bali ni wale walioelimika na wamejenga vitivo vya
vya akili zao kusudi ziweze kupokea kitu chochote wanachotaka mfano Henry Ford
hakuwa na elimu kubwa lakini alikuwa ana uwezo mkubwa wa kuthubutu kufanya
jambo pasipo kurudi nyuma tofauti na wengine wanavyoishia njiani.Mtu yeyote
aliyeelimika ni Yule ambaye anaweza
kupata maarifa anayoyahitaji,najinsi ya kuyapangilia hayo maarifa katika
mipango dhahiri ya kivitendo kupitia sehemu mbali mbali inaweza kuwa kundi lake
la kushauriana n.k.
Kabla hujaweza kuwa na uhakika wa uwezo wako wa kubadilisha
shauku kuwa katika kiwango chake cha fedha kinacholingana nayo,unahitaji ujuzi
maalumu wa huduma,bidhaa au utaalamu unaokusudia kuutoakwa ajili ya kupata
utajiri.Pengine unaweza kuhitaji ujuzi maalumu zaidi kuliko vile ulivyokuwa
nauwezo au mwelekeo wa kuupata na kama hii itakuwa kweli,unaweza ukauziba
udhaifu wako kupitia kundi lako la kushauriana.Mfano Endrew Carnegie
hakuwa anajua kitu kuhusu biashara ya
chuma cha pua na hakujisumbua bali ujuzi aliouhitaji aliupata kutoka kwa mmoja
kati ya kundi lake la kushauriana.Ukihitaji kuwa tajiri inabidi uongeze
jitihada kupitia ujuzi maalumu uliopangiliwa vizuri sana.
Amua juu ya aina ya aina ya ujuzi unaohitaji kuwa nao lengo
unalofanyia kazi ili kulifikia na hapa inabidi ujiulize kuhusu taarifa na
vyanzo sahihi vya maarifa unayopata;
(i)Uzoefu na elimu ya mtu mwenyewe
(ii)Uzoefu na elimu vinavyopatikana kupitia ushirikiano na
watu wengine
(iii)Makataba za umma au kupitia vitabu na majarida mbalimbali
(iv) Kozi maalumu za mafunzo kama kupiti mafunzo ya madarasa
ya jioni na zaidi mfumo wa njia za posta.Hivyo ujuzi maalumu,pamoja na
ubunifu ni viungo bora vya kukufanya
wewe kufanikiwa katika kila kitu aunachokifanya.
5.Kanuni ya tano
kuelekea utajiri ni kuwa na UBUNIFU
Ubunifu maana yake ni karama ambayo mipango yote inayopangwa
na mtu hutengenezwa.Msukukumo shauku hupewa umbo au vitendo kupitia msada wa
kitengo cha ubunifu wa akili.
Kuna msemo wa kuwa ,tunaweza
kutengeneza chochote kile ambacho
tunakifikiria.Katika zama zote za ustarabu,hizi ndiyo zama zinazofaa zaidi
kwa ajili ya ukuzaji na ubunifu kwa sababu ndiyo zama za mabadiliko ya haraka sana.Karibia
kila mahali tunakutana na vichocheo vinavyotufanya tuweze kubuni vitu
mbalimbali.
Kwa sasa wapo wabunifu mbalimbali mbao wamefanya mambo
makubwa ya kuishangaza dunia pia na kuisaidia dunia,hsahasa katika kutatua
baadhi ya matatizo mfano waliobuni ndege,meri ,Gaari,vifaa vya mawasiliano kama
simu tarakirishi na vitu vnginevyo vingi.Ndugu yangu mpendwa unawezaa ukabuni
kitu kwa sasa na kisakusaidia wewe lkutataua baadhi ya matatizo yanayoikumba
jamii na kukusaidia wewe mwenyewe.
Mwandishi anaonesha aina mbili za ubunifu:
1.Ubunifu sanisi,Hapa
mtu anaweza akapanga fikra za zamani,mawazo au mchanganyiko mpya.Kitivo hiki
akiumbi kitu chochote, bali hufanya tu kazi na vitu kama uzoefu,elimu na
ushuhuda ambavyo kinalishwa.Kinatumika sana an wagunduzi,ukiacha watu wenye
akili nyingi sana ambao hutumia ubunifu wanaposhindwa kutatua tatizo kupitia
ubunifu sanisi.
2.Ubunifu wa kujenga,Kupitia
kitivo cha ubunifu wa kujenga,akili ya mwanadamu inayo mawasilianao ya moja kwa moja na nguvu
ya uumbaji,hiki ni kitivo ambacho hutumia hisia na ufunuo unaopokelewa yaani
hapa mtu anaweza kuwasiliana na akili za watu wengine mfano( mzuri angalia
mafundisho ya dini yalivyo unaweza kuelewe ufunuoni nini).Kitivo hiki huwa
makini kwa sababau kinahusiana na uwezo wa kutuia hisi za wngine na mara nyingi
hufanya kazi chenyewe lakini katika umakini mkubwa sana.
Hivyo kadili kitivo chako cha ubunifu kinavyotumika ndivyo
kinavyozoidi kuwa bora na kisivyotumika ndivyo kinavyokuwa dhaifu.Kumbuka
kuibadili shauku ya kuwa na pesa siyo jambo linalofanyika siku moja au kwa
akauli moja inabidi lifanyike mara nyingi
ili akili na viungo vyako vya mwili vizoee.Viongozi wakubwa wa biashara
makampuni,viwanda fedha wasanii waandishi wakubwa wameweza kufanikiwa kwa
sababu walikuza vitivo vyao vya ubunifu.Shauku ni wazo tu ,msukumo ni kama
nyota ya mbali sana au wingu la muda mfupi sana,nikitu kisichoshikika ni kitu
kisocho na thamanimpaka kigeuzwe kuwa kitu kinachoshikika.Hapa ubunifu sanisi
ndio unaotumika mara nyingi zaidi katika mchakato huu wa kubadilisha msukumo wa
shauku kuwa pesa.Unapaswa kuelekeza umakini wako katika kubdili ubunifu wako
sanisi kuwa unaoshikikia maana unahitaji pesa an pesa ni kitu
kinachoshukika.Una mipango mbalimbali pesa inabidi itumike uwezi kumwambia mtu
ninamipango mbalimbali lakini pesa sina kwa sasa ntakulipa nikiipata ,hapo mtu
hawezi kukuelewa. Kila kitu uanweza ukakifanya kwa sababu kimeshawahi kufanyika
kabla.
Jiulize ningefanya
kitu gani kama ningepewa dola milioni moja
Penye nia pana njia’ Nilisimuliwa na yule mpendwa mwalimu na
mchungaji, Frank W. Gunsaulus, ambaye alianza kazi yake ya kuhubiri katika eneo
la Stockyards la Kusini mwa Chicago.Wakati Dr. Gunsaulus alipokuwa chuoni,
aligundua mapungufu mengi katika mfumo wetu wa elimu, mapungufu ambayo aliamini
angeliweza kuyarekebisha ikiwa kama angelikuwa Mkuu wa Chuo. Shauku yake kubwa
kabisa ilikuwa ni kuwa kiongozi mkuu wa chuo cha elimu ambacho vijana wadogo wa
kiume na wa kike wangeweza kufundishwa “kujifunza kwa vitendo”.
Alifanya uamuzi wa kuanzisha chuo kipya ambacho angeweza
kutekeleza wazo lake jipya pasipo kulemazwa na njia za jadi za utoaji elimu.
Alihitaji Dolla Milioni moja ili kutekeleza mradi ! Ni wapi angelaza mikono
yake kwa kiasi kikubwa hivyo cha pesa? Hilo lilikuwa ni swali lililotawala
sehemu kubwa ya mawazo ya mhubiri huyu kijana aliyekuwa na malengo makubwa.
Lakini hakuweza kuonekana kupiga hatua yeyote.
Kila siku aliingia kitandani na lile wazo. Aliamka nalo
asubuhi alitembea nalo kila mahali alipokwenda. Aliligeuza tena na tena katika
akili yake mpaka likageuka kuwa shauku isiyotulizika. Dolla Millioni moja ni
fedha nyingi. Alitambua ukweli huo lakini pia aligundua ukweli kwamba kikwazo
pekee ni kile ambacho mtu hujiwekea katika akili yake mwenyewe
Alikuwa mwanafilosofia na pia mhubiri, Dr.Gunsaulus
alitambua, kama wafanyavyo wale wote
wanaofanikiwa maishani kuwa, udhahiri wa lengo ndiyo kituo ambapo mtu ni lazima
aanzie. Alitambua pia kwamba udhahiri wa lengo huchukua umbo, uhai na nguvu
unaposaidiwa na Shauku kubwa kulibadilisha lengo hilo kuwa katika kitu
kinacholingana nalo.Alifahamu ukweli wote huu mkubwa, lakini bado hakujua ni
wapi au ni jinsi gani angeweza kuweka mikono yake kwenye dola milioni moja.
Utaratibu wa asili ingeliweza kuwa ni kukata tamaa na kuacha, akisema , ‘Ah
sawa, wazo langu ni zuri lakini siwezi kufanya nalo chochote kwa sababu kamwe
siwezi kupata dolla millioni moja zinazohitajika’. Hivyo ndivyo hasa ambavyo
watu wengi wangeliweza kusema, lakini sivyo Dr. Gunsaulus alivyosema.Alichosema
yeye, na alichokifanya, ni muhimu kiasi kwamba sasa namtambulisha na kumuacha
azungumze, mwenyewe.
Siku moja Jumamosi mchana nilikuwa chumbani kwangu
nikifikiria njia na namna ya kupata fedha ili kutekeleza mipango yangu. Kwa
karibu miaka niwili nilikuwa nikifikiria, lakini sikuwa nimefanya chochote
zaidi ya kufikiria.
Muda ulikuwa umewadia wa kuchukua hatua !
Niliamua mara moja kwamba ningeweza kupata dolla milioni
moja zilizohitajika, ndani ya wiki moja. Ki vipi? Sikujali kuhusiana na hilo.
Jambo kubwa na la muhimu lilikuwa ni uamuzi wa kuzipata fedha ndani ya muda
uliopangwa. Dakika niliyofikiria uamuzi huo, hisia ya ajabu ya kujiamini
ilinijia kwa namna ambayo kamwe sikuwahi kuhisi hapo kabla. Kitu ndani yangu
kilionekana kusema, “Kwanini hukufikia uamuzi huo muda mrefu? Pesa zilikuwa
zikikusubiri muda wote !”
Mambo yalianza kutokea kwa haraka. Niliita magazeti na
kutangaza kuwa ningeweza kutoa mahubiri(hotuba) asubuhi ya siku iliyofuata
yanayohusu, “Ningefanya nini kama ningepata Dola million moja”.‘Nilikwenda
kuifanyia kazi hotuba ile mara moja. Ni lazima nikueleze, ukweli haikuwa kazi
ngumu kwasababu nilikuwa nikiiandaa hotuba hiyo kwa karibu miaka miwili. Roho
yake ilikuwa sehemu yangu !muda kabla ya usiku wa manane nilikuwa nimemaliza
kuandika hotuba. Niliingia kitandani na kulala na hisia za kujiamini kwani
niliweza kuona mwenyewe kama tayari nilikuwa nazo dolla milioni moja.
Asubuhi
iliyofuata niliamka mapema, nikaenda bafuni, nikasoma hotuba, kisha nikapiga
magoti na kusali ili hotuba yangu iweze kusikika na mtu ambaye angeliweza kutoa
pesa zilizohitajika.‘Wakati nikiwa nasali, tena nilijiwa na zile hisia za
kujiamini, kwamba pesa zingeliweza kupatikana haraka. Kwa taharuki niliondoka
bila kuchukua hotuba yangu, na sikugundua kosa hilo mpaka nilipokuwa kwenye mimbari
yangu na karibu kuanza kuhutubia.
‘Muda ulishakwenda mno kurudi tena kuchukua karatasi, Baraka
iliyojea akili yangu ilifikiria vyote ninavyohitaji niakavisema nilipomaliza
mikakati ,wakati nimeketi mwanamme mmoj alikuja mbele akanishika mkono akaseam
nimeipenda hotuba yako unaweza kupata kiasi hicho ukichokihitaji naitwa Philip
Armour.Kesho asubhu alienda ofisini kwake akapewa hicho kiasi cha pesa
akaanzisha taasisi ya teknolojia Armor.Dola milioni moja zilipatikana kutokan
ana wazo liliotokana ana shauku aliyokuwa nayo muda mrefu,Ndani ya dakika 36
mpango wake ulikamilika na kufanikiwa kupatab kila alicho kihitaji.
Unaweza kupata chochote unachokihitaji kwa kutumia ubunifu
wako.
6. Kanuni ya sita
kuelekea utajiri ni KUWEKA MIPANGO
MATHUBUTI
Umeshajifunza kuwa kila kitu kinachoumbwa na kumilikiwa ukianza
na shauku.Shauku hiyo huchukua safari yake ya mwanzo pasipokuwa na kitu chochote
mpaka kwenye kitu kinachoweza kushikika katika karakana ya ubunifu mahali
ampapo mipango kwa ajili ya mabadiliko huandaliwa.
Katika sura ya pili ulielekezwa kuchukua hatua kama
hizi za kivitendo amabayo kupitia hizo
mageuzi haya yanaweza kufanyika.Hapa uanelekezwa namna ya kutengeneza mipango
kuwa vitendo:
1.Shirikiana wewe mwenyewe na kundi la watu wengi kadili
utakavyohitaji kwa ajili y kutengeneza na kutekeleza mpango wako au mipango
yako ya kujichumia fedha,ukitumia kanuni ya
‘’ushirika wa kushirikiana unaleta maendeleo’’.
2.Kabla ujaunda ushirika wako wa kushauriana amua faida zipi
na manufaa unayoweza kutoa kwa mwanachama mmoja mmoja wa kundi lako kama malipo
ushirikiano wao,hakuna mtu atakayefanya kazi milele pasipokuwa na malipo au
kumtegemea mwingine afanye kazi pasipokuwa na malipo yanayofaa ingawaje malipo
yale yanaweza yasiwe ya pesa moja kwa moja.
3.Panga kukutana ana wanachama awa kundi lako la kushauriana
anagalau mara mbili kwa juma au zaidi kwa malengo makubwa ya kuwezesha
uwezekano wakuchuma zaidi pesa.
4.Dumisha masikilizano kati yako na wengine amabao ni wana
kikundi cha kushauriana,maana popote pasipo na kusikilizana amna kitu chochote kinachoendelea,Katika hili
zingatia kuyatenda majukumu yako kikamilifu pia kuangalia uezo na ubunifu wao.
Hakuna mtu yeyote mwenye uzoefu wa kutosha,elimu,uwezo wa asili
wa kuhakikisha anajipatia utajiri pasipokuwa na ushirikianao na wengine.Mipango
mingi inafanikiwa mkiwa katika kundi kubwa la kushauriana pamoja na kuchangiana
mada mbalimbali ,maana kuna mipango utakayopanga .Hii itaangaliwana wengine
ambao mko nao katika kikundi cha kushauriana.
Ukitengeneza mpango ukashindwa usiache
anza upya na mara nyingi zaidi ili ifike hatua ufanikiwe.Mfano Thomas Edison alishindwa
zaidi ya mara 1000 kabla hajafanikisha kuunda balbu ya umeme,katika hali hiyo
alikutana na vikwazo vingi sana mpaka kufikia hatua ya kubwa ya kuiwasha balbu
hiyo.Henry Ford alipata utajiri si kwa sababu alikuwa na akili nyingi bali
alikubali kufuata mipango mathubuti mpaka akafanikiwa ,lakini wapo wengi
wanaopewa elimu bora kuliko ya Ford lakini bado ni maskini kwa sababu hawana
mipango mizuri.
Hakuna mfuasi wa falsafa hii anayeweza kwa makusudi
kutegemea kupata utajiri pasipo kukutana na anguko fulani,Anguko linapokuja ni
ishara kwamba mipango yako siyo mizuri tengeneza upya mipango yako vizuri
usiachie njiani.’’Muachaji kamwe
hashindi ,mshindi kamwe haachi’’.
Unapokuwa unachagua watu wa kushirikiana naoa jaribu
kuangalia watu wanajari ,wasiopenda kuanguka anguka.wajasiri,amabo wanaweza
kujizuia binafsi,matazamo ,uwezo wa kuamua wanaoweza kutengeneza mipango
mathubuti hao ndio wanaoweza kukupatia mafanikio/utajiri.
7.Kanuni ya saba
kuelekea utajiri ni MAAMUZI
Katika sura hii mwandishi anasema utafiti wa kweli
uliofanyika kwa watu zaidi ya 25000 unaonesha wengi wao kitu kinachofanya
wanashidwa kufanikiwa ni kushindwa kufanya maamuzi.Wengi wao wanashindwa
kufanya maamuzi ya haraka na kuyaghairisha kitu kinachowaletea madhara baadae.
Kuna wakati tunaona fursa ila kutokana na kwamba adui mkubwa
kughairisha ametuzingira hivyo tunajikuta tunaipoteza fursa ile.Mfano wa mtu
ambaye alikuwa na uharaka katika kutoa maamuzi alikuwa ni Henry Ford amabaye
alikuwa ni mkurugenzi wa magari ya “Ford”ambayo yaliamika kuwa na kasi sana.
Watu wengi hushindwa kupata mahitaji yao ya msingi hasa hasa
ya kifedha kutokana na kusikiliza maoni ya watu na kuruhusu majungu kutoka kwa
ndugu na majirani na kujikuta wanashindwa kufanya maamuzi mazuri wakiofia
kuwapoteza.Ili kuweza kuwa na maamuzi mazuri badala ya kufungua mdomo na kuanza
kuwaambia yaliyo yako ,Funga modomo fungua macho na masikio ukiufuata ushauri
huu utakusaidia sana kuufikia utajiri.Simamia maamuzi yako ,simamia imani yako.Maamuzi
ni baba wa IMANI na UJASIRI
Socrate aliona bora kunywa sumu kuliko kubadilisha imani
yake na huu ulikuwa ni uamuzi wa busara kwa sababu mengi aliyoyafanya
yameisaidia dunia hata na vizazi vinavyokuja.Jiulize je! Maamuzi yangu kuelekea
utajiri ni yapi?.
8.Kanuni ya nane
kuelekea utajiri ni UVUMILIVU
Mwandishi anajaribu kuelezea kwa jinsi Uvumilivu ulivyo kitu
cha msingi sana ambacho msingi wake unaleta
hamu nia katika ushindi.
Amejaribu kuonesha dalili za mtu mwenye uvumilivu na vitu
anavyokuwa amepanga kama ifuatavyo;
(i)malengo ya vitu anavyotaka kuvipata kwa kipindi Fulani.
(ii) Hamu ya kufanya kazi yake muda wote. (iii) Anayejitegemea. (iv) Mipango
mizuri ya kazi zote anazotaka kuzifanya ili kuufikia utajiri. (v) Anatumia
ujuzi alionao katika kuyatatua magumu
anayopitia. (vii)Ushirikiano. (viii) Yuko tayali kubadili tabia mpya lengo kuu
ni kuufikia utajiri .
Pia mwandishi
amejaribu kuonesha dalili za mtu anayekosa uvumilivu vitu anavyokuwa navyo au anavyoonesha;
(i) Kushindwa kuwa dhahiri kuwa na kitu anachokitaka hapa
unamkuta mtu mara anataka kile,ajakaa sawa anataka kingine yeye muda wake wote
ni kutaka vitu vingi pasipokuwa na msimamao wa kitu kikbwa kimoja anachotaka.(ii)Mtu
wa kughairisha mambo bila kuwa na sababu yoyote. (iii)Anakosa hamu ya kupata
maarifa mengine zaidi. (iv)Anakosa kuwa na maamuzi ya msingi mara kwa mara. (v)
Tabia ya kuwategemea wengine badala ya kutengeneza njia za kutatua changamoto.
(vii) Anakosa matumaini katika kile anachofanya (viii) Anapenda kulalamika kwa
makosa madogo madogo yanayofanyika. (ix) Anakosa nia na ni mtu wa majuto muda
wote .(xi) Anakosa mipango imara. (xii) Analalamikia umasikini badala ya
kuwazia utajiri (xiii) Anapenda kupata badala ya kutoa .(xiv) Anatufa njia za
mkato kuupata utajiri (xv) Anaofia sana kukosolewa .
9.Kanuni ya tisa
kuelekea utajiri NGUVU YA AKILI
Mastermind ni kuwa na timu ya watu mahali, ambayo kazi yake
ni kukusaidia kufanikiwa na kutekeleza mipango yako. Katika hali hii unachagua watu
wanaoendene na wewe kimawazo ili muweze kusaidiana. Hakuna mtu anayeweza kupata
nguvu kubwa ya mafanikio bila ya kuwa na
nguvu ya akili yaani mastermind. Kusudi la mastermind ni kubadili maarifa kuwa
nguvu, kwa kupanga mipango kuwa dhahiri kisha kutafsiri mipango hiyo katika matendo.Jiulize
je !watu wangu ninaoungana nao kila siku ni wakina nani?, Majibu yako yafanyie
kazi.
10. Kanuni ya kumi
kuelekea utajiri SIRI YA USAMBAZAJI WA
NGONO
Kitendo hiki huleta furaha kubwa miongoni wa wawili wafanyao
kwa wakati sahihi maana huleta hali ya ujasiri, utashi, uvumilivu na uwezo wa
ubunifu ambao haujulikani na watu wakati mwingine.Pia ameizungumzia siri ya
usambazaji wa ngono katika makundi makubwa matatu;
(i) Utangulizi wa wanadamu
(ii) Utunzaji wa afya
(iii) Mabadiliko ya upatanishi kuwa fikra.
Japokuwa ngono ni nzuri lakini anasema inabidi ifanyike kwa
wakati sahihi maana ikiendekeza inaweza kumpoteza mtu kufika katika safari yake
ya mafanikio.
11. Kanuni ya kumi na moja kuelekea utajiri AKILI YA CHINI YA UFAHAMU
Akili ya chini ya fahamu (sub conscious mind ) ni kiunga
kinachounganisha kati ya akili laini ya mwanadamu na akili isiyo na mipaka. Akili
ya chini ya ufahamu inaweza kutumika kama njia ya kupitisha tamaa zako kuwa
sawa na za mwili au pesa.lakini, ukishindwa kupanda matamanio yako ndani yako
hautapata matokeo mazuri.
Ili kupata udhibiti wa akili yako unapaswa kutumia faida
hizi zifuatazo kuu za hisia zifuatazo: Tamaa, Imani, Upendo, Jinsia,
Ushirikiano na Tumaini.
Unapaswa kupata ufahamu zaidi katika vitu hivi ili kuweza
kuifikia safari yako ya utajiri Hofu, Wivu, chuki, kulipiza kisasi, Penzi,
Ushirikina, Hasira.Tumia ufahamu wako vizuri kwa ajiri ya manufaa yako.
12. Kanuni ya kumi na
mbili kuelekea utajiri ni UBONGO
Mwandishi analinganisha ubongo kama kituo cha Utangazaji ,Kupokea
na Kufikiria,Kila ubongo wa mwanadamu ni kituo cha utangazaji na kupokea kwa
mtetemeko wa mawazo kutoka sehemu tofauti tofauti.Ubongo wetu na wanyama
wengine hauna tofauti kubwa ila tumewashinda tu kwenye kufikiria na kuchukua
hatua lakini wao wanaendeshwa kwa hisia tu.Hivyo kama mtu unayetaka kuwa na
utajiri kifedha lazima kuruhusu ubongo wako kufikiria kisawa sawa na kuchukua
hatua juu ya maisha yako.Kufikiria kunapaswa kuambatana na ubunifu mkubwa wa
mawazo mbalimbali yatakayo kupelekea kuupata utajiri.
13. Kanuni ya kumi na
tatu kuelekea utajiri HISIA YA
SITA
Mwandishi anailinganisha sixth sense (akili ya sita) kama lango
Kwa Hekalu la Hekima
Uelewa wa akili ya sita unakuja tu kwa kutafakari, kupitia
maendeleo ya akili kutoka ndani.Mara tu unapofahamu hisia ya sita, utakuwa na
uwezo wa kupokea maonyo juu ya hatari zinazokuja kwa wakati ili kuziepuka na
kujulishwa fursa za kukumbatia.Akili ya sita haitaweza kamwe kufanya kazi ikiwa
mawazo, shaka, na woga zitabaki akilini mwako.
Hofu 6 za msingi ni;
Umasikini, Ukosoaji, Afya mbaya, Upotevu wa upendo, uzee, Kifo anaongezea ya
saba ambayo ni ushawishi mbaya. Ili
kujikinga na adui huyu, kama watu wote wanaokusanya utajiri mkubwa, lazima
uweke matumizi yako ya nguvu kila wakati, hadi ujenge kinga dhidi ya ushawishi
mbaya katika akili yako mwenyewe,Tafuta kwa hiari kampuni ya watu
wanaokushawishi kufikiria na kutenda kwa mtazamo mzuri, na Tumia nguvu yako ya
dhabiti kupata udhibiti wa mawazo yako na ushawishi akili yako ndogo.
Tambua hofu ni hali ya akili tu. Imewekwa chini ya udhibiti
na mwelekeo. Tumia maarifa haya kwa faida yako.
MWISHO KWA MAELEZO ZAIDI NA JINSI YA KUJIUNGA NA GRUOP LETU TUMA UJUMBE KUPITIA 0767702659 LACKIUS ROBERT.
KARIBU TUJIFUNZE ZAIDI au bonyeza link hii https://t.me/SOMAONLINETELEGRAM
No comments:
Post a Comment