Sunday, August 11, 2019

Ujue zaidi mgogoro

MORNING MOTIVATION DIARY

Overview kuhusu migogoro

Ndugu,
Migogoro kama tulivyoona Kwenye makala iliyopita kuwa ni uwepo wa uhasama,kutoelewana au kutofatiana kinawazo au kimahitaji baina ya mtu mmoja au zaidi.Zipo aina mbali mbali za migogoro ,ikiwemo migogoro binafsi(intrapersonal conflict)mtu na mtu (interpersonal conflict),Familia(family conflict) ,Nchi na nchi kwa upande wa  kiuchumi,kisiasa kijamii na  kiutamaduni.
Lakini pia kuna migogoro sehemu za kazi(Workplace/Organization conflict).

Licha ya kuwepo aina nyingi za migogoro lakini napenda kuelezea tu Kwenye migogoro ya kifamila (family conflict )na migogoro kazi(workplace conflicts).

Nianze na migogoro ya kifamilia(Family conflicts):
Hii ni migogoro inayokea kutokana na uwepo wa mivutano kati ya wanafamilia baba,mama pia watoto au ndugu.
Taaaisi ya The Better Health Channel ya Australia 2019 baada kufanya utafiti kutokanana watu inaowahudumia wanasema wakati mwingine mgogoro hutokea kutokana na uwepo wa kutoelewana baina yao na kurukia hitimisho ambayo siyo nzuri yaani wrong conlusion.Kwa maana ya kwamba wabashindwa kuelewana hivyo hukimbilia hitimsho lisilo sahihi hali ambayo upelekea mgongano kuendelea.

Utafiti unaonesha migogoro ni kitu cha asili kipo,hivyo ni  sehemu ya maisha hata kwa mtu mmoja na familia pia maana familia inaundwa na watu. Hivyo isipotatuliwa kwa amani na itaendelea kuwa inatokea tokea.
Mfano unapokuwa njiani unatembea pindi ukijikwaa bila kujua taarifa zinaenda haraka kwenye ubongo ,kuna hali fulani ya maumivu unayasikia na unachukua dakika kadhaa kurejea katika hali yako ya kawaida.Hivyo ndivyo ilivyo wakati mgogoro umepamba moto
.Ndiyo maana kuharibu mahusiano kwa Sababu mmoja wapo hushindwa kuthibiti hisia zake na kuanza kulumbana na pengine kupigana.Baadhi ya visababishi kwenye familia ni kupeleka watoto shule,Kuzaa mtoto mwingine mfano nje ya ndoa,Kazi za Masafa marefu,magonjwa.

"Ushindi upo mikononi mwako kwa kuwa umebarikiwa".

Kupata makala zilizopita tembelea ukurasa wangu wa Instagram Lackius Robert au wasiliana nami 0767702659

No comments:

Post a Comment