Tuesday, August 06, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Visababishi vya migogoro

Ndugu,
Karibu katika mwendelezo unaoelezea visababishi vya migogoro katika sehemu tunazoishi au tunakofanyia kazi zetu:

=•Ubinafsi(Selfishness)
Hali ya mtu kujipenda mwenyewe pasipo kuwajali wengine.Licha ya kwamba tunasema jipende kwanza jisifie kama wakishindwa kukusifu lakini ni vema kuwapa nafasi wengine.

Kitendo cha kuweka mahitaji yake mbele,Kutosikiliza maoni ya watu wengine.Mtu mbinafsi anataka kudhibiti kila kitu kinachotokea katika maisha ,kazini au popote anapokuwa. hivyo, hafikirii mawazo ya wengine kama ni bora zaidi badala yake huona ya kwake ndio bora wakati wote. Kutokana na hali hiyo hali ya mawasiliano na wenzake inatokea iwe ofisini,kanisani ,shuleni kwenye mikutano mbali mbali kitu ambacho baadae kinaleta mgogoro mkubwa.

=•Usaliti,
Usaliti ni ukiukwaji mkubwa wa makubaliano baina na ya mtu mmoja au kikundi.Upo katika mahusiano baina ya wawili,kwenye familia,kazini, kwenye vikundi kama SACCOS ,VICOBA .Usaliti unaleta maumivu makubwa na huathiri malengo na mipango ya watu.
Uchungu wa kusalitiwa mara nyingi hutokea pale msaliti ukimtazama mbele na hapo ndipo utata unapoanza na kupelekea kukata kwa mawasiliano.Kwa wengi, maumivu ya usaliti ni mbaya zaidi kuliko ukatili wa kimwili, udanganyifu, au chuki.
Usaliti huharibu msingi wa uaminifu kwa kiasi kikubwa mwishowe upelekea migogoro. Chukua hatua acha ,fikiria kabla ya kutenda wape nafasi wengine.Wish you all the best let's meet on the next discussion.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Wasiliana namimi 0767702659
Kupata makala zaidi Instagram Lackius Robert

No comments:

Post a Comment