Friday, August 09, 2019

Usipite njia ya mkato

MORNING MOTIVATION DIARY

Usipite njia ya mkato

Ndugu,
Karibu katika siku nyingine tena ambapo tunakuatana katika program ya morning motivation diary ,yenye lengo kubwa la kukuongezea maarifa na kuing'alisha siku yako

Katika ulimwengu huu ukitaka  mafanikio ,haupaswi kupita njia ya mkato ili kuyafikia mafanikio hayo.Licha ya kwamba kuna usemi unaoitwa ukitaka kujua njia ya mkato kula nauli.

Unapokuwa na haraka, utafanikiwa ndio lakini mara nyingi ,Njia za mkato huwa na madhara, hasa unapokatisha kwenye ubora wa kile unachofanya.Kwa sababu unakuwa hauna maandalizi mazuri ikiwemo ujuzi,maarifa,changamoto n.k.Kwa kupitia njia sahihi zitachukua muda  kukamilisha jambo lakini ndo ukweli.Ukishakamilisha autahitaji gharama kubwa ikiwemo nguvu n.k

Tuwematazama ndugu ,marafiki wenzetu waliotaka kufanikiwa haraka walivyojiingiza katika matendo mabaya ikiwemo wizi,Uuzaji wa madawa ya kulevya ,Utekaji,ukahaba n.k pia yaliyowakuta baadhi tumeyaona.Malengo yao makubwa ni kutaka kufanikiwa haraka na kwa kipindi kifupi.
Tukumbuke hata mbuyu ulianza kama mchicha,ukiutazama umbo lake ukubwani uwezi amini kama umetokea kwenye umbo dogo.Hivyo mafanikio ya kweli na mazuri ni yale yenye maandalizi muda mzuri wa kutafakari,kujipanga na  kupitia njia sahihi za kuaminika.Jifunze ,elimika,Fanya kazi kwa bidii,usiubanie uwezo wako mafanikio ya kweli utayapata katika njia ya kweli.Wish you all the best.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kwa maelezo zaidi 0767702659
Kwa makala zaidi tembelea page yangu ya Instagram Lackius Robert
Karibu.

No comments:

Post a Comment